Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Nilisema huyu alojenga kwa 3m huenda ni zile styles za zaman...korido pemben vyumba! Sipend korido....nikasema kuna desgn nzuri km hyo ya pembe za shiling 5!ndan inakuwa hvyo sio nje!nje inakuwa sq tu
Anhaa kweli itakua nilichanganya na sikuelewa vizuri...hang over hizi zinasumbua...😁😁😁
 
Ni kweli
Ninyi vijana wa mjini kujifanya kujua kwingi ndio maana kila siku mnamaliza mtaa kwenye nyumba za kupanga,miezi sita tabata,inayofuata sinza,kimara hamjengi.
Wakati mwingine mkija mikoani mnaona aibu kwakuwakuta vijana wa umri chini yenu wapo kwenye nyumba zao na maisha yanasonga.
Hii ni kwasababu ya kujifanya wajuaji wakati kiuhalisia haimna isue kazi kuzurula na vibegi mjini hamna dira yoyote.
Ujenzi kama utausimamia mwenyewe na ukajua namna sahihi yakukwepa gharama utatumia pesa yakawaida.
Sio mbaya ninyi endeleeni kugombania na kujisifia kupanga nyumba za wenzenu zenye tiles nzuri,aluminium,uzio na ma geti mpaka mstuke mvi kichwani.
Kutojenga ni udunya, vijana wengi wanapora simu na kujifanya wanapenda kwenda kuishia moi kwa kuzunguka na bodaboda mjini.

Wengi wanadanganyana sana, na woga, unajichumbia dar es, wkt fursa kibao mikoani, nenda mbeya, fursa kibao, nenda mtwara, dar yenyewe ingia kariakoo chukua mzigo nenda chanika unauza. Wengi wanashoboka na videmu na kupigia ukimwi viuno. Nineeleezea hapa kajihela nilikokaweka kakafika 13M roughly 1M ikikuwa na nauli nk.

Nje ya mji kiwanja sh M2 kama inazidi ni 2.5 unakuta kijana apora wake na kula mali za watu,mwishowe anang'oka na laana, baadae asijue mchawi ni yeye mwenyewe
 
Ni kweli

Kutojenga ni udunya, vijana wengi wanapora simu na kujifanya wanapenda kwenda kuishia moi kwa kuzunguka na bodaboda mjini.

Wengi wanadanganyana sana, na woga, unajichumbia dar es, wkt fursa kibao mikoani, nenda mbeya, fursa kibao, nenda mtwara, dar yenyewe ingia kariakoo chukua mzigo nenda chanika unauza. Wengi wanashoboka na videmu na kupigia ukimwi viuno. Nineeleezea hapa kajihela nilikokaweka kakafika 13M roughly 1M ikikuwa na nauli nk.

Nje ya mji kiwanja sh M2 kama inazidi ni 2.5 unakuta kijana apora wake na kula mali za watu,mwishowe anang'oka na laana, baadae asijue mchawi ni yeye mwenyewe


Hahhaa mbona vichambo jamani!tutanuna ujue!
 
Hahhaa mbona vichambo jamani!tutanuna ujue!
Haya mambo bila kula kichambo hujengi, na utawatesa watoto wako kwenyr Nyumba za watu. Ukikutana na mwenye nyumba mnoko huyo ndio poa, maana utajenga tu. Ukikutana na mwenye huruma,ujue imekula kwako.
 
Ndo unajiuliza humu watu wanajenga nyumba au vitu vinavyofanana na nyumba,mtu anashangaa nyumba ya vyumba 3 kutumia milioni 50 na bado haijakamilika! hizo rate mbona ni za chini sana na hapo umehenya na hawa mafundi wa kitaa. Hapo umezunguka maduka kupata penye unafuu wa bei ya material na umesimamia mguu kwa mguu.
Maana nachoshangaa maana bati za migongo mipana or maxcover lazima huezekaji huende kwny 15m ,na hukigusa versatile,romanitile lazima ufike 30m hapo kuezeka tu maana haina hiyo ya huezekaji inahitaji mbao nyingi labda tuwaulize
Mkuu usibishane naye huyu huwezi jua anajenga nyumba ya kiwango gani?but kwa uzoefu nyumba hizi hizi za vyumba vitatu kimoja master unaweza ukaijenga hata 300m inategemea ramani yako ya nyumba na aina ya mafundi unatumia,but mm nimejenga nyumba ya hivyo kwa zaidi ya 200m
Kwa vyovyote hizi reply zinahusu post zangu nilizo-post kwenye huu uzi,hata utumie material gani kutoka Tanzania hakuna nyumba ya chini ya room tatu even nne inajengwa boma tu bila kuezekwa kwa million 35 msiwatishe watu na kuwakatisha tamaa kwa vitu vyenu vya kubuni.

Hapo chini nitaonekana kama natafuta kick but siyo lengo langu nataka mkuu Nyumisi utuwekee hilo paa lililo-cost ml15 kwenye nyumba ya rooms zisizozidi tano,hapa nimeambatanisha picha bati ni ALAF order kiwandani moja nilinunua Tsh28,580 zimeingia bati 120,kuna kofia hesabu za mbao nk haijafika mill12 fundi 1.3mill nyumba ina master bedroom,vyumba viwili vya kulala,choo&bafu public,store,jiko dinning na sitting room kubwa inaenea set mbili za sofa na baraza mbili ya mbele kubwa na nyuma ya wastani,msingi wa hii nyumba chini ya ndugu yangu engineer ulikata mil8 na cent kadhaa.

Nimejengea tofali Nch 6,imekula tofali 4,170 cement sikuinyima nondo sikuinyima na kwa sababu pana kama kilima ina nguzo tano permanently za zege zilizosimama kutoka kwenye kiuno mpaka kwenye lintel zizolinigharimu cement ya kutosha sasa nimeshaipiga plaster iliyopimwa kwa TIMANZI cement tu nje na ndani mifuko 73,frame za milango nimeweka mbao Mninga nyumba nzima milango ipo saba frame moja 190K tayari nimeshafunga milango mitatu mkubwa umeni-cost 475K midogo @270K,nimepiga brandering na rough floor kwa ajili ya kupokea tiles napo nimeingiza mchanga na cement za kutosha,grills nimeweka chuma mml6 zipo dirisha 11 vyooni na store 4 ila nimepiga hesabu imegota kwenye Tsh46,475,000/=.

Huu ujenzi nimejenga Dar,naweza kusema nipo zaidi ya %70 nyumba kuimaliza it means kutoka sasa nikiwa na na 20mill nitakuwa naongea mengine halafu nyie mpo hapa mnadanganya jamii mnajenga maboma kwa mil50...siyo vizuri haipendezi kuna watu wanatamani waanze ujenzi ila wakikutana na haya mambo ya kuambiana habari za mamilioni wanaogopa hela wanaenda kuichoma bar au kununua magari wakiamini muda wao wa kuanza ujenzi bado kumbe hata million 10 inafaa kuanza.
IMG_20191228_210008.jpg
IMG_20191228_205833.jpg
IMG_20191228_205235.jpg
IMG_20191228_205000.jpg


Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Nyumisi fanya kama nilivyofanya hapo juu post #149 watu wapate idea wanaoamini kuna kujenga boma kwa mil50 nao waone hilo paa linalo-cost mil15 linavyofanana,wabongo sometimes tunapenda sana kukatishana tamaa kitu ambacho ni kibaya sana hasa kwa sisi vijana tunaohangaika kuinuka.

Tuepuke hilo siyo jambo zuri hata kama tunaandikia sifa tukumbuke madhara yake kwa wanaosoma maandiko yetu ila siyo kwa sababu tunapata likes basi tujiandikie tu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Wote mnaotaka kujenga,msisikilize watu wa dar kama uko mkoani,nimejenga nyumba kama yako na hatua hiyo hiyo kwa mil 15. Na nimetumia bati ya Alaf PC 115 @ 28000, tofali za kuchoma zile ndogo 36000, @ 50 Mchanga huku fuso moja ya cubic m 4 ni 60000, mawe ni 70000 mbao created 2*4 futi 12 ni 4500,nilitumia mbao za milion 1.2 na zilibaki mbao 30,fundi kujenga kuanzia msingi hadi juu million 2,fundi kupaua laki 8,cement mfuko 15000,nondo 19000,kokoto huku ni 150000, Manunuzi nilifanya mwenyewe na nimekomaa site mwenyewe kipindi hiki cha likizo, shimo la choo nilijenga kabla ili nipate udongo wa kujengea na wa kujaza kwenye msingi,

Usifananishe bei za za dar na mikoani,
Mfano mafundi wa kupaua dar huwezi pata kwa laki 8,

Fanya research zako mwenyewe kulingana na eneo ulipo uanze ujenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom