Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

Bila kukopa Dangote asingejenga kiwanda cha Cement Mtwara
Tofautisha mikopo ya matajiri, Level za kina dangote hakopi kwa kuwa hana fedha, kuna financial intelligence huwa zinawafanya matajiri wakope ili kuendesha mambo yao na sio kwamba wamepungukiwa hela 😁
 
Uzi umenifikia too late,pengine kama ningekutana na wewe mapema nisingefikia huku,mkopo unaofaa ni ule usiozidi miaka 3
 
Seriously, kukopa ili kununua gari ni risk.

Kutegemea na mkoa aliopo inawezekana hata swala la bolt haliwezekani.

Kinachotokea ndiyo unakuta mtu kila training anataka aende yeye. Yupo kwenye hiyo training inakuja nyingine analazimisha aunge training mbili huko huko.

Kila safari anaitolea macho. Kazi kukimbizana na madokezo tu.

Sasa walimu mna hata madokezo? Training? Na si ndo mafunzo yenu yale mnalipwa buku tatu?
 
Tofautisha mikopo ya matajiri, Level za kina dangote hakopi kwa kuwa hana fedha, kuna financial intelligence huwa zinawafanya matajiri wakope ili kuendesha mambo yao na sio kwamba wamepungukiwa hela 😁
Ndio elimu niliyoitoa hapo maana yake kopa ila kopa kwa faida, yaan mfano ukikopa million 100 basi jua hio million 100 itakuingizia million 500 ndani ya muda fulani, kukopa gari sio vibaya swali ni kwamba analitumiaje hilo gari kurudishia pesa ya mkopo? Unaelewa hapo sijui
 
Seriously, kukopa ili kununua gari ni risk.

Kutegemea na mkoa aliopo inawezekana hata swala la bolt haliwezekani.

Kinachotokea ndiyo unakuta mtu kila training anataka aende yeye. Yupo kwenye hiyo training inakuja nyingine analazimisha aunge training mbili huko huko.

Kila safari anaitolea macho. Kazi kukimbizana na madokezo tu.

Sasa walimu mna hata madokezo? Training? Na si ndo mafunzo yenu yale mnalipwa buku tatu?
🙌🙌 safari kwa mwalimu ni ngumu
 
Ukianza tu kuwaza wao (Bank) watachukua kiasi gani kwenye mkopo wako then huwezi kukopa kamwe!

Kikubwa ni kukopa kwa malengo yanayoeleweka tu!
 
Mwaka wa 7 kazini sasa na sijawahi hata kufikiria mambo ya mikopo.

Wengi wa staffs wenzangu waliochukua mikopo kwa mambo mbalimbali, hakuna walilofanikisha, tuko nao level moja, ila wao stress ya mikopo inawatesa.

Kuna Theory inasema hiviii: "99% ya employees huwa wana idea ya ujasiriamali pindi wanapoajuriwa, na wengi huingia kwenye ujasiriamali. Lakini ni 1% tu ndiyo hufanikiwa kujikwamua kiuchumi".
Yaani mtu akope m 10 mfano akafanya jambo halafu uwe naye level moja na wewe unasubiri 600k kwa mwezi???

Kama hili ni la kweli basi jua umezungukwa na kundi la wajinga na usiposhituka na wewe utaambukizwa ujinga.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka wa 7 kazini sasa na sijawahi hata kufikiria mambo ya mikopo.

Wengi wa staffs wenzangu waliochukua mikopo kwa mambo mbalimbali, hakuna walilofanikisha, tuko nao level moja, ila wao stress ya mikopo inawatesa.

Kuna Theory inasema hiviii: "99% ya employees huwa wana idea ya ujasiriamali pindi wanapoajuriwa, na wengi huingia kwenye ujasiriamali. Lakini ni 1% tu ndiyo hufanikiwa kujikwamua kiuchumi".
Kama miaka yote saba ujakopa, na bado hauna nyumba kali na ipo location ya maana, na huna gari basi na wewe inabidi tukuchunguze pia.

Kwa mishahara yetu ikifanya saving inakuchukua almost miaka 10 au zaidi kupata nyumba na gari. Kama mtu ameamua kuchukua risk basi tumpe hongera zake tu.
 
Kimaendeleo ukoje mkuu? Natamani sana kujua kwa miaka saba upo kazini na hukopi hata mia, umewezaje kupiga hatua za kimaendeleo?
Umeulizwa swali moja zuri sana.

Kuna mwalimu mkuu mmoja alikuwa na notion kama ya huyu mwamba hakuwahi kukopa ila alikuwa na maisha magumu kuliko hata wenye mikopo. Akiitwa kwenye vikao katani anatembea kwa miguu kwenda katani zaidi ya km 7, hana hata TVS.

Wakati mwingine kukopa ni security, kazi zenyewe za watu hizi. Kuna mwamba mmoja alipona kufukuzwa kazi kisa tu alikuwa na mkopo mkubwa benk m 20+.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Maisha ya sasa usipokuwa na financial literacy (elimu ya pesa) unaweza kujikuta umeingia kwenye utumwa wa matumizi makubwa, ambayo baadaye yanakupeleka kwenye uraibu wa mikopo usioisha.

Mambo haya huwa yanawakumba sana watumishi wa serikali, hasa walimu. Watumishi wa sasa wengi wanatamani kuishi maisha ya ndoto zao, kama kumiliki nyumba nzuri, kuwa na magari, kuwa na miradi ya kuongeza kipato kama mashamba na fremu za biashara.

Kutokana na kuwa na mishahara ya wastani huku wengi wao wakiwa na extended family, hushindwa kujizuia na msukumo wao wa ndani wa kutaka kulazimisha mambo bila kujali wataathirika vipi.

Mfano, kuna jamaa yangu mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali (mwalimu) alitaka kununua Toyota IST kwa bei ya Shilingi milioni 14. Alikuwa na Shilingi milioni 6 na alihitaji kukopa benki kiasi cha Shilingi milioni 10 ili aweze kukamilisha manunuzi yake.

Kwa sasa, karibu kila benki inatoza riba ya asilimia 16. Jamaa alishawishiwa achague muda mrefu wa malipo ili alipe kidogo kidogo, akaingia mkenge.

Kitu ambacho hakujua ni hiki: (72 ÷ riba), yaani (72 ÷ 16) = 4.5. Mkopo wowote kwa riba hiyo ukifika miaka 4.5 na kuendelea, utalipa mara mbili ya kiasi ulichokopa. Hivyo, kama alichukua milioni 10, atalipa milioni 20.

Sasa mwenzangu alichukua mkopo wa miaka 6 ili awe analipa Shilingi 300,000 kila mwezi. Aliposanuliwa kwamba atalipa mara mbili ya alichokopa, alichoka sana maana ilikuwa too late.

Hivi ninavyoandika haya, hana hamu ya kuendesha gari hilo, kwani anategemea mshahara pekee na gari halimuingizii pesa, bali linahitaji gharama za mafuta na matengenezo mbalimbali.

Watumishi mkumbuke kuwa serikali imewaajiri wenyewe, haijaajiri matumizi yenu.

Kwa haraka, pato lako kwa siku ni Shilingi 20,000. Hivyo, chunga matumizi yako, usijitumbukize kwenye mzigo wa madeni bila mpango.
mkeka nimeuelewa mkuu, ila hapo kwenye 4.5 ndo hujafafanua vizuri. hii 4.5 ina nini cha kufanya na kulipa mkopo twice???

anyway, kwa riba ya 16% ambayo ni sawa na 1.6M/mwaka, mtu huyu anapaswa kulipa jumla ya 19,600,000/=TZS kwa kipindi cha miezi 72 (5 years). hapo unaeleweka vizuri. tuambie sasa hiyo 4.5 nayo ina maana gani????
 
Back
Top Bottom