Nimejiondoa kwenye makundi sogozi ya harusi

Nimejiondoa kwenye makundi sogozi ya harusi

Joined
Feb 11, 2023
Posts
96
Reaction score
182
Jumla ya magroup sita yananitaka nitoe si chini ya laki laki.

Nimeleft. Sitaki ujinga.

Hizi ndoa za maghalama hizi ni upuuzi mtupu. Watu kuoana muoane wenyewe mizigo mtubeneshe sisii, shenzi.

Mimi natoaga tu mwanaharamu apite mara zote kulipishana mahela ni ujuha.

Kwani mnashindwa nini kujichanga mkala ubwabwa na ndugu zenu au washkaji wako? Chai, soda kalimati tosha kuolea au kuoa. Yanini uchamgishe pesa uipoteze, na kiasi hicho lets say 15 millions wewe mwenyewe unakihitaji.

Hakikuumi kukipoteza kuwapa deal wapikaji? Wapambaji? Madomo kaya aka wasema hovyo ma MC. Unajisikiaje kupoteza pesa kukodi magari? Kulipia millions ukumbi ambao ni siku moja kwa nini usiipate millioni ukannua matofali ukajenga?

Mimi nadhani ule mapango wa kulipa kodi ya sherehe ianzishwe, kutokomeza huu upuuzi.

Cha ajabu wengi mnaoana kwa mamilions of money hamdumu kwenye ndoa na pesa huishia kupotea na kwamba umewatia hasara wachangiaji.

Nimeleft magroup ya harusi si kwa nia Mbaya ni kwa ustawi wa maisha ya watu wanaoumia na hawasemi.
 
Umeamua kuwa Anti-Social
Sio Antisosho naunga mkono hoja wenye harusi mnakwaza sana unaweza kulala kuamka unakuta umeaddiwa kwenye group la michango ya Harusi mbaya zaidi uwa mnajipangia mchango tena kuanzia 30k wakipiga mahesabu kwenye kamati ukiangalia pesa inayohitajika na maisha ya wanandoa mtarajiwa. Unabaki kustaajabu tu kweli TUSIPANGIANE MAISHA ila wamichango ya harusi mmezidi
 
Unataka sisi maMC tukale wapi ndugu yangu, changeni nasi tupate za kusomesha watoto...
Ninyi na madalali wa nyumba, viwanja na magari ndugu mmoja.

Mc kule kijijini analipwa shilingi ngapi, kwani uemc pay slip ni sh ngapi, kwani shilling ngapi.

Katika watu ambao nawachukia ni MC na madalali.

Gari sh million 24 yeye ana million 3 ya burebure tu.

Mara nyingi nikitaka vyumba mm mwenyewe mguu kwa mguu
 
Wewe bado ulikuwepo kwenye huo upumbavu wa wanawake?[emoji849][emoji849] swala la ndoa wewe unatakiwa kuwa mualikwa na mualikwa ni yule ambaye aja andaa harusi ....ukichangia pesa wewe unakuwa kwenye kundi la walika siyo mualikwa ...harusi ni wajibu wa muoaji na familia yake ....kukubali kuchangishwa harusi ni umama wa hali ya juu kabisa ...wao waowaji kama wanataka anasa ya kuvunja rekodi kwenye ndoa yao wao ndiyo watoe hiyo pesa wenyewe na familia yao.
Mambo ya kimama mama mtoto wa kiume utakiwi kuyakubali hata hapa kwenye huu uzi tizama kwa makini wanawake watatoka povu kukupia au kuonyesha kuto kukubaliana na wewe
Wanawake wanaolamisha ndoa na kuandaa sherehe mwanaume anakua kama ceremonial. Wanawake wa aina hii nawadharau sana.

Unakuta ana force mjumbi amuoe anazama anaanzisha shughuli ya hatari na ukute na jombi naye anamega nje humo madem kibao.

Hao ndio wananikasikia sana
 
Hao ndio wananikasikia wale waelewa anarakani sehemu ya pesa waanzie maisha.

Majuzi kuna sherehe ten million na kuku wameoza emergine
 
Huu utamaduni wa kuchangishana ifike wakati tu tuone ni kama changamoto ya kutuongezea umasikini wa kipato tu badala ya jambo la furaha.

Na ndio maana ndoa za siku hizi huwa hazidumu kwasababu watu wanatoa pesa kuchangia shughuli ila wanasononeka lakini wanatoa tu kwasababu ya kuficha aibu na kutokuonekana sio watoaji kwenye mambo ya wengine.

Mtu akiwa anakuomba mchango anaona amekuomba wewe tu na anahisi anahaki ya kupewa na wewe ila anasahau kuwa wakati anakuomba wewe pengine kuna watu wengine zaidi ya 10 wameshakuomba au watakuja kukuomba. Na hii hutokea kwa kufuatana.

Matokeo yake unakuta ni kuwa na jukumu la kulipia zaidi ya laki tano hadi milioni kila mwaka kwenye michango tu. Hii ni kitu mbaya sana kiuchumi na inaleta shida sana kwa wale ambao nyakati hizi wana mizigo ya bili za kulipa. Kodi, gharama za ujenzi wa makazi mapya, ada za mtoto au watoto, bili za nyumbani, matumizi binafsi ya mke na muhusika, kusapoti familia zetu. Haya yote yanataka pesa hivi kwa kipato gani sasa hadi mtu aishi kwa amani?

Ndio maana watu muda wengine tunaonekana tuna mambo ya ajabu. Kumbe ni swala la kubadilika kwa mazingira na hali ya uchumi.
 
Back
Top Bottom