Nimeishiwa nguvu na nimekuwa Mtu mwenye kukata tamaa kwa Mkasa ulionikuta

Wakuu habarini!
Nimekuja kwenu naomba nisaidiwe kimawazo na ushauri.

Hivi karibuni nilipeleka barua ya uchumba (posa ) na Mambo yalienda freshi tu.
Kikao Cha kupangiana mahari makubaliano yalikuwa kifanyike ijumaa hii.
Nimejikuta Nina mawazo Sana kwani hela niliyoiandaa kwa ajili ya kuitolea mahari kiasi Cha 700,000 nimekitumia chote kutokana na mkasa ulionipata pasipo kutegemewa jana usiku.

Hipo hivi, Mimi ni dereva bajaji dsm nilijikuta nimeikwaruza gari ubavuni na kuivunja taa ya kulia maeneo ya round about. So mwenye gari akaniamuru ili tusifikishane mbali nimlipe kiasi Cha sh. 650,000 ili akafanye matengenezo ya gari lake, vinginevyo atachukua Hatua za kisheria kwani makosa yalikuwa ni yangu. Hivyo nikamlipa.

Nahisi kukata tamaa, kikao ni jumatatu na Sina mpango wa kupata hela nyingine kwa Sasa.
Wazee wangu wapo mikoani hivyo hapa town nawatumia wazee tu wa kujuana, na ninaogopa Hata kuwaambia kwani watahisi nafanya usanii

Hivyo nilikua nauliza , je itawezekana kwenda ku bargain mahali tu kwa sasa hiyo siku, then nitalipa siku nyingine ? Hata baada ya mwezi?
Au ni lazima kwenye kikao hicho watanitaka kulipa hela kidogo?

Kama Kuna mtu mwenye uzoefu au utaalamu na haya Mambo naomba anisaidie kimawazo au ushauri

Ahsante!

Moniely
Dsm.
Kama nakuona vile unavoenda kubargain
 
Tafuta pesa ya kuwakimu na kuwasafirisha wazee wako wa mjini, kisha wapatia hata 100,000 kwaajili ya kutanguliza posa na wakatihuo watatoa ahadi ya kulipa mahari mwezi wa October au November inakua imeisha hiyo.
Hayo yafanye baada ya kuongea na mke wako mtarajiwa, naamini hakuna kitakacho haribika sababu lazima binti atamshirikisha mama yake changamoto yako.
Zingatia kwasasa ukweni kwako pressure kubwa walio nayo ni wewe kwenda kujitambulisha na kubagain mahari. Yaani saizi kwenda kwako ndio jambo kubwa kwao na sio mahari.
 
Mkuu usiwe na hofu.Ipo hivi, wakati wakujadiliana Mahari watafikia muafaka kuwa Maharibhiyo iwe pesa kiasi Fulani au mifugo au vyote au na baadhi ya bidhaa kama nguo etc. Baada ya hapo wajumbe wa upande wako watawataarifu wale wa upande wa mke mtarajiwa kuwa ngoja wakajipange halafu watawaletea taarifa ni lini watawasilisha Mahari hiyo. Kipindi hicho Cha kujipanga kinaweza chukua hadi miezi 3 na kuendeleza hivyo utakitumia kupata pesa ya kulipa hiyo Mahari. Pia Mahari siyo lazima ilipwe Kwa mara moja bali inaweza kulipwa Kwa awamu. Ahsante
 
Nimekupata mkuu,
Posa tayari ilishaenda mkuu, ilikuwa ni suala la mahari tu na kupatana.
Ntafuata ushauri wa kutoa august
 
Mbona unaogopa wakati hata mahari yenyewe hujafahamu ni bei gani?

Haya mambo ya mahari mara nyingi huwa hailipwi yote, wanaojielewa hufanya hivyo, wale wabishi tunawaacha wadai mpaka wanasahau wenyewe, siku mtoto wao akiwa na mimba tu ndio mwisho wa hizo kelele.

Hapo usiwe na shaka, tafuta kiasi cha kuanzia, hata laki mbili iwepo mfukoni, siku ukienda iwepo, au hata kama haitakuwepo, itafute taratibu, muhimu wakikupa kiasi usisahau kuwauliza namna ya kulipa.

Kama ni mafungu au yote, wakisema yote waambie unaenda kujipanga, ikifika tarehe ya kulipa, toa ile laki mbili ya mwanzo wapelekee waambie yakuanzia.

Hapo wazazi wa mtoto wa kike kama wanajielewa tayari watajua una maanisha kumchukua binti yao, wataiona nia yako, watakuamini, kwasababu wanajua hapa mjini hatushindani kwa pesa, kupata na kukosa yote ni majaliwa tu.

So utaendelea kuwalipa kwa kadri utavyojaliwa, ila hata usipomaliza sio kesi, muhimu tarehe ya ndoa ijulikane ujibebee mtoto mazima, iliyobaki itaenda kumlisha ugali ghetto.
 
Mkuu usiwe na hofu.Ipo hivi, wakati wakujadiliana Mahari watafikia muafaka kuwa Maharibhiyo iwe pesa kiasi Fulani au mifugo au vyote au na baadhi ya bidhaa kama nguo etc. Baada ya hapo wajumbe wa upande wako watawataarifu wale wa upande wa mke mtarajiwa kuwa ngoja wakajipange halafu watawaletea taarifa ni lini watawasilisha Mahari hiyo. Kipindi hicho Cha kujipanga kinaweza chukua hadi miezi 3 na kuendeleza hivyo utakitumia kupata pesa ya kulipa hiyo Mahari. Pia Mahari siyo lazima ilipwe Kwa mara moja bali inaweza kulipwa Kwa awamu. Ahsante
Shukran sana mkuu
Kikubwa sitaki wanione Kama msanii aubabaishaji ndo nachofikiria kwa sasa
 
Wakuu habarini!
Nimekuja kwenu naomba nisaidiwe kimawazo na ushauri.

Hivi karibuni nilipeleka barua ya uchumba (posa ) na Mambo yalienda freshi tu.
Kikao Cha kupangiana mahari makubaliano yalikuwa kifanyike ijumaa hii.
Nimejikuta Nina mawazo Sana kwani hela niliyoiandaa kwa ajili ya kuitolea mahari kiasi Cha 700,000 nimekitumia chote kutokana na mkasa ulionipata pasipo kutegemewa jana usiku.

Hipo hivi, Mimi ni dereva bajaji dsm nilijikuta nimeikwaruza gari ubavuni na kuivunja taa ya kulia maeneo ya round about. So mwenye gari akaniamuru ili tusifikishane mbali nimlipe kiasi Cha sh. 650,000 ili akafanye matengenezo ya gari lake, vinginevyo atachukua Hatua za kisheria kwani makosa yalikuwa ni yangu. Hivyo nikamlipa.

Nahisi kukata tamaa, kikao ni jumatatu na Sina mpango wa kupata hela nyingine kwa Sasa.
Wazee wangu wapo mikoani hivyo hapa town nawatumia wazee tu wa kujuana, na ninaogopa Hata kuwaambia kwani watahisi nafanya usanii

Hivyo nilikua nauliza , je itawezekana kwenda ku bargain mahali tu kwa sasa hiyo siku, then nitalipa siku nyingine ? Hata baada ya mwezi?
Au ni lazima kwenye kikao hicho watanitaka kulipa hela kidogo?

Kama Kuna mtu mwenye uzoefu au utaalamu na haya Mambo naomba anisaidie kimawazo au ushauri

Ahsante!

Moniely
Dsm.

Inawezekana, sema ukweli, ila wakati mwingine komaa hata kama umegonga mtu, hatulegeagi kirahisi hivyo, ukienda kituoni siku 2 utarudi tu mtaani
 
Nimekupata mkuu,
Posa tayari ilishaenda mkuu, ilikuwa ni suala la mahari tu na kupatana.
Ntafuata ushauri wa kutoa august
Wetafuta pesa ya kutumia siku hiyo, then ongea na mkeo mtarajiwa kuhusu changamoto ukilioata. Then nendeni mkapatane mahari bila shaka alafu unawapiga tarehe, na lazima watakubali kwasababu binti atamwambia mamake shida uliopata na mama atamwambia baba, then baba atafanya wepesi
 
Mbona unaogopa wakati hata mahari yenyewe hujafahamu ni bei gani?

Haya mambo ya mahari mara nyingi huwa hailipwi yote, wanaojielewa hufanya hivyo, wale wabishi tunawaacha wadai mpaka wanasahau wenyewe, siku mtoto wao akiwa na mimba tu ndio mwisho wa hizo kelele.

Hapo usiwe na shaka, tafuta kiasi cha kuanzia, hata laki mbili iwepo mfukoni, siku ukienda iwepo, au hata kama haitakuwepo, iweke karibu, muhimu wakikupa kiasi usisahau kuwauliza namna ya kulipa.

Kama ni mafungu au yote, wakisema yote waambie unaenda kujipanga, ikifika tarehe ya kulipa, toa ile laki mbili ya mwanzo wapelekee waambie yakuanzia.

Hapo wazazi wa mtoto wa kike kama wanajielewa tayari watajua una maanisha kumchukua binti yao, wataiona nia yako, watakuamini, kwasababu wanajua hapa mjini hatushindani kwa pesa, kupata na kukosa yote ni majaliwa tu.

So utaendelea kuwalipa kwa kadri utavyojaliwa, ila hata usipomaliza sio kesi, muhimu tarehe ya ndoa ijulikane ujibebee mtoto mazima, iliyobaki itaenda kumlisha ugali ghetto.
Ahsante Sana 🙏🏼 kwa ushauri huu mkuu
 
Wetafuta pesa ya kutumia siku hiyo, then ongea na mkeo mtarajiwa kuhusu changamoto ukilioata. Then nendeni mkapatane mahari bila shaka alafu unawapiga tarehe, na lazima watakubali kwasababu binti atamwambia mamake shida uliopata na mama atamwambia baba, then baba atafanya wepesi
Shukran sana ndugu yangu ✊🏿
 
Back
Top Bottom