Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

Mbona bati ni kukuu au ulijenga mwaka 47 na ndio nitakubaliana na kiwango ulichosema,choo chenyewe kukijenga si chini milioni 2 sembuse nyumba iliyosimama,au umetumia mazingaombwe kaka
 
Hongera sana kwakuweza pata hiyo nyumba mkuu inshaalah mungu atkuwezesha upigerangi na wasemayo waseme ila unacho mkuu
 
nyumba yako mwenyewe lakini unashindwa kuisogelea na kupiga picha kwa ukaribu, badala yake unapiga picha ukiwa kwenye gari mita kama 50 toka nyumba ilipo? waliosoma photograph watagundua kitu cha tofauti

Mkuu nilivyoona huu uzi jamaa anatamba na nyumba yake waliyompiga Tsh. 4.5 mil, nikaona ngoja na mimi niipige picha nyumba yangu. Na kwa kuwa sina camera, wakati napalilia bustani yangu akapita msamalia mwema na gari yake ikabidi nisimame nimwombe anisaidie kuipiga picha nyumba kisha niirushe hapa kwa great thinkers!

Nisamehe kama hujapata taswira vizuri!
 
Mh!sikubaliani na wewe labda utoe mchanganue na utueleze uliijenga lini?
 
Nashani Mwenye nyumba kuna ratakimu ameiacha. X4,500,000. Hiyo X inaweza kuwa 1 au 2 nikiitazama na nyumba ilivyo.
 
Mbona ni kuu kuu hivyo? Ama ni ya urithi, jamaa kakuuzia kwa 4.5mm then akaenda kunywa chang'aa!!
 
Fafanua,umejenga kwa hichi kiasi na kiasi kingine umesaidiwa au?Sidhani kama ni kweli,labda kama uliwatumikisha watu usiku.
 
Moshi- Kahe, tofali za kuchoma @Tshs 300/= tofali kubwa

Mchanga mjini lori tani 7 Tshs 135,000/=

Cement kg 50 Tshs 15000/=
Labda wewe umejenga Ulanga-Morogoro hongera bana
 
mkuu naona unafanya utani na ujenzi....hiyo nyumba ya 4.5m 'umepanga' tofali ngapi? hizo nguzo pamoja na beams zimekula nondo kiasi gani? bado saruji, labor charge, mchanga, frame za madirisha/milango na karai uliloweka juu!..ww acha kuchezea ujenzi!
 
Kama 4.5m umemaliza nyumba hii ungejenga kwa ngapi ?nisaidie nateseka
 

Attachments

  • dau.jpg
    dau.jpg
    12.1 KB · Views: 188
Mkuu mwala
nimekupenda sehemu moja ambayo umeacha watu wakilipuka na kujaza ma nanii kibao umeweka just a frg
ila ningetamani wa kwanza kuuliza ahizo ni sh ama maana inawezekana mwenzetu umeweka interms of dollers sie tunabwabwaja unatuchora haya nisaidie yangu hapo juu na untajie nitumie kwa doller ama ili ikamilike
 
Mmmh!Hapo hata kama umenunua cement kwa tsh 5000 kwa mfuko kama CDM walivyoahidi kwa kiasi hicho cha fedha utaishia kujenga chumba kimoja tu!!
 
Kwa mjengo wa aina hii inawezekana, ila inatakiwa atufahamishe ameijenga wapi. Nimejaribu kuhesabu bati naona haziwezi zidi 40 na tofali za sementi hazita zidi elfu
 
Hongera sana, najua umejikamua na kujikwamua, kwa hali na uwezo wako ni dhahiri yakupasa ufurahie climax ya hatua hii

Hongera sana tena sana
 
Abdulhalim dharau siyo nzuri,
nyie ndo mnaotamba mjini kumbe wazazi wenu hawana hata pa kujibanza
kwanini usimpe stahili yake aliyejenga jamani.
mie nipo kijijini na wazazi wangu ni matajiri kuliko mimi, hata hivo sioni dharau unayoiongelea ni ipi/
 
Acheni league hebu 2muulize mwaka gani na ni wapi? Hiyo fedha nyingi saana isitoshe kiwanja kilikuwepo tu cha dingi, mbona change inabaki.
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe kila kitu ni maamuzi tu.

Nyumba ya 4.5M!!! Walahi wewe ni miongoni mwa matajiri. asilimia 80% ya waTZ hizo 4.5M ni ndoto ya mchana kuzipata. Nyumba standard za TZ ni za tembe na nyasi kwa walio wengi. Wanapenda sana wawe na nyumba kama hiyo uliyojenga lakini umaskini umetudidimiza. Hata hivyo hongera.
 
Back
Top Bottom