Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
Acha wana wale maisha wewe.
 
Mwaka wa 7 kazini sasa na sijawahi hata kufikiria mambo ya mikopo.

Wengi wa staffs wenzangu waliochukua mikopo kwa mambo mbalimbali, hakuna walilofanikisha, tuko nao level moja, ila wao stress ya mikopo inawatesa.

Kuna Theory inasema hiviii: "99% ya employees huwa wana idea ya ujasiriamali pindi wanapoajuriwa, na wengi huingia kwenye ujasiriamali. Lakini ni 1% tu ndiyo hufanikiwa kujikwamua kiuchumi".
Kimaendeleo ukoje mkuu? Natamani sana kujua kwa miaka saba upo kazini na hukopi hata mia, umewezaje kupiga hatua za kimaendeleo?
 
Dah!! yani ukisoma comments nyingi humu jinsi watu wanavyomponda huyo aliye nunua gari kwa mkopo, unaweza kudhani kuwa wananidhamu saana ya fedha. Lakini ukitokea ukachunguza hali ya kiuchumi ya kila mmoja utakuta ni mbaya na ya kukatisha tamaa hata kuliko ya huyo mkopaji. Kwenye haya maisha kila mtu ana kipaumbele chake, ni vile tu unaona kipaumbele chako ni cha muhimu na cha thamani kuliko cha mwenzio ndo maana nyuzi kama hizi zinaanzishwa na kukejeli vipaumbele vya wengine.

Jinsi watu wanavyo jinasibu humu ndani kuhusu ujuzi wao wa elimu ya fedha ingekuwa hivyo hii nchi ingekuwa na matajiri wengi sana.
 
Kopa mkopo usizidi miaka mitatu.
Huu wa miaka tisa unalipa mara mbili au tatu yake,ukibeba gharama za kuendesha bank kwa mshahara wako huku ukikatwa pesa ukigawana kidogo chako na hawa wezi.
 
Mbaya zaidi siku hizi watumishi uhitaji kwenda bank unakopa tu kupitia simu yako hata ukiwa kijijini ili ujimalize kabisa unawasiliana tu na HR wako anakupitishia tu kwenye system unajimaliza mwenyewe
 
Watu wengi wanajidanganya eti huwezi kuendelea bila kukopa. Kimsingi unakopa ili uzalishe uweze kulipa riba na wewe kubaki na faida.

So kabla ya kukopa piga hesabu. Riba ni shs ngapi kwa mwezi? Je utapata faida ya kiasi gani kwa mwezi? Je faida ni kubwa kuliko riba?

Kama faida ni kubwa kuliko riba unaweza kukopa.

Sasa tatizo la watu wengi wanakopa wanaenda kutumia mikopo kwenye vitu visivyo zalisha kama kununua gari au kujenga nyumba.
Kwahy asijenge aendelee kumlipa mwenye nyumba sio?
 
Bila mikopo unapataje maendeleo, imagine una mshahara wankawaida kabisa, unafanyaje kupata maendeleo kama hukopi?

Comments nyingi zimekuwa za kuponda, tuambieni nyie mnaishije na kupata maendeleo bila kukopa.
 
Kusema kweli kwa mshahara wa watumishi wa kawaida gari ni gharama maana kimsingi ni liability na si asset.
Inahitaji matengenezo, mafuta, bima hapo sometimes hujadaiwa parking na rushwa kwa wazee wa barabarani.
Lakini pia gari inaweza kuwa asset. Sisi wazee wa mtaa, unaitwa kwenye deal unaenda kukutana na tajiri anaanza kukuzoom toka unaingia. Akiona umechoka anaweza kukunyima hata huo mchongo.
Lakini ukienda unafika pale uko safi, una usafiri, basi anajua huyu huu mchongo atauweza na amezoea kushika pesa ndiyo maana ameweza kuafford na usafiri.
So sometimes unamiliki chombo kama kuongeza tu thamani yako ili kikupe miamala zaidi.
kweli kqbisa mtu anakupa mchongo kwa kukuangalia upoje huna gari inampa mawazo sasa siku ikiwa inahitajika mchongo ufike kwa haraka si atasema daladala leo zina jaza kwahy amekosa usafir
 
Bila mikopo unapataje maendeleo, imagine una mshahara wankawaida kabisa, unafanyaje kupata maendeleo kama hukopi?

Comments nyingi zimekuwa za kuponda, tuambieni nyie mnaishije na kupata maendeleo bila kukopa.
Lazima ukope hata km utalipa mara 3 ila ulichokopa una uhakika kitakunufaisha na kukupa faida zaidi ya mara 3 ulizolipa mkopo wote, nimewahi kukopa hua nakopa na nitaendelea kukopa kwa manufaa ya faida sio hasara yaan mzani lazima u-balance, unachokopa kisizidi faida ya kile ulichokopa km kikizidi basi usikope achana na huo mkopo
 
Back
Top Bottom