Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

jozee jose

Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
52
Reaction score
120
Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
 
Waalimu huwa wanafundishwa kozi ya ujinga kwa siri wakiwa vyuoni? Hakuna mtu makini atachukua mkopo bila kupiga vizuri hesabu za riba. Na inajulikana ukilipa mapema ndo riba inakuwa ndogo. 10m kuilipa kwa 6yrs ni umaskini uliokithiri.
 
Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Mwaka wa 7 kazini sasa na sijawahi hata kufikiria mambo ya mikopo.

Wengi wa staffs wenzangu waliochukua mikopo kwa mambo mbalimbali, hakuna walilofanikisha, tuko nao level moja, ila wao stress ya mikopo inawatesa.

Kuna Theory inasema hiviii: "99% ya employees huwa wana idea ya ujasiriamali pindi wanapoajuriwa, na wengi huingia kwenye ujasiriamali. Lakini ni 1% tu ndiyo hufanikiwa kujikwamua kiuchumi".
 
Kheri yeye wengine tuna tafuta nafasi VETA
 
Attachments

  • Screenshot_20250314_121918_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20250314_121918_WhatsApp.jpg
    92.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom