Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Gharama ujenzi mikoani ni nafuu kuliko Dar, viwanja na mafundi ni bei ya chini sana,material bei zake tofauti yake na DSM ni kidogo sana kwa sababu ya ushindani wa kibiashara.
Kwani cement Dar sh ngapi? Huku Mwanza ni 19-19500
 
Wee jamaa bhana, unaongelea milioni 50. kwa rate za mainjinia wengine hiyo nyumba wanakamilisha kwa milioni 200.
 
Mbona tayar ushakuwa! Sema amen kwanza!
Halaf k hebu Fanya kutupia bas digits zako kwa waziri mkuu,nilizipoteza et[emoji849]

Hahaaha eti tayari..nacheka kifwala!.changa🔥 ni nyingi sana aisee unaenda mbele hatua kumi unaridi 3😑.muombe@Bushmamy namba zangu😅😅!
 
Watu wengi wanawadanganya watu kuwa finishing gharama....

Chumba cha kawaida cha sqm 10.8 kinachukua vigae vya 1.8sqm box 6 (60*60)
Ambapo ukichukua vya gharama tuseme 40000 kwa box ni 240000
Ufundi ni 50000
Cement na powder ya vigae hautazidi 50000

Jumla 340000

Gypsum chumba cha kawaida huchukua hicho hicho kitachukua 5 gharama zake ni chini ya 100000 pamoja na ufundi

Chumba 1 finishing haiwezi zidi 2 mil hapo ushapiga na rangi na mlango na upvc au aluminium tena hii ni gharama kwa vifaa grade 1

Vyumba 3 inaangukia kwenye 6mil na kubakia
Ukienda sebre dining na jiko haiwezi zidi 6 mil

Hivyo finishing kwa jumla yake inaweza isizidi 12 mil na hapo ushafanya wiring

Tatizo kubwa twaachia mafundi hatuendi kupima wala kununua bidhaa husika

Fundi wa geti anapiga mahesabu ya juu anakwambia kitasa 70000 anaenda weka cha 22000
Square pipe anakuambia ameweka ya 25000 kumbe dukani ni 17000
Bati anakwambia 65000 kumbe kapata kwa 40000


Umeme nao anakulia hela kwa kuambia kanunua mcb za 12000 kumbe kanunua za 5000
Wire anakwambia kanunua 2.5 kwa 1.5 kumbe kanunua 2.5 pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au labda jamaa Iyo nyumba anapaua kwa ZEGE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetubania picha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
acheni kupotosha na kukatisha watu tamaa! .
 
bora umewachana wapuuz kweli!
 
Mkuu naongelea nyumba siyo kibanda kama mleta mada anavyodai, kwa rate za mainjinia hii nyumba hujengi chini ya 100m. Unaongelea milioni 50, hauko serious..

Mtu ambae hajawahi kufanya ujenzi wa nyumba kubwa ukimwambia hivi atakuelewa,hakuna namna nyumba yenye master bedroom,vyumba viwili vya kulala jiko na store ikatumia 50 mill huku hujapiga hata plaster,pale juu ulisema paa tu limekula 15mill.....

Well,kwa hiyo wewe boma tu umejenga kwa 35millions?nyumba gani ya hivyo brother!ndo maana pale juu nikakwambia kupitia wewe yupo mtu anajiandaa kuhamia kwake huku ukijisifu kujenga boma lenye paa tu kwa hela ambayo wenzako kwa hela hiyo hiyo wanajenga 75% ya ujenzi wa nyumba kubwa na yenye viwango vyote.

Kingine mtu anaposema ana kibanda hamaanishi kama cha kuku,ni aina tu wabongo tumezoea kuwakilisha tunapozungumzia nyumba zetu ili kuondoa kuonekana tunaringa.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Sir_Mimi,
Tusibishane sana mkuu, wengine wanatumia material reject, low quality au zilizoibwa mahali. kuna jamaa aliwahi kusema hatumii pesa nyingi kwa mafundi, anavizia wakiwa wamepigika hasa anawaita wanapiga msosi ambao wataufanyia kazi. Kwa upande wako inawezekana kabisa upo sahihi..
 
Hawa vijana wa Daslama ni wapuuzi sana yani wakishakua na uwezo wa kupanga kachumba kamoja Sinza tv flat screen,kasofa,kafliji na kitanda cha 6x6 basi wanamuona kila mtu ni fala.
 

Kwa uzoefu wangu wa ujenzi huwa sibishi mtu akiweka bei yake.. Nitakachomuomba ni atuambie ametumia material ipi. Inawezekana ameamua kutumia vigae. Inawezekana ameenda kununua tofali za SUMA JKT ambazo inaaminika ni imara sana na amesafirisha umbali mrefu, inawezekana uwanja wake haupo square, inawezekana dizain ya grills zake ni unique (zimemuingizia cost) etc..

Naamini factors za bei ni nyingi sana ukiachia kigezo cha Kupigwa na Fundi.

Kuna wakati unaisimamia site yako, kuna cost unakutana nazo hadi unasema "Hapa nisingekuwepo ningeamini fundi ananipiga"

Nukta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…