Nimeishiwa nguvu na nimekuwa Mtu mwenye kukata tamaa kwa Mkasa ulionikuta

Nimeishiwa nguvu na nimekuwa Mtu mwenye kukata tamaa kwa Mkasa ulionikuta

Moniel

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2020
Posts
274
Reaction score
603
Wakuu habarini!
Nimekuja kwenu naomba nisaidiwe kimawazo na ushauri.

Hivi karibuni nilipeleka barua ya uchumba (posa ) na Mambo yalienda freshi tu. Kikao Cha kupangiana mahari makubaliano yalikuwa kifanyike ijumaa hii. Nimejikuta nina mawazo Sana kwani hela niliyoiandaa kwa ajili ya kuitolea mahari kiasi Cha 700,000 nimekitumia chote kutokana na mkasa ulionipata pasipo kutegemewa jana usiku.

Hipo hivi, Mimi ni dereva bajaji DSM nilijikuta nimeikwaruza gari ubavuni na kuivunja taa ya kulia maeneo ya round about. So mwenye gari akaniamuru ili tusifikishane mbali nimlipe kiasi Cha sh. 650,000 ili akafanye matengenezo ya gari lake, vinginevyo atachukua hatua za kisheria kwani makosa yalikuwa ni yangu. Hivyo nikamlipa.

Nahisi kukata tamaa, kikao ni jumatatu na Sina mpango wa kupata hela nyingine kwa Sasa. Wazee wangu wapo mikoani hivyo hapa town nawatumia wazee tu wa kujuana, na ninaogopa hata kuwaambia kwani watahisi nafanya usanii.

Hivyo nilikua nauliza, Je itawezekana kwenda ku bargain mahali tu kwa sasa hiyo siku, then nitalipa siku nyingine? Hata baada ya mwezi? Au ni lazima kwenye kikao hicho watanitaka kulipa hela kidogo?

Kama Kuna mtu mwenye uzoefu au utaalamu na haya Mambo naomba anisaidie kimawazo au ushauri

Ahsante!

Moniely
Dsm.
 
Unaenda kulipa mahari ili iweje??

Umlipie mahari,
Umlishe,
Umvishe,
Umjengee makazi,
Umsomeshee watoto,
Umfikishe kileleni. N.k

Mwanaume anamajukumu mengi kwenye ndoa, hicho Kiasi kilipaswa kiwasaidie kuwainua nasio kutumika kuwarudisha nyuma wewe na mkeo mtarajiwa.

Huu utamaduni hauendani na mazingira ya sasa, zamani familia zilikuwa zinamiliki mifugo mingi ilikuwa rahisi kufanya hivi. Sasa hivi familia nyingi ni masikini kuendeleza huu utamaduni ni kuendelea kupalilia umasikini
 
Mahari hulazimiki kulipa siku hiyo. Labda makabila yanatofautiana. Kabila letu sisi utalipa utakapopata kabla ya kumchukua binti.

Tena hulazimiki kulipa yote. Ukilipa kiasi, nyingine utalipa kidogo kidogo mkiwa kwenye ndoa.

Pole sana na kuwa makini huko barabarani.
 
Back
Top Bottom