Nimeishi Moshi, Bukoba, Lushoto aisee watanzania tuna ukarimu sana tofauti na tunavyoshambuliana kwa tofauti zetu

Nimeishi Moshi, Bukoba, Lushoto aisee watanzania tuna ukarimu sana tofauti na tunavyoshambuliana kwa tofauti zetu

Aisee nimejifunza kitu kimoja kuhusu sisi watanzania baada ya kutembea mikoa tofauti na kuishi huko. Watanzania tunaweza kuwa tunatofautiana na kurushiana maneno mitandaoni juu ya sijui kabila fulani, hivi mkoa fulani hivi..ila kiuhalisia tunaishia kwa upendo sana.

Ok kiufupi, nimezunguka mikoa mingi..nimeishi Kagera aisee ilikua safi majirani na watu walikua na upendo sana japo sikua mwenyeji.

Nimeishi moshi big up sana kuna wajamaa waliiishi na mimi kama mdogo wao na hata kunisaidia naul kurudi Dar nilipokua hali tete braza George Mramba big up popote ulipo ulinisaidia first day kiuaminifu sana kama mdogo wako.

Unakaribishwa chakula tena unalazimishwa aisee watu wa mikoani big up sana ila na kiujumla watz safi sana.

Lushoto nimeishi Lukozi napo ilikuwa safi sana watu walikuwa wakarimu vibaya mno kama wanakujua. Aisee watz sisi safi sana!
Ulipokuwa Moshi hukuitwa Chasaka??
 
Nimebahatika kufanya kazi karibu wilaya zote Tanzania nzima Ila mkoa wa Tanga pamoja na wilaya zake zote toka kilindi, kwediboma, Handeni, Korogwe, Lushoto, muheza, tanga mjini Mpaka Mkinga kwa wadigo ndo the best place kwa kuishi na watu wakarimu. Nimetembea Tanzania nzima Ila hakuna sehemu nzuri unayoweza kuishi kwa Raha na amani kama Tanga.
Ukikaa Tanga huwezi kupachoka miaka 800 na usipokuwa makini unaweza amia mazima Kama ww ni mgeni.
wadigo ndio best kwa Tanzania kwa ukarimu wanapenda wageni noma akifika mgeni hata kweny myu,na ya ,akuti atapikiwa bilyani
 
Arusha ukiwa mgeni na haujaja kuleta competition na biashara/mbishe za watu utaishi fresh tu,yaani unatakiwa kua fala flani hivi ili uishi fresh.Lkn ukija Kama mpambanaji na umeleta competition ya maana utaukimbia huu mji.

Nimeongea Kama mzaliwa na mwenyeji wa hapa.
Nimesoma na jamaa wa chuga si fichi ni wabaguzi mno mbaya walikuwa wachache mpaka wakawa wanagombana na watu wa dar makundi daily maisha ya boarding bhana
 
Bukoba ulisha fanya nao kazi ofisini ukajua usemacho? Kilimanjaro pia changanya na waMeru. Sehemu pekee inakaribisha wageni pasi kuwabagua ni Kanda ya Usukumani na Kusini, kila mtu hua ana lake la kusema na tukitaka kusema hapa tutazua mjadala mkubwa usio na faida
mi nimefanya na wachaga ni wabaguzi kiasi fulani haswa mtu hawezi kumtakia mwenzie hbd mpaka aandike mara chugaboy mara chaga boy mtu alifunga tu kuna mechi wanampost eti wanyumbani
😀 😀 😀
 
Sijaona kabisa MTU akiiongelea iringa........wale jamaa ndo definition ya ukarimu kwa kweli


Nilitoka zangu huku kaskazini kwetu kwenda KJ 841 nilivyopokelewa na watu ambao siyo ndugu zangu na hatujuani mm mwenyew nilinyoosha mikono juu
 
Wa huko Dar wamejaa roho mbaya na umaskini kiasi kwamba ukiwatembelea wanakuuliza unaondoka lini? Cha ajabu hapo umeshawabebea debe la mchele, maharage na mandizi yakutosha.
Halafu wakija mikoani wanaomba na nauli ya kurudia
 
Arusha ukiwa mgeni na haujaja kuleta competition na biashara/mbishe za watu utaishi fresh tu,yaani unatakiwa kua fala flani hivi ili uishi fresh.Lkn ukija Kama mpambanaji na umeleta competition ya maana utaukimbia huu mji.

Nimeongea Kama mzaliwa na mwenyeji wa hapa.
Tobaaaaaa... "... Ukija kama mpambanaji na kuleta competition utaukimbia huu mji...". Duuuuuh
 
Nina mashaka kama wanaocomment washawahi kufika bukoba.
Maana kungekuwa hakukaliki almost asilimia kubwa ya bar zilizoko bukoba mjini za wachaga, maduka ya vyakula ya wachaga na bado watu wanakunywa pombe na kununua kama.kawa.
Wachagga wamejenga bukoba mjini, aliyekuwa anauza bia kwa jumla bkb mjini alikuwa mchaga sina hakika kwa sasa na alikuwa anamiliki bar kubwa hapo.
Watu uwa wanasema wahaya wanaongea kilugha tu, lakini hii nimeiona mikoa mingi.
Kuna kipindi nimekaa kahama full kisukuma.
Ila wasukuma wakarimu sana sana na wachapa kazi.
Mwaka jana nimeenda bukoba vijijini nikashangaa kuan wasukuma wanalima.mpunga maana bukoba hakukuwa na kilimo cha mpunga nikashangaa mashamba ya mpunga.
Tz kokote unaweza kwenda ukaishi fresh tu
Hio sentensi ya mwisho ndio ime summarize content ya post yako. Tanzania hii unaishi popote tu, sio ajabu ukamkuta Mhaya pale Mpanda Katavi, na si ajabu kukuta Moemba akiwa na duka Kyela Mbeya.
 
Hio sentensi ya mwisho ndio ime summarize content ya post yako. Tanzania hii unaishi popote tu, sio ajabu ukamkuta Mhaya pale Mpanda Katavi, na si ajabu kukuta Moemba akiwa na duka Kyela Mbeya.
Kabisa mkuu. Kuna jamaa yangu yuko katavi alikuwa anaishi dar akapata kazi wakamrusha huko. Anakwambia katu harudi dar now mwaka wa pili keshanunua eneo anataka anza kujenga.
Ukabila upo ila sio kiasi hicho.
 
Ebu kajaribu zenji..uje utupe mrejesho..nenda huko vijijini halafu uanze kula mdudu ndio utajua tz hakuna amani bali utulivu.

#MaendeleoHayanaChama
Sasa unaona matatizo yako, unataka kuwapelekea nguruwe wakati kwao ni haramu? Wewe kauze urojo kama utamwona mtu yeyote ana muda wa kukubagua.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kweli, wapo wakarimu Sana ila usipokuwa mhaya Kuna jina utaitwa.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Mnyamahanga? Halafu sio tusi maanake ni mtu wa sehemu nyingine. Hata ukiwa mkoani wanasema uko kwenye mahanga. Hauko nyumbani. Ni sawa na watu wa dar wanavyosema watu wa mikoani haina tofauti kabisa.
 
Lushoto sawa
Moshi sawa
Lakini Bukoba? Mhhh Bukoba ipi wewe ulikwenda?
Isije ikawa unaongelea mtaa wa Bukoba hapo Manzese nyuma ya Bakhresa.
Bakini na ukabila wenu kuwahukumu hata ambao hawajawai kuwakosea kisa kabila ila msisahau siku ya mauti kila nafsi itahukumiwa kutokana na mzigo wake wa dhambi.

Tusisahau hakuna aliveyekua na option ya kuchagua kabila
 
Back
Top Bottom