Watu wengi wanawadanganya watu kuwa finishing gharama....
Chumba cha kawaida cha sqm 10.8 kinachukua vigae vya 1.8sqm box 6 (60*60)
Ambapo ukichukua vya gharama tuseme 40000 kwa box ni 240000
Ufundi ni 50000
Cement na powder ya vigae hautazidi 50000
Jumla 340000
Gypsum chumba cha kawaida huchukua hicho hicho kitachukua 5 gharama zake ni chini ya 100000 pamoja na ufundi
Chumba 1 finishing haiwezi zidi 2 mil hapo ushapiga na rangi na mlango na upvc au aluminium tena hii ni gharama kwa vifaa grade 1
Vyumba 3 inaangukia kwenye 6mil na kubakia
Ukienda sebre dining na jiko haiwezi zidi 6 mil
Hivyo finishing kwa jumla yake inaweza isizidi 12 mil na hapo ushafanya wiring
Tatizo kubwa twaachia mafundi hatuendi kupima wala kununua bidhaa husika
Fundi wa geti anapiga mahesabu ya juu anakwambia kitasa 70000 anaenda weka cha 22000
Square pipe anakuambia ameweka ya 25000 kumbe dukani ni 17000
Bati anakwambia 65000 kumbe kapata kwa 40000
Umeme nao anakulia hela kwa kuambia kanunua mcb za 12000 kumbe kanunua za 5000
Wire anakwambia kanunua 2.5 kwa 1.5 kumbe kanunua 2.5 pekee
Sent using
Jamii Forums mobile app