Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Wana jukwaa naomba nisipoteze muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Nimepitia misuko suko mingi sana katika mahusiano,ilifika mahali nikaomba wadau mnishauri kwa baadhi ya mambo yaliyonikumba,nawashukuru wengi mlinishauri na maisha yakaendelea.

Nilipata binti,mpole na mtaratibu sana,nimekuwa naye katika vipindi vigumu na hakuwahi kuonyesha hali yoyote yenye mashaka.

Nimeshitushwa sana leo baada ya kuona vitu vya ajabu kwenye mkoba wake,(ambao sikuwahi kuuona tangu nimefahamiana naye,).

Naviweka hapa,wataalamu wa lugha ya kiarabu naomba mnisaidie kutafsiri maana ya maneno haya,nimekuta karatasi ikiwa na picha yangu,imeandikwa kwa maandishi mekundu kwa lugha ya kiarabu,halafu imefungwa na karatasi nyeusi!!!

View attachment 532069View attachment 532071View attachment 532072
Hapo hakuna herefu ya kiarabu hata moja.kama ni rangi nyekundu kila mtu anayo maana tuna damu na kama ni uzi kila mtu anavaa nguo zilizo shonwa na kama n karatasi kila mtu kasoma shule kwa kutumia makaratasi.endelea kupiga mzigo kama kawa kama dawa tena mpakie na congo dust.kama huna nambie mm mina stock ya kutoshaaa.
 
Hiyo kitu nilipigwa miaka nane na limama limoja hivi,nikapoteza network ya maisha,nililipenda balaaa,mshahara wote nampelekea yeye,ilibidi mama yangu aingilie kati nae akaenda kwa sangoma ili nimchukie huyo mpenzi jimama,yan hiyo karatasi inalowekwa kwenye kikombe chenye maji then ananuia maneno jinsi anavyotaka iwe,then hayo maandishi yanayeyuka ,maji yanakuwa mekundu ,halafu hayo maji yanawekwa kwenye mboga,yaan hapo baba angu ukila lazima uisome namba,utafanya kila atalolitaka,mimi sitasahau yaliyonikuta.
Naomba uzoefu wako bhana,maana mimi nimekasirika kweli kweli,nasema akija,namwelezea maamuzi yangu basi,lakini kuna wakati napofikiria maisha pasipo yeye roho inaumaaa,lakini lazima nimuache!!!
 
Hiyo kitu mbaya mkuu,ukimwacha haitapita siku mbili utamtafuta wewe mwenyewe tena kwa tochi[emoji23] [emoji23] [emoji23] ,ukionà unashindwa kumwacha huna budi nawe wende kusafishwa mkuu, kwa mganga,kuna namna watakusaidia.
 
Ni imani yake tu, hapo atakuwa aliambiwa na "mtaalam/ fundi" aka mganga au "shehe" kuwa hiyo karatasi aiweke kwenye chupa ya maji na maji yabadilike rangi kisha ayanywe maji hayo kwa kiasi kadhaa pia ajipake hayo maji kama mafuta kwa siku kadhaa, yawezekana pia amenyunyuzia ktk msosi au maji ya kunywa ili na wewe elements zikuingie! Lengo lake sijajua la kwenda kwa mtaalam ila posibly mapenzi au mali yako au kukulainisha! Maana ya maneno sijui ila sidhani kama yana impact, yaweZekana ni maneno ya kawaida tu ila kwa imani yake akiona hivyo basi anamkubali fundi au yawezekana ni herufi tu zisizo na maana au yawezekana ikawa ni mochoro tu inayoonekana kama ni lugha ya kiarabu, wataalam huwa wanacheza na akili za mteja tu ili kumpiga pesa kisawa sawa! Hapo ameshatoa sana pesa ya huduma na ya vifaa!
Ila mwisho wa siku hivi vitu havina impact kama hauna imani navyo, lakini demu hafai maana ana imani mbaya na akipata fursa ya kukudhuru sababu ya imani yake anaweza kukudhuru, anza achana nae mdogo mdogo!!
 
Upuuzi mtupu..!! Huna hata sababu ya kumuacha we akija mwambie tu ukweli umegundua ujinga wake. Muulize kwa upendo akueleze alienda kwa mganga kwa ajili ya nn!!? Unaweza kumtisha kuwa umefuatilia so asikufiche chochote. Akikueleza ukweli,anza kumueleza ukweli kuhusu upuuzi wa mambo yanayoitwa ushirikina! Km ataendelea tatizo ni moja tu,mganga atakuja kumpa sumu ya kukuua ww au yeye mwenyewe!!
 
Sasa si umuulize yeye na kwann amefanya hivyo????HUYO NI MPENZI WAKO UMEKUTA PICHA YAKO NA HAYO MAANDISHI YA KIARABU SASA UNAKUJA KUTUULIZA SISI.?Una umri gani??
 
Soma kwa makini,halafu uje tena,then wewe nadhani haujui maana ya uwepo wa jamii forum,bora ukae kimya tu!
 
Ni imani yake tu, hapo atakuwa aliambiwa na "mtaalam/ fundi" aka mganga au "shehe" kuwa hiyo karatasi aiweke kwenye chupa ya maji na maji yabadilike rangi kisha ayanywe maji hayo kwa kiasi kadhaa pia ajipake hayo maji kama mafuta kwa siku kadhaa, yawezekana pia amenyunyuzia ktk msosi au maji ya kunywa ili na wewe elements zikuingie! Lengo lake sijajua la kwenda kwa mtaalam ila posibly mapenzi au mali yako au kukulainisha! Maana ya maneno sijui ila sidhani kama yana impact, yaweZekana ni maneno ya kawaida tu ila kwa imani yake akiona hivyo basi anamkubali fundi au yawezekana ni herufi tu zisizo na maana au yawezekana ikawa ni mochoro tu inayoonekana kama ni lugha ya kiarabu, wataalam huwa wanacheza na akili za mteja tu ili kumpiga pesa kisawa sawa! Hapo ameshatoa sana pesa ya huduma na ya vifaa!
Ila mwisho wa siku hivi vitu havina impact kama hauna imani navyo, lakini demu hafai maana ana imani mbaya na akipata fursa ya kukudhuru sababu ya imani yake anaweza kukudhuru, anza achana nae mdogo mdogo!!

Mkuu umenena vema, waganga au washirikina ni wajanja sana wa kucheza na saikolojia ya mteja/anaehitaji huduma zao. Kwa kifupi hayo maneno sio kiarabu wala lugha yoyote, yanafanana na herufi za lugha ya kiarabu lakini si sawa kabisa na zinavyoandikwa wala kusomeka, yaani alichokieleza Barafuwamoyo ndicho kilichoendelea, huyo mwanamke kwa imani yake potofu na kutokujua kwake kafungiwa hilo karatazi lililochorwa chorwa kapewa akidhani hayo maadishi yana maana yoyote.

Kwako muhusika, hicho kilichoandikwa hakina maana yoyote katika lugha yoyote ile uijuayo au ambayo unahisi inafanana na hayo. Hivyo basi wewe ondoa hofu na kaa na huyo mwenzio, mueleze ukweli kwamba kapoteza muda wake wa bure na pesa zake kidogo alizopeleka huko, ila hicho kitu hakitakudhuru wala hakina madhara ya aina yoyote kwako wala kwake hakina faida yoyote, nyie kama mna malengo yenu ya kuwa pamoja kimaisha mtegemeeni Mungu tu, hayo aliyoyafanya ni kwa sababu ya ufinyu wake wa imani na kuwekeza katika njia zisizokuwa sahihi.

Nawatakia maisha mema ya mahusiano yenu.
 
Nashukuru Mkuu,ni jambo linalotia hasira sana,na kwa kiasi kikubwa linaongeza hofu ya kuishi na mtu wa aina hii,kesho na kesho kutwa nikimuacha si ajabu ukamkuta kwa social networks analalama kuwa wanaume hatufai.

Nimeelewa ushauri wako,lakini ni wazi kuwa sehemu ya ushauri wako naichukua na kuifanyia kazi,lakini ushauri wa kuishi naye nadhani hautakuwa na nafasi tena,maana baada ya tafakuri ya kina,nimeamua KUTOKUISHI NAYE!!
 
Back
Top Bottom