Nimeishi na mwanamke miaka mitatu bila kupata mtoto, nifanyaje

Kama una shida umekaa miaka mingi hupati mimba na hospital umeenda umeambiwa hauna shida HANGAIKA, UTAFANIKIWA
 
Wataalamu wa masuala ya afya walisema HATUNA SHIDA YOYOTE
Hamna shida yoyote na hamzai?shida ipo.

Nakushauri tumieni dawa asili..kama upo desperate sana na watoto kaze nje au ongeza mke wapili uendeleze uzao wako.
 
Hamna shida yoyote na hamzai?shida ipo.

Nakushauri tumieni dawa asili..kama upo desperate sana na watoto kaze nje au ongeza mke wapili uendeleze uzao wako.
Moshi mweupe umeanza kuonekana, natulia kwanza NITALETA UPDATE KUSAIDIA NA WENGINE, KUHUSU DAWA ZA ASILI UMEONGEA POINT KUBWA SANA.
 
10% walinishauri ushauri ambao unaweza kunisaidia.

90% wengi walinishauri vibaya na kunikejeli

Mungu Yupo na Uchawi pia upo.
 
Kwa maelezo yako huyo mke wako atakua kafungwa sio ugonjwa wa hospitali, ndio maana hospital vipimo vinaonyesha mpo sawa.
 
Matokeo ya jambo hayaji kama kushiba ukila chakula (ghafla)

Pengine unachelewa kupokea hitaji kwasababu hauna msimamo na una pupa sana.

Ushauri wangu: chagua eneo moja la kushughilika nalo iwe maombi au kwa waganga (imani) ama hospital. Tulia na ustick hapohapo hata kwa mwaka mzima utaona matokeo
 
Post ya mwaka jana hiyo, hujui sasahivi imeakuaje, subiri update nmesema nitaandika, pia unahangaikaje hospital wakati kote umeshaenda hadi hospital za gharama umeambiwa hakuna tatizo kabisa kwa wote wawili?
 
1. Haujatuambia ulikutana na mkeo mazingira gani na akiwa na umri gani? Gari iliyotumika sana au aliyofanyishwa kazi ngumu ndani ya muda mfupi huwa inakuwa na changamoto za kiutendaji na higher maintenance costs. (Siongelei magari hapa).

2. Ninyi kwasasa mnajamiiana hamfanyi mapenzi. Mwili unatakiwa kuwa katika hali ya utulivu na focus kuweza kutenda vema. Wewe una struggle na mkeo kutafuta mtoto miili yenu ina tension haijawa relaxed. Ndio shida ya kutafuta mtoto wa kwanza umri ukiwa umeenda.

3. Jambo la mwisho, wewe umetaka mtoto na huu ni mwaka wa tatu umekosa ila bado haujamkatia tamaa mkeo na umeendelea kuwa nae bega kwa bega ukimjali na kuendelea kuishi nayo ingawa unayo nafasi na haki ya kwenda nje kutafuta binti mbichi au wanawake wengine uzae nao kwa siri bila hata kumwambia chochote, sikwambii umuache mkeo,ila nakuuliza je, wewe ungekosa kazi na kipato kwa muda wa miaka 3 angeendelea kuwa Loyal kwako na kujikana tamaa zake za kukutoroka huku mkiendelea kubaki na kuishi pamoja? Pengine MUNGU anakwambia kitu wewe binafsi kuhusu huyo mkeo ila haumsikilizi.
 
Nilimtoa kwao akiwa na miaka 22

Hayo mengine tuyaache kwani uzi wa mwaka jana
 
Shida mna stress wote kwasababu ya kutaka mtoto. . Chakufanya mnatakiwa mtafute kitu mnacho furahiya kufanya kwa pamoja. Halafu focus kufurahishana na sio kutafuta mtoto. Kwanini statute mchepuka wa kuzaa naye ila usimwache mke wako ili angarau ujuwe tatizo liko upande gani. Hao wataalamu huwenda hata hawajui chochote wanakwambia tu unachotaka kusikia.
 
Post ya mwaka jana hiyo, hujui sasahivi imeakuaje, subiri update nmesema nitaandika, pia unahangaikaje hospital wakati kote umeshaenda hadi hospital za gharama umeambiwa hakuna tatizo kabisa kwa wote wawili?
Haya ni madhara ya kuomba ushauri huku ukiwa umeshapanga matokeo. Ungekuwa unahitaji ushauri huku ukiwa neutral ungeelewa dhamira yangu
 
Hio hali nilishawahi pitia, nachotaka kukwambia kama Mungu alikupangia kupata mtoto utapata. Acha kuhangaika kwa waganga, wewe amini ipo siku utapata mtoto.

Mimi na Wife tuliacha kuwaza hili jambo na Mungu akatujaalia siku ilipowadia. Nilihangaika kama wewe ila mwisho niliachana na hayo mambo.

Kuna mdau aliwahi sema humu ukiona unachelewa kupata mtoto, huwezi jua huyo anayekuja Mungu kamuandaa kufanyika baraka na kubadilisha maisha yenu. Kama wadau wengine walivyokushauri ukiachana na kuwaza hili jambo na ukaamini ipo siku utapata, utapata mtoto
 
Em jazia nyama hapo kwenye ujanani ushatia sana watu mimba
Hizo mimba nini kilihappen?ni ngapi?
Unalea?
Hao babymama?wana hali gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…