Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
Kasome tena. hivi unaijua thamani ya fedha au Time value of money? shilingi ya leo si ya jana mkuu. Tuache kulalamika vitu ambavyo vipo wazi. Hivi shilingi uliyokopa leo thamani yake au vitu inavyoweza kununua ni hivihivi miaka mitano ijayo?
 
Soma vizuri upya mkuu, uelewe ninachozungumzia, au nawe ni muhanga wa mikopo?😄😄 pole komaa kulipa ni sehemu ya maishs
 
Bila kukopa Dangote asingejenga kiwanda cha Cement Mtwara
Watu wengi wanajidanganya eti huwezi kuendelea bila kukopa. Kimsingi unakopa ili uzalishe uweze kulipa riba na wewe kubaki na faida.

So kabla ya kukopa piga hesabu. Riba ni shs ngapi kwa mwezi? Je utapata faida ya kiasi gani kwa mwezi? Je faida ni kubwa kuliko riba?

Kama faida ni kubwa kuliko riba unaweza kukopa.

Sasa tatizo la watu wengi wanakopa wanaenda kutumia mikopo kwenye vitu visivyo zalisha kama kununua gari au kujenga nyumba.
 
Mwisho wa point yangu ndipo palipokuwa na hoja yangu
 
Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
Kusema kweli kwa mshahara wa watumishi wa kawaida gari ni gharama maana kimsingi ni liability na si asset.
Inahitaji matengenezo, mafuta, bima hapo sometimes hujadaiwa parking na rushwa kwa wazee wa barabarani.
Lakini pia gari inaweza kuwa asset. Sisi wazee wa mtaa, unaitwa kwenye deal unaenda kukutana na tajiri anaanza kukuzoom toka unaingia. Akiona umechoka anaweza kukunyima hata huo mchongo.
Lakini ukienda unafika pale uko safi, una usafiri, basi anajua huyu huu mchongo atauweza na amezoea kushika pesa ndiyo maana ameweza kuafford na usafiri.
So sometimes unamiliki chombo kama kuongeza tu thamani yako ili kikupe miamala zaidi.
 
Sio degre holder
Tutamlaumu bure ila ukweli ni kwamba wengi hawana maarifa ya kifedha. Hiyo yote inatokana na misingi tuliyojengewa sio ya kutafuta elimu ni kuikimbia elimu.

Sehwmu ninayotafutia kipato kuna mtu niliwahi kumtamkia issues za UTT nilipugwa butwaa aliponiambia hao UTT wana tofauti na gani na Kalyinda au LBL. Nkamuuliza LBL ni nini na UTT ni nini akajibu mi najua hizo zote watu wanaweka pesa tu.

Sasa imagine huyo ni degree holder ameshindwa kutafuta maarifa ameamua kurahisisha mambo kwa style hiyo. Niliamua kumuacha abaki kama alivyo.
degree si shida degree ya pharmacy huwezi fananisha na degree ya mtu wa account fieldya fedha ni sawa na field ya health account hajui kitu naye mpharmasia anashangaa hujui hii,,,, shida haianzii hapo isitoshe kuna baadhi ya degree holder hawajui hata UTT ni nn na ni field za business na accounting,,, vitu vingine vinahitaji uwezo binafsi kufatilia mambo hzo lbl sijui kuzijua ni rahisi sababu ya nguvu kubwa wanaotumia washawishi watu wenye akili fup, wavivu kufanya kazi na wanaopenda mitelezo walainike
 
Tumia akili anachosema jamaa anakielewa ww umekalili Time value of Money hajasema bank wapunguze au wasiweke riba anajaribu toa elimu juu ya namna bora ya kuweka maisha kuepuka vitu visivyo na msingi hio time value of money na gari ulonunua mbna hujasema lina depreciation 😂 acha kukalili vitu
Kasome tena. hivi unaijua thamani ya fedha au Time value of money? shilingi ya leo si ya jana mkuu. Tuache kulalamika vitu ambavyo vipo wazi. Hivi shilingi uliyokopa leo thamani yake au vitu inavyoweza kununua ni hivihivi miaka mitano ijayo?
 
Amewaonyesha kuwa ana gari. Gari limepaki chini ya mwarobaini shuleni, kila mtu anajua la nani...dadeeki wanafunzi walionywa wasicheze karibu ni gari la sivyo wangeona cha mtema kuni 😀 roho yake kwaaatu. Hayo mengine mtajua ninyi kwani kawafuta kuwaomba hela
 
Mwaka wa 7 kazini sasa na sijawahi hata kufikiria mambo ya mikopo.

Wengi wa staffs wenzangu waliochukua mikopo kwa mambo mbalimbali, hakuna walilofanikisha, tuko nao level moja, ila wao stress ya mikopo inawatesa.

Kuna Theory inasema hiviii: "99% ya employees huwa wana idea ya ujasiriamali pindi wanapoajuriwa, na wengi huingia kwenye ujasiriamali. Lakini ni 1% tu ndiyo hufanikiwa kujikwamua kiuchumi".
Bado mtoto wewe utajaa tu kwenye mfumo
 
Amewaonyesha kuwa ana gari. Gari limepaki chini ya mwarobaini shuleni, kila mtu anajua la nani...dadeeki wanafunzi walionywa wasicheze karibu ni gari la sivyo wangeona cha mtema kuni 😀 roho yake kwaaatu. Hayo mengine mtajua ninyi kwani kawafuta kuwaomba hela
Alieshauri ni rafiko ake maana hata mwalimu anajutia hv vitu huwez elewa usipokua navyo ukiwa na jicho au upande wa wanafunzi
 
Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
Kuishi maisha ya hali juu kuliko kipato ni janga kinalotusumbua wengi.

Ukiweza kuishi ndani ya kipato chako hautawezi kusumbuka
 
Back
Top Bottom