Ndo unajiuliza humu watu wanajenga nyumba au vitu vinavyofanana na nyumba,mtu anashangaa nyumba ya vyumba 3 kutumia milioni 50 na bado haijakamilika! hizo rate mbona ni za chini sana na hapo umehenya na hawa mafundi wa kitaa. Hapo umezunguka maduka kupata penye unafuu wa bei ya material na umesimamia mguu kwa mguu.
Maana nachoshangaa maana bati za migongo mipana or maxcover lazima huezekaji huende kwny 15m ,na hukigusa versatile,romanitile lazima ufike 30m hapo kuezeka tu maana haina hiyo ya huezekaji inahitaji mbao nyingi labda tuwaulize
Mkuu usibishane naye huyu huwezi jua anajenga nyumba ya kiwango gani?but kwa uzoefu nyumba hizi hizi za vyumba vitatu kimoja master unaweza ukaijenga hata 300m inategemea ramani yako ya nyumba na aina ya mafundi unatumia,but mm nimejenga nyumba ya hivyo kwa zaidi ya 200m
Kwa vyovyote hizi reply zinahusu post zangu nilizo-post kwenye huu uzi,hata utumie material gani kutoka Tanzania hakuna nyumba ya chini ya room tatu even nne inajengwa boma tu bila kuezekwa kwa million 35 msiwatishe watu na kuwakatisha tamaa kwa vitu vyenu vya kubuni.
Hapo chini nitaonekana kama natafuta kick but siyo lengo langu nataka mkuu
Nyumisi utuwekee hilo paa lililo-cost ml15 kwenye nyumba ya rooms zisizozidi tano,hapa nimeambatanisha picha bati ni ALAF order kiwandani moja nilinunua Tsh28,580 zimeingia bati 120,kuna kofia hesabu za mbao nk haijafika mill12 fundi 1.3mill nyumba ina master bedroom,vyumba viwili vya kulala,choo&bafu public,store,jiko dinning na sitting room kubwa inaenea set mbili za sofa na baraza mbili ya mbele kubwa na nyuma ya wastani,msingi wa hii nyumba chini ya ndugu yangu engineer ulikata mil8 na cent kadhaa.
Nimejengea tofali Nch 6,imekula tofali 4,170 cement sikuinyima nondo sikuinyima na kwa sababu pana kama kilima ina nguzo tano permanently za zege zilizosimama kutoka kwenye kiuno mpaka kwenye lintel zizolinigharimu cement ya kutosha sasa nimeshaipiga plaster iliyopimwa kwa TIMANZI cement tu nje na ndani mifuko 73,frame za milango nimeweka mbao Mninga nyumba nzima milango ipo saba frame moja 190K tayari nimeshafunga milango mitatu mkubwa umeni-cost 475K midogo @270K,nimepiga brandering na rough floor kwa ajili ya kupokea tiles napo nimeingiza mchanga na cement za kutosha,grills nimeweka chuma mml6 zipo dirisha 11 vyooni na store 4 ila nimepiga hesabu imegota kwenye Tsh46,475,000/=.
Huu ujenzi nimejenga Dar,naweza kusema nipo zaidi ya %70 nyumba kuimaliza it means kutoka sasa nikiwa na na 20mill nitakuwa naongea mengine halafu nyie mpo hapa mnadanganya jamii mnajenga maboma kwa mil50...siyo vizuri haipendezi kuna watu wanatamani waanze ujenzi ila wakikutana na haya mambo ya kuambiana habari za mamilioni wanaogopa hela wanaenda kuichoma bar au kununua magari wakiamini muda wao wa kuanza ujenzi bado kumbe hata million 10 inafaa kuanza.
Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk