Wadau,ninaomba kuleta mrejesho kidogo juu ya uzi wangu huu,HAKIKA WANAUME TUWENI MAKINI SANA NA BAADHI YA WANAWAKE TULIOWAAMINI.
Baada ya ile circumstance ya kukuta karatasi iliyoandikwa kwa lugha isiyoeleweka,nilijitahidi sana kuvumilia pasipo kumwambia mchumba wangu ambaye mpaka sasa bado hajarudi kutoka safari yake.
Tangu siku ile,kila nikikaa ndani roho inakuwa nzito sana,nashindwa kabisa kutulia,jioni hii baada ya kutoka kazini nikaamua kufumua mikoba yake yote,ikiwemo ya zamaniii,nilichokiona hakika MUNGU aturehemu sisi binadamu,nimekuta viburungutu vya madawa ya kienyeji kama utakavyoviona hapo chini.
Mbaya zaidi ni maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi ndogo,nayo naambatanisha hapa chini,ameandika kwa lugha ya kiswahili,eti "ewe jini makata,nakuagiza kuanzia leo,Rose aondoke Morogoro na asirudi tena,nakuagiza ukamnyonye damu mpaka mauti yatakapomfika"
Huyu Rose ni msichana ambaye nilizaa naye,na kuna wakati aliwahi kuja na nilimueleza wazi kabisa huyu mpnz wangu kuhusu huyo Rose na kilichowahi kutokea huko nyuma!!!
Nimevichoma moto vitu vyote,na leo mpnz wangu huyo ndo anarudi kutoka safari yake.
Vitu vyote nimevichoma moto,baada ya kushindwa kuvumilia kubaki navyo,sasa ni wazi kwamba ninaishi na mtu hatari sana,picha ni kama zifuatavyo
View attachment 536129View attachment 536130View attachment 536131View attachment 536132View attachment 536133View attachment 536134View attachment 536135View attachment 536136