Nimeishi na mwanamke miaka mitatu bila kupata mtoto, nifanyaje

Nimekuja hapa JamiiForums kuomba ushauri na msaada Kwa namna moja au nyingine, hapa nimekuwa nikisoma tu nyuzi za watu nilikuwa sina account na mimi nimeona nijiunge nitoe yanayonisibu labda nitapata msaada, hapa naamini ni sehemu sahihi japo kuna ambao sometimes wanaleta masikhara.

Ishu inayonisumbua ni kwamba nimekaa na mwanamke kwasasa takriban Miaka mi3 hatujafanikiwa kupata mtoto.

Tulishakwenda hospitali kupima wote tukaonekana tupo sawa hatuna shida (hospitali special za uzazi) pia mimi kwenye pita pita zangu maisha ya nyuma huko nishawahi kutia sana wanawake mimba.

Harakati zetu za kutafuta mtoto zilianza baada ya kukaa Kwa mwaka mzima bila mwanamke kupata ujauzito, ndio akaanza na dawa za kupevusha mayai na za hormone imbalance (hii ni baada ya kupima hospitali kuambiwa hatuna shida akashauriwa atumie hizo), baada ya kuona mwaka wa pili unaingia bilabila ikabidi tuhamie kwenye dawa za kienyeji za chango, kanywa Sana Lakini hatukupata matokeo.

Tukahamia Kwenye kuombewa, manabii, wachungaji wa madhehebu karibia YOTE ya kikristo ashaombewa, ilifika kipindi maji ya kunywa na mafuta ya kupikia tulikua tunachukulia Kwa mwamposa.

ikabidi sasa nitafute mtaalamu japokuwa hayo sio mambo yangu, nijaribu kuchekiwa(ramli) ili nijue Kwa upande wa pili kama kuna shida yoyote.

Hapa sasa ndio nikaja kuamini kuwa uchawi upo, niliwasiliana na mtaalamu wa kwanza (namba zake nilipewa na mshkaji wangu), nikamtumia majina yetu wote watatu ili aangalie nani ana shida, nilipomtumia baada ya nusu saa akanipigia akaniambia kaangalia kwa upande wangu hakuna shida ila tatizo lipo Kwa mwanamke amefungwa, akanielezea kama kuna ndoto anaota usiku nikamwambia ndio, akaniambia ana kitu cha kichawi kimefunga uzazi.

Kwakweli sikuamini, nikahisi labda huyo Mtu ananichezea akili, huyo anakaa mikoa ya kaskazini ikabidi nitafute mwingine wa mkoa tofauti kabisa (Mimi nakaa Dar).

Nilipotafuta mwingine wa mkoa tofauti, maajabu ni kwamba ALINIAMBIA KITU KILEKILE KAMA HUYO WA KWANZA😳, nilishangaa Sana nikahisi hawa watu wanajuana wanaambiana au?! Lakini mbona ni watu hawajuani kabisa??! Na wanakaa mikoa ya tofauti kabisa??

Sikuridhika na majibu ya hao wawili japo yanafanana, NIKATAFUTA MWINGINE WA TATU kutoka mkoa mwingine (wote hawa ni wale wanatibu kiarabu, masheikh)

Huyu wa tatu nae alinipa majibu yaleyale kama ya wale wawili wa mwanzo, hapo ndio nikaamini, nikachukue hatua ya kwenda kwa yule wa kwanza ili huyu mwanamke atibiwe.

Kufupisha story, baada ya kwenda kutibiwa Kwa huyo wa kwanza, akapata nafuu Kwa kutokuota ndoto mbaya Kwa miezi mitatu tuu lakini mimba haikushika, baada ya miezi mitatu ndio ikawa kama tumechokoza kwani alikuwa akiota ndoto za kutisha mara nyingine anaota anaingiliwa.

Nilienda Kwa wote hao lakini HATUKUFANIKIWA, na pia nilienda Kwa wataalamu wengine nao wakaniambia amefungwa, tukajaribu na huko lakini hatujafanikiwa mpaka sasa.

Nikiwaza nimuache roho inakua nzito kwani ni Mwanamke alietulia Hana mambo mengi ya kimjinimjini (nilitoka nae mkoani), nawaza kurudi tena kutafuta alietulia kama huyu inaweza kuwa kazi ngumu sana kwa maisha ya sasa hivi.

Naombeni msaada wenu, najua hii kitu wapo waliopitia ambao wapo hapa JF, kwa ambao mlishawahi kupitia hili mkatoboa nakaribisha ushauri.

Tokea nimeanza kuhangaikia hii ishu nimecalculate nimetumia zaidi ya millioni 5 Kwa nauli za kwenda mikoani na kulipa wataalamu.

Kwa upande wa Imani Sisi ni wakristo na yeye anazingatia maombi hata Mimi kumpeleka Kwa wataalamu ilikuwa mbinde kwani alikua haamini hayo mambo, ikumbukwe ashaombewa sana, kwa manabii na wachungaji pia tulishaenda sana tulipooona hamna suluhisho ndio tukaanza kwenda upande wa pili.

Kama kuna Mtu atanipatia suluhisho la kunipa connection ya mtaalamu wa uhakika ambae atamtibia akishapona ndio tunalipa nitashukuru Sana, atakaenipa hiyo connection kama akitibika kweli nitampatia hata 500K ya maji.

Mambo haya yanaumiza, hapa nilipo Niko makazi mapya, tulipokua tunakaa mwanzo tuliondoka kwasababu ya maneno ya watu.

Haya mambo yanaumiza vibaya mno, kunajirani yangu alishawahi Kukaa Miaka 10 ndio wakafanikiwa, kuzaa nnje ya ndoa ndio kitu sijakifiria kabisa.

NATAMANI WAJITOKEZE WATU AMBAO WASHAPITIA HUU MSOTO TUPEANE EXPERIENCE NA NAMNA WALIVYOJINASUA.
Huyo kafungwa au kulogwa na mama yake mzazi nendeni mkamweleze mama yake juu ya shida anayopitia mwanaye ni lazimq anafahamu chanzo cha mwanaye kutokuzaa bila hivyo hata muhangaike vipi mtamaliza waganga na hatokuja kuzaa maishani mwake yaani hata aombe vipi hawezi kufanikiwa maana Kuna mtu ameshikilia nafasi yake
 
Connection Kaka naomba kama unao manguli unaowajua
Mambo ya uchawi yapo ! Hapo kosa la tiba kwa mkeo ni kwamba hana KINGA baada ya kutibiwa.
Majini na uchawi ni wabishi sana. Ukitibu wanarudia kwa Kasi.
Fanya kumtibu kisha anafanyiwa Kinga either ya kuvaa au kuchanja.
 
Huyo mkeo ulikutana nae akiwa bikira? Kama jibu ni hapana. Unaijua background yake(ulikua unaona maisha anayoishi au umepewa taarifa na chanzo chako cha kuaminika) kabla haujakutana nae?. Fuatilia historia yake uenda maisha yake ya nyuma alishaaribu kizazi kwa abortions au kumeza p2.

Suala la kwenda hospitali jaribu pia kwenda kwenye hospitali nyingi au nenda kwenye hospitali ambayo dokta atakayewahudumia unajuana nae. Masuala ya uzazi uko mahospitalini mara nyingi ethics za kazi zinawataka wauguzi kuficha taarifa nyeti za mwanamke mfano ugumba au kubambikizia mimba waume zao hili kunusulu ndoa na watoto.

Suala jingine akikisha unafanya sex na mkeo kila siku kuanzia siku mbili kabla hajaingia kwenye siku za hatari na wakati wa tendo tumia style ambayo ni rahisi sperm zako kuingia kwenye mji wa mimba(kifo cha mende ina ufanisi zaidi). Ukiwa unamwaga usipige zile in-out badala yake stopisha mashine kule kule ndani kwenye mlango ambao uke unaishia mpaka bao lote liishe, baada ya hapo akikisha mkeo analala chali kwa angalao dakika 15 ili sperm ziweze kushuka kwenye mji wa mimba
 
😃😃😃😃😃😃😃😃 Ushauri mzuri sana huu
 
Mambo ya uchawi yapo ! Hapo kosa la tiba kwa mkeo ni kwamba hana KINGA baada ya kutibiwa.
Majini na uchawi ni wabishi sana. Ukitibu wanarudia kwa Kasi.
Fanya kumtibu kisha anafanyiwa Kinga either ya kuvaa au kuchanja.
Kweli mkuu
 
Huyo mkeo ulikutana nae akiwa bikira? Kama jibu ni hapana. Unaijua background yake(ulikua unaona maisha anayoishi au umepewa taarifa na chanzo chako cha kuaminika) kabla haujakutana nae?. Fuatilia historia yake uenda maisha yake ya nyuma alishaaribu kizazi kwa abortions au kumeza p2.

Suala la kwenda hospitali jaribu pia kwenda kwenye hospitali nyingi au nenda kwenye hospitali ambayo dokta atakayewahudumia unajuana nae. Masuala ya uzazi uko mahospitalini mara nyingi ethics za kazi zinawataka wauguzi kuficha taarifa nyeti za mwanamke mfano ugumba au kubambikizia mimba waume zao hili kunusulu ndoa na watoto.

Suala jingine akikisha unafanya sex na mkeo kila siku kuanzia siku mbili kabla hajaingia kwenye siku za hatari na wakati wa tendo tumia style ambayo ni rahisi sperm zako kuingia kwenye mji wa mimba(kifo cha mende ina ufanisi zaidi). Ukiwa unamwaga usipige zile in-out badala yake stopisha mashine kule kule ndani kwenye mlango ambao uke unaishia mpaka bao lote liishe, baada ya hapo akikisha mkeo analala chali kwa angalao dakika 15 ili sperm ziweze kushuka kwenye mji wa mimba
ALikua Bikra nilimchukua alivyomaliza 4m4, tushawah kufanya kila siku mwezi mzima lakin wap
 
Huyo kafungwa au kulogwa na mama yake mzazi nendeni mkamweleze mama yake juu ya shida anayopitia mwanaye ni lazimq anafahamu chanzo cha mwanaye kutokuzaa bila hivyo hata muhangaike vipi mtamaliza waganga na hatokuja kuzaa maishani mwake yaani hata aombe vipi hawezi kufanikiwa maana Kuna mtu ameshikilia nafasi yake
Asante Kwa ushauri mkuu
 
Pole sana mkuu, hicho ni kilio cha wengi japo kinaliliwa kimyakimya hakuna kutoa sauti.
Wakati wa Mungu ni wakati sahihi miaka mitatu siyo michache pia siyo mingi sana jipe muda na upunguze pressure,epuka sana kusikiliza ya majirani mtachanganyikiwa maradufu kila mtu na wakati na majira yake ya kufanikiwa kwa jambo lake. Epuka sana pressure za ndani na za nje.
 
Achana na mambo ya ramli na waganga, huko utaliwa pesa na kitakachofuatia mkeo ataambiwa alale na mganga kama dawa ya kupata mimba. Kuna waganga wapuuzi wanamwambia mkeo hiyo dawa inabidi waiingize ukeni kwao kwa njia hiyo kwa hivyo usipokuwa makini utaziniwa mkeo na waganga. Na kwa sababu wanawake wengi wako desperate atakubali na hatakwambia

Wewe ni dini gani? Lakini amka usiku mida ya saa 9 au kumi kisha sali muombe Mungu. Fanya hivi mara kwa mara. Mwenyezi Mungu anajibu dua za watu na insha Allah atawajibu na nyinyi. msiache kuomba.
 
Ngoja tusubiri, maana MPAKA SASA MIMI MWENYEWE SIAMINI.
 
Pole sana mkuu, hicho ni kilio cha wengi japo kinaliliwa kimyakimya hakuna kutoa sauti.
Wakati wa Mungu ni wakati sahihi miaka mitatu siyo michache pia siyo mingi sana jipe muda na upunguze pressure,epuka sana kusikiliza ya majirani mtachanganyikiwa maradufu kila mtu na wakati na majira yake ya kufanikiwa kwa jambo lake. Epuka sana pressure za ndani na za nje.
Sawa mkuu lakini kukaa tuu bila kuhangaika ukimtegemea Mungu sahau kuhusu mafanikio
 
1.mruhusu kuchepuka ipo siku utaamini hajafungwa ila kuna factor hukizi,
2.Kama anaweza aje nimbebeshe mimba ya kwanza mimi,ila gharama za nauli na kulala juu yenu,
JF ina ujinga mwing sanaaaa
 
Wasioamini kwenye nguvu za giza na ushirikina ni suala na mda tuu, IPO SIKU YATAWAKUTA
 
KAMA UNA TATIZO LA UZAZI USIMUOMBE USHAURI KWA MTU AMBAYE HANA SHIDA HIYO AU HAJAWAHI KUPITIA HIYO CHANGAMOTO, ATAKUPA USHAURI WA KIJINGA NA KUKUKATISHA TAMAA TUU
 
Back
Top Bottom