Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000


Kwa mtu makini anayejua kucheza na pesa kwenye ujenzi kama nyumba ya ukubwa huo imeshakula 50millions na hujafikia hata kupiga plaster basi amini usiamini fundi wako au unayemwamini kukusimamia ujenzi atahamia kwenye nyumba yake akuache ukiwa bado kwenye nyumba ya kupanga.

Materials unaagiza kwa container kutoka ulaya au?sipo hapa kubishana nimekupa tahadhari tu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Ni shida, na hapo umebananabanana na mafundi wa mitaani, umezunguka maduka kupata material za bei nafuu hadi karikaoo umeenda, ingejengwa na injinia hadi sasa ingekuwa inasoma milioni 100.
Hii nyumba unasimamia mwenyewe maana kuna mtu kwa hela hiyo kuna mtu namfahamu alijenga vyumba vinne chumba kimoja master, sebule mbili ambapo moja ipo chini na nyumba ni underground
 
Melo kawafungulia dunia,kuweni mnachotaka!!

Ukishindwa kuwa Don hata Jf then you'll never be!

Humu watu kazi kujifaragua tu,kosa uombe picha utajibiwa "oooh na-maintain anonymity choroko,kunde,maharage".

Weka hata floor plan basi ndo kimoja mtu ana-log off.

BTW:Ukiona mbongo hakukatishi tamaa jua you're aiming too low.

Komaa Mzee
 
..........Mkuu umemaanisha au?hata hivyo sikubishii inawezekana ulipo wewe gharama zikawa kubwa zaidi but kwa ujenzi wa nyumba standard Dar gharama zipo juu kiasi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk

Uki-weigh out inabidi gharama za mikoani ziwe sawa na za Dar.. Huwa sijui kwanini raia wa Dar wanasema bei ya kujenga kwao ni gharama kulinganisha na mikoani.

Dar: Gharama za mafundi ni kubwa. Bei ya kununua eneo/kiwanja ni kubwa. Bei ya mbao ni kubwa. Mawe na mchanga vinapatikana mbali and hence bei ni kubwa

Mikoani: Cements ni bei (Mwanza-18,000 to 19,000/bag), Mabati ni bei, Chokaa Plus white cement ni bei, gypsum board ni bei, Rangi ni bei na vinginevyo vinavyosafirishwa from Dar.
 
Ndugu usitishwe na maneno kama Haya. Hatua uliyopiga ni kubwa. Angalia huyu ndugu milion 50 na bado ajamaliza finishing vyumba vitatu? Kupau 15 unapau nini? Ndio fundi wako anakupiga namna hii?? Kama kweli unajenga na sio porojo na umetumia kiasi hicho basi huyo fundi wako kamtimue haraka.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] choroko kunde maharage
Hum ndani buana [emoji114][emoji114]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshawahi kujenga mkuu? Unajua chumba kimoja matofali mangapi yanaingia mkuu? Chumba cha ft 12 x 10?
 
Mleta uzi kazana, hapo ulipofika sio pabaya.
 
Drill ni mashine ya kupekechea ukuta au chuma....unamaanisha grill?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naongelea nyumba siyo kibanda kama mleta mada anavyodai, kwa rate za mainjinia hii nyumba hujengi chini ya 100m. Unaongelea milioni 50, hauko serious..
 
Hapo nahisi hakuna plaster. Hakuna ceiling board ya aina yoyote. Mbao ni zile rejected.
Imejengwa kama za Wapemba was jenga uza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…