Nimekaa pale. Natazama tu wanaojipa vyeo vya Ujinga

Nimekaa pale. Natazama tu wanaojipa vyeo vya Ujinga

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
Eti msiba wa wengi ni harusi! Jiulize mbona matanga hayalaliwi ukumbini kwa taarabu na slow jam?

Eti siogopi kudaiwa, serikali yenyewe inadaiwa! Jiulize deni la nchi analipa nani kama sio wewe? Halafu tafakari lini serikali ilibeba deni lako? Akili itakaa sawa pindi utakapolala nje au kurudi usiku wa manane na kusepa alfajiri na kukwepa wadeni wako vichochoroni.

Eti nisome sana kwani nataka kuwa Rais/ mbunge?! Kazi zenyewe hakuna siku hizi?! Oyaa!! Elimu inakupa maarifa, maisha ni matokeo ya jitihada zako na bahati katika utafutaji!

Niolewe, nioe? Maisha ya bata nimwachie nani? Tambua umri wako ni sawa na plate number ya gari. Gari ikishachoka na kupitwa na wakati inasukumwa tu kwa njia mbili a) kwa bei ya nyanya na b) itapigwa bei kama chuma chakavu!

Mimi nimekaa palee, wewe umekaa wapi kucheki majenerali wengine wa kujipa vyeo vya ujinga?
 
Eti ooo pesa si kila kitu we zikose uone utavyopitwa na kila kitu.
Mi nimekaa pale nawatazama wajinga wzliofeli kuzinyaka wakizitamtakia kauli za kushindwa.
 
Eti ooo pesa si kila kitu we zikose uone utavyopitwa na kila kitu.
Mi nimekaa pale nawatazama wajinga wzliofeli kuzinyaka wakizitamtakia kauli za kushindwa.
Afu anajitapa "sisi tumepata bilioni kadhaa au timu yetu bongo ndo tajiri".
Aga kidogo mara anakutokea chemba kukupiga ukware wa buku.....
Mkate kelebu kabisa azinduke kwenda kutafuta hela
 
Eti..
Aliye juu mngonje chini.

Wote Ni wa udongoni tu, Akhera hamna pesa.

Weeeh..kama unaishi tafuta pesa upate mahitaji yako uishi kwa furaha!
 
Back
Top Bottom