Nimeishiwa nguvu na nimekuwa Mtu mwenye kukata tamaa kwa Mkasa ulionikuta

Kama nakuona vile unavoenda kubargain
 
Tafuta pesa ya kuwakimu na kuwasafirisha wazee wako wa mjini, kisha wapatia hata 100,000 kwaajili ya kutanguliza posa na wakatihuo watatoa ahadi ya kulipa mahari mwezi wa October au November inakua imeisha hiyo.
Hayo yafanye baada ya kuongea na mke wako mtarajiwa, naamini hakuna kitakacho haribika sababu lazima binti atamshirikisha mama yake changamoto yako.
Zingatia kwasasa ukweni kwako pressure kubwa walio nayo ni wewe kwenda kujitambulisha na kubagain mahari. Yaani saizi kwenda kwako ndio jambo kubwa kwao na sio mahari.
 
Mkuu usiwe na hofu.Ipo hivi, wakati wakujadiliana Mahari watafikia muafaka kuwa Maharibhiyo iwe pesa kiasi Fulani au mifugo au vyote au na baadhi ya bidhaa kama nguo etc. Baada ya hapo wajumbe wa upande wako watawataarifu wale wa upande wa mke mtarajiwa kuwa ngoja wakajipange halafu watawaletea taarifa ni lini watawasilisha Mahari hiyo. Kipindi hicho Cha kujipanga kinaweza chukua hadi miezi 3 na kuendeleza hivyo utakitumia kupata pesa ya kulipa hiyo Mahari. Pia Mahari siyo lazima ilipwe Kwa mara moja bali inaweza kulipwa Kwa awamu. Ahsante
 
Nimekupata mkuu,
Posa tayari ilishaenda mkuu, ilikuwa ni suala la mahari tu na kupatana.
Ntafuata ushauri wa kutoa august
 
Mbona unaogopa wakati hata mahari yenyewe hujafahamu ni bei gani?

Haya mambo ya mahari mara nyingi huwa hailipwi yote, wanaojielewa hufanya hivyo, wale wabishi tunawaacha wadai mpaka wanasahau wenyewe, siku mtoto wao akiwa na mimba tu ndio mwisho wa hizo kelele.

Hapo usiwe na shaka, tafuta kiasi cha kuanzia, hata laki mbili iwepo mfukoni, siku ukienda iwepo, au hata kama haitakuwepo, itafute taratibu, muhimu wakikupa kiasi usisahau kuwauliza namna ya kulipa.

Kama ni mafungu au yote, wakisema yote waambie unaenda kujipanga, ikifika tarehe ya kulipa, toa ile laki mbili ya mwanzo wapelekee waambie yakuanzia.

Hapo wazazi wa mtoto wa kike kama wanajielewa tayari watajua una maanisha kumchukua binti yao, wataiona nia yako, watakuamini, kwasababu wanajua hapa mjini hatushindani kwa pesa, kupata na kukosa yote ni majaliwa tu.

So utaendelea kuwalipa kwa kadri utavyojaliwa, ila hata usipomaliza sio kesi, muhimu tarehe ya ndoa ijulikane ujibebee mtoto mazima, iliyobaki itaenda kumlisha ugali ghetto.
 
Shukran sana mkuu
Kikubwa sitaki wanione Kama msanii aubabaishaji ndo nachofikiria kwa sasa
 

Inawezekana, sema ukweli, ila wakati mwingine komaa hata kama umegonga mtu, hatulegeagi kirahisi hivyo, ukienda kituoni siku 2 utarudi tu mtaani
 
Nimekupata mkuu,
Posa tayari ilishaenda mkuu, ilikuwa ni suala la mahari tu na kupatana.
Ntafuata ushauri wa kutoa august
Wetafuta pesa ya kutumia siku hiyo, then ongea na mkeo mtarajiwa kuhusu changamoto ukilioata. Then nendeni mkapatane mahari bila shaka alafu unawapiga tarehe, na lazima watakubali kwasababu binti atamwambia mamake shida uliopata na mama atamwambia baba, then baba atafanya wepesi
 
Ahsante Sana 🙏🏼 kwa ushauri huu mkuu
 
Shukran sana ndugu yangu ✊🏿
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…