Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.

Remember a story of the three little pigs.

When a big bad wolf comes and asks you to let him in, you will boast 'not by my hair of my chin chin chinny' . Bad luck when the wolf huffs and puffs your house will be blown in.

Cheap can be expensive.
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.


aah kumbe wewe ndo Mwala J, halafu mwana JF mwenzangu!!!. Leo nikija kuangalia mpira jioni lazima unipe punguzo la angalau Tshs 200/= sitoi 500/=. Hata hivyo hongera, Hawa matomaso waache tu waendelee na ubishi wao. Wewe endelea kutoza tozo la DSTV umalizie nyumba (wengine wanaita banda) yako. Kila la kheri
 
Yawezekana amejenga huko SANGAMWALUGESHA!!!!

Kokote mkuu atusaidie mchanganuo ili watu tuingie kwenye mchakato. Maana hiyo hela naona hata mbao za kenchi tuu haitoshi. Ndio maana nikasema labda foundation, na yenyewe ya kawaida mno. Ukijenga nyumba kama hiyo, hata kodi ikawa 50elf, hela yako yote itakuwa imerudi kabla hata ya kufika miaka, ukizingatia kodi itakuwa ikipanda. Ni sehem nzuri ya kutunzia pesa na unakuwa unakula taratibu.
 
Haya mambo ya kupiga picha vibanda vya watu na kusema umejenga siyo vizuri,kwanza kama ni yako tuambie hilo dish ulilifunga ili iweje kabla ya kuhamia hali kuna hatari ya kuibiwa?
 
tATIZO UMEJENGA WAPI? MIMI KIJIJINI KWETU NAKUJENGEA HIO KWA MIL 1. I MEAN PESA YA MABATI TU BASI
 
hongera kwa kujenga
bila shaka ulisimamia mwenyewe na kazi nyingi ukafanya wewe,
hii inawezekana hasa ukiwa nje ya miji mikubwa.
 
Hii kitu inawezekana sana tu sana sana gharama ni bati za kuezeka tu mchanganuo
Matofali ya kuchoma 3000 unafetua na kuchoma mwenyewe

Mawe unakusanya mwenyewe trekta ni tshs 15000 kwa trela

Cement mifuko 20 unatumia kwenye kona tu sehemu zingine motar ni udongo

Mbao unanunua mti kwa mtu kijijini unapasua mwenyewe tu hakuna tatizo katika hilo

Fundi kijijini ni rahisi kupindukia unaweza mlipa per day 4000
 
Hongera, lakini ungetuwekea mchanganuo wa hiyo pesa mpaka ukafikia hapo ili nasi tujifunze. Mwingine anaweza kujenga kwa chini ya hiyo gharama kwa kutumia vifaa vya ujenzi vya wizi.
 
Hiyo ni bei ya mabati au huenda vifaa vingine ulipewa msaada. Au ulibomoa nyumba nyingine na hizo materials ukatumia tena. Fundi huenda ni wewe mwenyewe
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.
4.5Mill kwa hii nyumba still bado ni NYINGI sana, labda kama bei inajumuisha na kiwanja.
 
Naomba mto hoja na mjenzi wa nyumba hii aweke mchanganuo hapa ili tuweze kumuamini, hata mimi sikubaliani kwama hicho kiwango kingeweza kumjengea nyumba kama hii, anaonekana amepiga lipu, hiyo simemti ya lipu ni shs ngapi? hizo kench ni mbao za sh ngapi? nyumba hii umetumia matofali mangani ya sh ngapi? mimi nina mradi wa interlock sana sana lowest cost ninayoweza tena kwa kujibana sana itakuan 25 - 30m. kwa hili naweza kutoa mchanganuo mkiniuliza, lakini lazima mwenye nyumba awe na kiwanja, hii ni bila hela za kiwanja na bila kuezeka, msingi sichimbi mrefu na huko natumia tofali za kawaida, na interlocking zangu ni nchi 4 ndogo kidog kwa tofali ya kawaida
 
Mwenye nyumba akiweka mnyambulisho na mlinganyo wa gharama jinsi alivyo jenga hiyo nyumba kwa kiwango cha fedha alicho sema na mimi najenga yangu kesho asubuhi na mapema.

Ukiichunguza picha vizuri...unaijiwa na mawazo kuwa hii nyumba imejengwa miaka 10 iliyopita au imetuia 'vifaa vya mtumba'. Mtazamo wangu.
 
Energy aliyotumia mkeo kuchota maji umehesabia? Na mchanga aliokupa jirani uliobaki wakati yeye anajenga?
 
Embu ngoja kwanza

Madirisha yote+milango= 1mil.

Rafu chini+nilu za ukutani+kokoto=1mil

Simenti iliyotumika tufanye mifuko mia=1.6mil.

Mbao za kuezeka+mabati =1mil.

Kumimina kibaraza+nondo za lenta?

Gharama za mafundi?

Kufanya wiyaring'

Plumbering ya maji safi na taka?
Mchanga uliotumika?

Mwala J,mimi nakukatilia kwa asilimia miana ushee kuhusiana na hesabu zako ulizotuwekea hapa.
Mods wafunge uzi tu hakuna cha kujifunza hapa.
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.

Hongera sana!! Acha namie nianze utaratibu ktk kijipori changu Pugu.


Sent via EyePhone
 
hongera kwa kujenga
bila shaka ulisimamia mwenyewe na kazi nyingi ukafanya wewe,
hii inawezekana hasa ukiwa nje ya miji mikubwa.

BOLDBLACK: Nadhani gharama halisi ya nyumba inabidi ihusishe pia gharama hizi. Bila kuziweka unakuwa unadanganya umma vinginevyo aseme "Nimejenga nyumba hii kwa pesa 'taslimu' 4,500,000/= bila kuhusisha gharama za usimamizi na nyingine nilizofanya mimi mwenyewe"
 
Back
Top Bottom