Nimejichanganya kuoa mwanamke mwenye mimba

Mwezi watano katika mihangaiko yangu nikakutana na mdada mmoja nikamwelewa tukayajenga mwisho tukakubaliana kuishi pamoja.

Alinieleza changamoto zinazomkabili huku akiwa na mimba ya miezi 2 anasema baba wa mtoto wamepotezana ni watu waliokutana katika kudanga hivyo hajui namna ya kumpata.

Hivyo basi nikajitoa kwa nia ya kumpata mke na kutoa msaada. Tukakubaliana itakuwa ni siri yetu na nikimuoa mtoto atatambulika ni wangu kawaida.

Sasa basi tukakaa pamoja kama miezi miwili akaniambia nimtambulishe kwa wazazi nikafanya hivyo nikampeleka Kwa wazazi wakamwona na wakampenda.

Sasa baada yakurudi mjini akaanza dharau ananidharau mpaka aibu Kwa majirani Yani ananifokea kama mtoto.

Kibaya zaidi anafanya kosa nikimweleza anakuwa mkali huku akisema kwa sauti "unafanya hivi kwasababu sio damu yako" ameshatangaza Kwa majirani wote kuwa mimba sio yangu.

Mwisho ameamuwa kuongea maneno mengi ya aibu na dharau kisha akaondoka mwenyewe. Ikumbukwe kwamba ameshataka kuondoka zaidi ya mara tatu nikamzuia akaona kama namng'angania akazidisha jeuri na dharau.

Sasa alipoamuwa kuondoka alisema hatarudi nyuma kwanza kwangu palikuwa panamtesa analishwa vyakula ambavyo hataki kwani yeye anataka ale chipsi Kila siku. Akafikia hatua ya kuniambia mimi sio mwanaume.

Mimi nikamuacha akakusanya virago vyake akaondoka zake mwenyewe. Sasa cha kushangaza kesho yake tu anaanza kuomba kurudi nikamwambia mimi ndio sirudi nyuma nenda kakae huko huko Kwa walio wanaume.

Akaenda akapangisha jirani na hapa napoishi mimi kisha ananisumbua sana anasema anateseka anaomba msamaha lakini mimi simtaki tena lakini kwaupande mwingine mimi roho inaniuma mimba sio yangu lakini Kuna roho ya huruma ninayo juu yake.

Ukizingatia mimba imefika miezi 8 ananiambia anataka vifaa vya kujifungulia na analala njaa hana chakula na analala kwenye mkeka.

Naomba ushauri nifanyaje nashindwa nitawaelezaje nyumbani kuhusu hili suala.
HUYO MWANAMKE NI MPUMBAVU ACHANA NAYE KABISA.
 
Usimrudiane nae kwasababu ya huruma ,

Nakushauri uhame apo ulipopanga asijue YOYOTE anaekujua ulipohamia
 
Umevumilia hiyo mimba, uvumilie na matusi tena!! Hayo matusi yanakuonyesha kuwa umeingia choo cha wanawake. Kimbia haraka.
 
Sielewe nicheke ama nikuhurumie ama nifanyeje,kwa makusudi kabisa ukiwa na akili timamu umeamua kulea bao la mme mwenzio?
Pamoja na matukio yote bado hujakoma baba huruma?kama ana shida kweli si arudi nyumbani kwao,hana wazazi?
Mtu wa aina yako ni hasara kwa wazazi.
 
Mwezi watano katika mihangaiko yangu nikakutana na mdada mmoja nikamwelewa tukayajenga mwisho tukakubaliana kuishi pamoja.

Alinieleza changamoto zinazomkabili huku akiwa na mimba ya miezi 2 anasema baba wa mtoto wamepotezana ni watu waliokutana katika kudanga hivyo hajui namna ya kumpata.

Hivyo basi nikajitoa kwa nia ya kumpata mke na kutoa msaada. Tukakubaliana itakuwa ni siri yetu na nikimuoa mtoto atatambulika ni wangu kawaida.

Sasa basi tukakaa pamoja kama miezi miwili akaniambia nimtambulishe kwa wazazi nikafanya hivyo nikampeleka Kwa wazazi wakamwona na wakampenda.

Sasa baada yakurudi mjini akaanza dharau ananidharau mpaka aibu Kwa majirani Yani ananifokea kama mtoto.

Kibaya zaidi anafanya kosa nikimweleza anakuwa mkali huku akisema kwa sauti "unafanya hivi kwasababu sio damu yako" ameshatangaza Kwa majirani wote kuwa mimba sio yangu.

Mwisho ameamuwa kuongea maneno mengi ya aibu na dharau kisha akaondoka mwenyewe. Ikumbukwe kwamba ameshataka kuondoka zaidi ya mara tatu nikamzuia akaona kama namng'angania akazidisha jeuri na dharau.

Sasa alipoamuwa kuondoka alisema hatarudi nyuma kwanza kwangu palikuwa panamtesa analishwa vyakula ambavyo hataki kwani yeye anataka ale chipsi Kila siku. Akafikia hatua ya kuniambia mimi sio mwanaume.

Mimi nikamuacha akakusanya virago vyake akaondoka zake mwenyewe. Sasa cha kushangaza kesho yake tu anaanza kuomba kurudi nikamwambia mimi ndio sirudi nyuma nenda kakae huko huko Kwa walio wanaume.

Akaenda akapangisha jirani na hapa napoishi mimi kisha ananisumbua sana anasema anateseka anaomba msamaha lakini mimi simtaki tena lakini kwaupande mwingine mimi roho inaniuma mimba sio yangu lakini Kuna roho ya huruma ninayo juu yake.

Ukizingatia mimba imefika miezi 8 ananiambia anataka vifaa vya kujifungulia na analala njaa hana chakula na analala kwenye mkeka.

Naomba ushauri nifanyaje nashindwa nitawaelezaje nyumbani kuhusu hili suala.
Kwa hakika hakukosea kusema "Wewe sio Mwanaume", the rest watakuja kumalizia wengine
 
Mapenzi na huruma havikai pamoja mkuu, achana na huyo mshenzi wa tabia. Shukuru sana hilo baya limekuepuka, kama una huruma sana msaidie gharama ya vifaa vya kujifungulia ila sio kumrudisha kwako..
Unachukua mwanamke mwenye mimba ya mtu mwingine yanini? Ng'ombe tu ndio unaweza mchukua akiwa na mimba ila sio binadamu. Nna imani umejifunza na usirudie kosa.
NAKAZIA
 
Daa eti ananidharau na kunifokea kwa hiyo hapo wewe ndio umepanga kuoa au ndio unaolewa hivyo.
Hivi wanawake wa hivyo huwa mnawaokota wapi, mtu akikufanyia dharau piga chini endelea na maisha mengine mkuu
Sasa mwanaume kama umelegea kufikia kuoa mdangaji unataka akuheshimu vipi wakati unaonekana popoma
 
Naomba ushauri nifanyaje nashindwa nitawaelezaje nyumbani kuhusu hili suala.

20240910_234515.jpg
 
rudi tena kwa wazazi wake, na wako na uwaeleze ukweli kama ulivyotuelekeza sisi hapa, kisha waambie kabisa kwamba hakuna harusi tena na hauko na huyo mwanamke, kabla hujaonekana wewe ni tatizo, mkuu suala la kujifungua ni suala la kufa na kupona, chukua tahadhali mapema, kwa maelezo yako huyo mwanamke humpendi tena bali unamuonea huruma, na iko hivyo, si kila mwanamke unayempenda wewe naye anakupenda pia, wewe ni kama daraja kwake, hakufai huyo, huwa sipendagi kushauri watu kuhusu mapenzi, lakini imenibidi sababu nilishawai kuoa single mother, niliyokutana nayo najua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom