Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

Acha wana wale maisha wewe.
 
Kimaendeleo ukoje mkuu? Natamani sana kujua kwa miaka saba upo kazini na hukopi hata mia, umewezaje kupiga hatua za kimaendeleo?
 
Dah!! yani ukisoma comments nyingi humu jinsi watu wanavyomponda huyo aliye nunua gari kwa mkopo, unaweza kudhani kuwa wananidhamu saana ya fedha. Lakini ukitokea ukachunguza hali ya kiuchumi ya kila mmoja utakuta ni mbaya na ya kukatisha tamaa hata kuliko ya huyo mkopaji. Kwenye haya maisha kila mtu ana kipaumbele chake, ni vile tu unaona kipaumbele chako ni cha muhimu na cha thamani kuliko cha mwenzio ndo maana nyuzi kama hizi zinaanzishwa na kukejeli vipaumbele vya wengine.

Jinsi watu wanavyo jinasibu humu ndani kuhusu ujuzi wao wa elimu ya fedha ingekuwa hivyo hii nchi ingekuwa na matajiri wengi sana.
 
Kopa mkopo usizidi miaka mitatu.
Huu wa miaka tisa unalipa mara mbili au tatu yake,ukibeba gharama za kuendesha bank kwa mshahara wako huku ukikatwa pesa ukigawana kidogo chako na hawa wezi.
 
Mbaya zaidi siku hizi watumishi uhitaji kwenda bank unakopa tu kupitia simu yako hata ukiwa kijijini ili ujimalize kabisa unawasiliana tu na HR wako anakupitishia tu kwenye system unajimaliza mwenyewe
 
Kwahy asijenge aendelee kumlipa mwenye nyumba sio?
 
Bila mikopo unapataje maendeleo, imagine una mshahara wankawaida kabisa, unafanyaje kupata maendeleo kama hukopi?

Comments nyingi zimekuwa za kuponda, tuambieni nyie mnaishije na kupata maendeleo bila kukopa.
 
kweli kqbisa mtu anakupa mchongo kwa kukuangalia upoje huna gari inampa mawazo sasa siku ikiwa inahitajika mchongo ufike kwa haraka si atasema daladala leo zina jaza kwahy amekosa usafir
 
Bila mikopo unapataje maendeleo, imagine una mshahara wankawaida kabisa, unafanyaje kupata maendeleo kama hukopi?

Comments nyingi zimekuwa za kuponda, tuambieni nyie mnaishije na kupata maendeleo bila kukopa.
Lazima ukope hata km utalipa mara 3 ila ulichokopa una uhakika kitakunufaisha na kukupa faida zaidi ya mara 3 ulizolipa mkopo wote, nimewahi kukopa hua nakopa na nitaendelea kukopa kwa manufaa ya faida sio hasara yaan mzani lazima u-balance, unachokopa kisizidi faida ya kile ulichokopa km kikizidi basi usikope achana na huo mkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…