Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

Mwenye nyumba akiweka mnyambulisho na mlinganyo wa gharama jinsi alivyo jenga hiyo nyumba kwa kiwango cha fedha alicho sema na mimi najenga yangu kesho asubuhi na mapema.

Mohamedi Mtoi you are not serious bro. nakushauri anza ujenzi bila kusubiri mchanganuo wa huyo jamaa. kwa kijijini inawezekana lakini kuanzia manisapaa hiyo kitu hakuna labda kwa kuwachukua mafundi toka vijijini.
 
Hongera sana mkuu...ma baazazi wengi humu mjini hawana hata kakibanda aisee...hiyo nyumba ukiifanyia makeke ni ya ukweli balaa...........
 
Mkuu hongera, ingawa nahisi mafundi au vifaa wamekuibia kidogo.

Mimi nyumba yangu hii hapa chini nimeijenga kwa gharama ya Tsh. 600,000 (laki sita). Nimeshahamia kwangu na kuondokana na adha za wenye nyumba na pembeni nina kibustani changu cha mboga mboga maisha yanaendelea.

Nyumba hii nimejenga Bunju kwenye kiwanja nilichopewa na serikali baada ya kuhamishwa kwa nguvu Jangwani wakati wa mafuriko ya December mwaka juzi.
ImageUploadedByJamiiForums1358837045.114359.jpg
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.
Naona dstv hapo juu, wewe ndo kati ya wale walimuelewa JK kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana..!
 
Heri yako wewe kuliko hawa watu hapa chini:
... Katika mkutano huo Dk. Slaa alitoa kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2005, iliyoandaliwa na mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa, inayoonyesha kuwa halmashauri ya wilaya hiyo, ilitumia sh milioni 700 kujenga matundu manne ya choo katika shule za msingi nne.
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.

Hongera. lakini mkubwa nisamehe, mimi siamini kwa hela hiyo. In a nut shell, tupe mchanganuo. Tutajifunza toka kwako!
 
Yes nakubaliana na wewe,maana bati zenyewe naona umechukua pale veterinary-tazara,hali kadhalika madirisha na mirango,pia tofadhi ni za tope,alafu inaonyesha ni rufiji sio Dar.
By the way hongera.
kaka Rufiji huwezi kujenga nyumba kama hii kwa bei hii hata kidogo..kule Nyaminywili au Mwasemi mpaka Mibuyu Saba..huwezi kabisaaa..take my words
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.

Namsubiri Natalia (Muke ya Muzungu aka republican) atoe comments kwanza then nitarudi...!!
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.
Hii nyumba most likely ina ukubwa wa square metre zisizopungua 50. Kwa shilingi 4.5m maana yake ni kwamba gharama za ujenzi ni shilingi 90,000 kwa kila square metre. Hii ngumu sana kuiamini labda kama walivyosema wengine hapo juu, kazi nyingi zinazohusiana na ujenzi huu utakuwa ulizifanya mwenyewe na vifaa vingi ulivyotumia katika kujenga ulikuwa unavipata "bure" au ulivilipia kwa namna nyingine ('barter trade' basis).
 
Tofauti ni kubwa sana kati ya kwako na ya kwake. Mimi naona jamaa katoa changamoto pamoja na yule wa Bunju ingawa 600,000/= sijui. Natafuta ramani kama nyumba ya kwako nielekeze kwa mchoraji

Mkuu embu nipe info za hiyo yako urefu kwa upana I mean square meter ngapi
 
Tofauti ni kubwa sana kati ya kwako na ya kwake. Mimi naona jamaa katoa changamoto pamoja na yule wa Bunju ingawa 600,000/= sijui. Natafuta ramani kama nyumba ya kwako nielekeze kwa mchoraji

uko wapi mkuu?
 
Mkuu embu nipe info za hiyo yako urefu kwa upana I mean square meter ngapi

Sijaelewa ila kama unataka ninayofikiria kuanzisha mchakato wa kujenga ni kama 192 m^2
Kwa Mdau mwingine Mimi nipo Dar lakini project itakuwa kanda ya ziwa
 
Mkuu hongera, ingawa nahisi mafundi au vifaa wamekuibia kidogo.

Mimi nyumba yangu hii hapa chini nimeijenga kwa gharama ya Tsh. 600,000 (laki sita). Nimeshahamia kwangu na kuondokana na adha za wenye nyumba na pembeni nina kibustani changu cha mboga mboga maisha yanaendelea.

Nyumba hii nimejenga Bunju kwenye kiwanja nilichopewa na serikali baada ya kuhamishwa kwa nguvu Jangwani wakati wa mafuriko ya December mwaka juzi.
View attachment 80410

nyumba yako mwenyewe lakini unashindwa kuisogelea na kupiga picha kwa ukaribu, badala yake unapiga picha ukiwa kwenye gari mita kama 50 toka nyumba ilipo? waliosoma photograph watagundua kitu cha tofauti
 
wapi huko mkuu?
Maana morogoro wanachoma sana tofari na bei ya jumla ni kuanzia 120-180.
Huko kwenye tsh50 sijui ni wapi!
mkuu tatizo kunawatu wajinga na hawatakikujua ujinga wao, hata mbeya tofari za kuchoma ni tsh 150 - 250
 
Kwa uzoefu wangu wa ufundi hiyo sio kweli. Gharama tu za msingi yani Mawe, Mchanga, Saruji, Kokoto, wachimba msingi na fundi ni zaidi ya 1.8m. Kuseti msingi ni 5laki kwa bei ya kirafiki, one meta deep and one meta long with 45cm to excavate ni 2000. Sasa urefu wa msingi wote na vyumba kuchimba tu inafika laki4 hiyo ni pamoja na clearance of the site. Kama amejena wakati wa mkoloni Mwl Nyerere sawa tena 80's.
 
Back
Top Bottom