Naunga mkono hoja yako pal, Zawadi kubwa tuliyopewa watanzania inawezekana kuliko hata waafrika wengine ni Upendo na ukarimu, Watanzania ni wakarimu mno nahisi ndio sababu ya umaskini wetu.
Mwanzo nikienda vijiji vya mkoa wetu jinsi majirani wanavyotupokea na kutupa vyakula nilikia najua ni mkoa wetu ndio wakarimu sana kumbe ni karibu mikoa yote. Mikoa yote niliyokua naishi nimeshuhudia upendo na ukarimu wa watanzania tena sehemu hizo unakuta hauna ndugu kabisa ila Unaishi kwa amani. Eg, Usukumani, Unyaturuni, Wandengereko, Wachaga/Masai nimekaa kwa raha sana, Wanyakyusa pia wakarimu sana asee..
Zanzíbar watu ni wakarimu sana ghalama ya kupata kitu chochote kwa Shamba ni kusema "naomba" Shida yao sometimes udini unawameza kiasi but nao wakarimu sana.
Dar ndio wwtu wanaishi kama magaidi ukipanda gari kila mtu anamuona mwenzake Mwizi, hata ukiulizia njia hasa maeneo ya Ubungo, kino,temeke, ilala Ndio kwanza mtu anakutafutia chance ya kukuibia/tapeli.