Nimeishi Moshi, Bukoba, Lushoto aisee watanzania tuna ukarimu sana tofauti na tunavyoshambuliana kwa tofauti zetu

Tanzania sehemu nyingi Tu unaishi kama hutokuwa mjivuni na kiburi,

Na kama vijijini ndio rahisi, unawaonesha Tu kuwa umependa tamaduni zao na kuwanogesha zaidi unajitahidi kujifunza hata lugha yao. Watakupenda haswaaa

Ila Kuna wengine hasa wale born town, unaenda uhayani, uchagani, usukumani, ungonini au kabila yoyote ile maarufu. Kwa
fikra zako mbovu za kuskia, unaanza kuwakejeli na kuvimbia wenyeji,

Nikuambie tu, wakikukomesha unastahili
 
Nimebahatika kufanya kazi karibu wilaya zote Tanzania nzima Ila mkoa wa Tanga pamoja na wilaya zake zote toka kilindi, kwediboma, Handeni, Korogwe, Lushoto, muheza, tanga mjini Mpaka Mkinga kwa wadigo ndo the best place kwa kuishi na watu wakarimu. Nimetembea Tanzania nzima Ila hakuna sehemu nzuri unayoweza kuishi kwa Raha na amani kama Tanga.
Ukikaa Tanga huwezi kupachoka miaka 800 na usipokuwa makini unaweza amia mazima Kama ww ni mgeni.
 
Nenda pale saloni kwa mndengereko ukanyoe!!
 
Nipo Arusha sina ndugu hata mmoja ninaye mjua huu mkoa lakini najihisi nipo nyumbani.

🇹🇿❤️
Arusha ukiwa mgeni na haujaja kuleta competition na biashara/mbishe za watu utaishi fresh tu,yaani unatakiwa kua fala flani hivi ili uishi fresh.Lkn ukija Kama mpambanaji na umeleta competition ya maana utaukimbia huu mji.

Nimeongea Kama mzaliwa na mwenyeji wa hapa.
 
Unaposema mgeni unamaanisha nini?
Mtu asiye kabila la hapa ama mhamiaji yeyote?

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha wahaya walikuchangamkia bila shaka walikuwa after something.
 
Hii ndio maana iliitwa bongo ukizubaa unapigwa chap kwa ukali😅
 
Kweli kabisa, mfano wilaya ya karagwe full kilugha hata maofisini na wakijua sio wa uku wanakasirika. Wabaguzi sana
Ukiona hupendwi na jamii nzima ujue wew ndo una kasoro..


Huko uhayani ukiwa mjivuni na mwenye dharau hakuna atakayekukubali tu...

Wew ndo una matatizo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Bukoba ulisha fanya nao kazi ofisini ukajua usemacho? Kilimanjaro pia changanya na waMeru. Sehemu pekee inakaribisha wageni pasi kuwabagua ni Kanda ya Usukumani na Kusini, kila mtu hua ana lake la kusema na tukitaka kusema hapa tutazua mjadala mkubwa usio na faida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…