Wakuu, niaje?
Mwaka Jana mwezi September, nilikua na road trip ya Dar - Kigoma - Dar, nilidrive na nilikua na vituo kila mkoa/mji njiani. Nikaleta mrejesho hapa:
Mrejesho wa Safari yangu ya Dar Kigoma na kurudi Dar. Nimetumia Mafuta ya Tsh 230,000/= tu!
Wengi wanaulizia maswali mbalimbali na kushare experience mbalimbali, ikawa poa. Ila Kuna Jamaa anaitwa
Kiranga akaongea like ushauri, kwamba ningeigeuza hii kua documentary narecord njiani na kuonesha miji na njia mbalimbali, ingekua poa.
View attachment 3683534
Niliichukulia poa, ila nikasema why not? Ukichukulia napenda sana kudrive na kuvisit new places daily. Ngoja nijaribu, maybe Kuna mtu atavutiwa au anapqta inspiration ya kwenda nilipo pita. Nikaanza.
Sikutaka kuingia gharama, nikastick na iPhone yangu, nikanunua dash mount na kuanza kurecord, for reason of anonymity, nikawa nafanya silent tours, just naweka subtitles siongei.
Kiutani kufika mwezi wa saba mwaka huu, YouTube wakanitumia email kwamba nimekua monetized na naweza kuanza kulipwa. Nikasema No way.
Nikamuambia shemeji/wifi yenu, akanipongeza, kama zawadi akanipa camera (GoPro 12) ili niache kutumia simu wakati wa kurecord.
So nikawa nikisafiri au nikiwa misele mjini naweka GoPro pale kwenye dash nakua narecord silent videos. So Kuna fans/subs wakapenda, wanashauri iki na kile, na Mimi nikawa najaribu ushauri, just ikawa my new hobby.
How much napata, ni kiasi kidogo hadi sasa. Sio cha kulipia kodi Wala nini. Ndio maana nafanya kama hobby, siendi trip yoyote just kurecord, narecord ninavyoenda sehemu so nisiingie unnecessary gharama. Mfano tokea niwe monetized hiki ndio nimepata:
View attachment 3683540
Ukiwa more serious na ukachagua interesting niche, unaweza pata zaidi. Niche yangu Haina wadau wengi, ila ukiwa na niche za burudani, za umbea unatoboa mapema.
Kua monetized, YouTube wanataka uwe na angalau na Subscribers 1,000 na Watch hours 4,000 au kama Shorts views Mil 10. Mi nilifikisha subs 1,000 kama zali.
View attachment 3683547
Kuna video moja unaweza kukuingizia ata $5 kwa views 1.5k wakati nyingine same views ata isivuke $1 kwahiyo ni hit and miss. Factors kama RPM, niche, urefu wa video, short au long form zina matter.
Shorts ni takataka, zinakupa subs, ila hazikupi pesa. Mfano short Ina views 30k ila ata $1 haifiki, ila inalipa subs karibia 40.
View attachment 3683548View attachment 3683549
Kwahiyo kama hauna mishe na hauna aibu, simu Yako, mic na akili unaweza pata pesa ya mlo.
Pamoja.