Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Nashukuru Mkuu,ni jambo linalotia hasira sana,na kwa kiasi kikubwa linaongeza hofu ya kuishi na mtu wa aina hii,kesho na kesho kutwa nikimuacha si ajabu ukamkuta kwa social networks analalama kuwa wanaume hatufai.

Nimeelewa ushauri wako,lakini ni wazi kuwa sehemu ya ushauri wako naichukua na kuifanyia kazi,lakini ushauri wa kuishi naye nadhani hautakuwa na nafasi tena,maana baada ya tafakuri ya kina,nimeamua KUTOKUISHI NAYE!!

Kaka ChiefMangu, katika dunia ya sasa sahau kabisa kupata mwanamke au mwenza asiekuwa na mazonge au makandokando, shukuru Mungu huyo umembaini mapema na angalau aliyoyafanya ni kutokana na upeo wake finyu tu wa kiakili na kifikra, yawezekana ni kwa sababu anakupenda sana na ndio imemlazimu ili akutulize akatafute booster, lakini nakuhakikishia; yawezekana huyo akawa ni bora zaidi ya wanawake wengi uliowahi kukutana nao au ambao utakutana nao katika safari yako ya kimaisha ya kimahusiano. Jaribu kuzungumza nae, kuwa muwazi kwake, na kama ana vigezo vinginevyo vyote unavyohitaji kwa mwenza usithubutu kumuacha kwa sababu ni mara elfu 50 bora kuishi na shetani umjuae kuliko kumkimbilia malaika usiyemfahamu, kwa hatua uliyofikia ya kumgundua mwenzio kuwa anakwenda kwa waganga ni hatua nzuri sana ya kuelekea kwenye mapenzi ya kweli. Piga moyo konde, hakuna mwanadamu mkamilifu na inawezekana kwa huyo mwenzio baada ya kumuelewesha madhaifu yake akawa angalau 95% "perfect" kuliko kwenda kuanza moja kusoma mahusiano mapya kwa ujiti. Unaweza ukamkimbia huyo ukaangukia kwa mchawi kamili! Huu ni ushauri wangu kama mzoefu wa mahusiano ya jinsi nyenza kwa zaidi ya miaka 20.

Tafakari kwa kina, nakuhakikishia dunia yote hii huyo uliyenaye anaweza kuwa nafuu kuliko wengi unaowaona au utakaojaribu kuwa nao katika mahusiano. Kosa moja halimuachi mke!
 
Hahahaaa!!! duuh hizo ndoa taratibu basi,hapo si ndo atasugua bench zaidi maana mimi na yeye ndo basi tena,inabidi aanze upya!!!
Ehh mmezoea kupotezea mda watoto wa watu, saiv wamewashika pabaya ehhh...
 
Ehh mmezoea kupotezea mda watoto wa watu, saiv wamewashika pabaya ehhh...
Heeh kupotezea muda namna gani,tuna karibia miaka miwili tu,na wala sijaonyesha dalili yoyote ya kumtosa,hapo si ndo ananifukuza kabisa!!
 
La kwanza ni Kumshukuru Mungu kakuonyesha la pili umwambie ukweli kabisa na akwambie lengo lake ni nini na kwanini kafikia kufanya hicho kitu.

la msingi usije kuamini tu na kuingiza hofu na mashaka na wewe kuanza kwenda wa waganga HAPANA mshirikishe kiongozi wako wa kiroho atawapeni msaada na uendelee Kusali kwa Imani yako.

tusiowaogope wasio na uwezo wa kutoa Roho bali tumwogope yule tu mwenye uwezo na kutoa roho
 
Wana jukwaa naomba nisipoteze muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Nimepitia misuko suko mingi sana katika mahusiano,ilifika mahali nikaomba wadau mnishauri kwa baadhi ya mambo yaliyonikumba,nawashukuru wengi mlinishauri na maisha yakaendelea.

Nilipata binti,mpole na mtaratibu sana,nimekuwa naye katika vipindi vigumu na hakuwahi kuonyesha hali yoyote yenye mashaka.

Nimeshitushwa sana leo baada ya kuona vitu vya ajabu kwenye mkoba wake,(ambao sikuwahi kuuona tangu nimefahamiana naye,).

Naviweka hapa,wataalamu wa lugha ya kiarabu naomba mnisaidie kutafsiri maana ya maneno haya,nimekuta karatasi ikiwa na picha yangu,imeandikwa kwa maandishi mekundu kwa lugha ya kiarabu,halafu imefungwa na karatasi nyeusi!!!

View attachment 532069View attachment 532071View attachment 532072
Hakuna kitu hapo ni tisha toto hiyo. Huyu aliandika ni tapeli tu. Ichome moto. Wajinga ndio waliwao
 
Dini za kigeni zimewaharibu sana binadamu wa leo hasa waafrika,

Huyo dada yupo safi sana rohoni, hajaathiriwa na imani zenu za kizungu na kiarabu.... Yeye anaamini uafrika na imani zake, alichofanya ni sawa na angeenda kanisani akaombewa na mchungaji ili usimuache, sasa yeye katumia imani nyingine, unaitwa utaalamu wa kiafrika...

Huna haja ya kuogopa na kumuacha au kumchukia, kaa nae chini, rudisha moyo wako na akili yako Afrika, simama kama mwanamume wa Afrika, mwambie akufundishe huo utalaamu utawasaidia huko mbeleni kujilinda na kushambulia maadui.
 
Yericko Nyerere,mtazamo na ushauri wako nitavichukua,lakini niwe muwazi tu kwamba,SITAUFANYIA KAZI HATA KIDOGO,na kama huu ndo uafrika wenyewe kama unavyodai,basi ni halali yetu kuendelea kuwa masikini tu.

Yaani badala kufikiria namna gani tukuze technology inayoonekana,tunatafuta kuwafanya binadamu wenzetu kuwa mazezeta kwa mgongo wa mapenzi???
Hahahaaa, hapana tena nasema hapana,na kama ingekuwa na nguvu hiyo uisemayo hata ukoloni usingetia mguu Africa,kwani mababu zetu wangetumia imani hiyo kuwasambaratisha,(kujilinda),zaidi zaidi waliishia kudanganya watu kuwa wana uwezo wa kubadili risasi kuwa maji,ili kuwatia ujasiri wapiganaji,kilichotokea bila shaka unakijua!

Ahsante kwa kuchangia kaka!!!
 
ChiefMamgu, kwani hiyo karatasi ina ushahidi gani kuwa yaliyoandikwa yanakuhusu wewe? Huenda hayakuhusu, mfano labda ni zindiko lake mwenyewe la biashara au kazi zake (ofisini kwake), au dhidi ya mbaya wake/adui yake mahali fulani. Japokua simsapoti katika hili for any reason that she may have. Cha msingi just be courageous to face her and demand her explanations! Kisha ndiposa utaweza ku draw conclusion. Pole mkuu, ndo dunia hii
 
Ahsante sana kwa mchango na ushauri wako,lakini naomba kujibu swali lako kwanza.
"Hiyo karatasi ina ushahidi gani kuwa yaliyoandikwa yananihusu mimi?"

Jibu;Ukisoma maelezo yangu,kuna sehemu nimeandika kuwa,niliikuta hiyo karatasi ikiwa imefungashwa na passport size yangu,ambayo sikutaka kuiweka hapa jukwaani kwa sababu maalum,(in short sikutaka niiweke sura yangu hapa!)

Bila shaka umenielewa Mkuu!!
 
Duh! Hapo nimekusoma mkuu! Nakubali hiyo karatasi Inakuhusu.
 
Wadau,ninaomba kuleta mrejesho kidogo juu ya uzi wangu huu,HAKIKA WANAUME TUWENI MAKINI SANA NA BAADHI YA WANAWAKE TULIOWAAMINI.

Baada ya ile circumstance ya kukuta karatasi iliyoandikwa kwa lugha isiyoeleweka,nilijitahidi sana kuvumilia pasipo kumwambia mchumba wangu ambaye mpaka sasa bado hajarudi kutoka safari yake.

Tangu siku ile,kila nikikaa ndani roho inakuwa nzito sana,nashindwa kabisa kutulia,jioni hii baada ya kutoka kazini nikaamua kufumua mikoba yake yote,ikiwemo ya zamaniii,nilichokiona hakika MUNGU aturehemu sisi binadamu,nimekuta viburungutu vya madawa ya kienyeji kama utakavyoviona hapo chini.

Mbaya zaidi ni maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi ndogo,nayo naambatanisha hapa chini,ameandika kwa lugha ya kiswahili,eti "ewe jini makata,nakuagiza kuanzia leo,Rose aondoke Morogoro na asirudi tena,nakuagiza ukamnyonye damu mpaka mauti yatakapomfika"

Huyu Rose ni msichana ambaye nilizaa naye,na kuna wakati aliwahi kuja na nilimueleza wazi kabisa huyu mpnz wangu kuhusu huyo Rose na kilichowahi kutokea huko nyuma!!!

Nimevichoma moto vitu vyote,na leo mpnz wangu huyo ndo anarudi kutoka safari yake.

Vitu vyote nimevichoma moto,baada ya kushindwa kuvumilia kubaki navyo,sasa ni wazi kwamba ninaishi na mtu hatari sana,picha ni kama zifuatavyo
IMG_20170705_170156.jpg
IMG_20170705_170156.jpg
IMG_20170705_170315.jpg
IMG_20170705_171203.jpg
IMG_20170705_172002.jpg
IMG_20170705_172013.jpg
IMG_20170705_172010.jpg
IMG_20170705_171212.jpg
 
Hizo ni baadhi tu ya mafurushi aliyoyaficha kwa ustadi mkubwa,lakini Mungu mkubwa nimeyaona.

Swali ninalojiuliza kwa sasa ni je,NIMWAMBIE AKIFIKA JUU YA HAYA MAMBO YAKE YA GIZA?au NIACHE TU HALAFU NISIKILIZIE ATASEMAJE??

Wana jamii forum wenzangu huu ni mtihani miongoni mwa mitihani migumu sana niliyowahi kuipitia,ningekuwa mnywaji leo ninhekunywa sana!!lakini ndo vile tena,si mnywaji na kichwa kama kina-burst kwa maumivu!!!
 
Tafadhali Mods,naomba mu-update huu Uzi wangu,ili kupata mawazo ya wanajukwaa kwa hili ninalolipitia wakati huu!!
 
Hatari sana mkuu, vipi bado utaendelea kuishi na mtu huyo?
Pole sana.
 
Mkuu ushauri wangu muepuke huyo mtu ni kheri nusu shari kuliko shari kamili, mungu amekuonyesha kuwa huyo si mwema kwako baadae anaweza kukufanyia mambo mabaya zaidi.
 
Back
Top Bottom