Nimekata mawasiliano na mama yangu kwa sababu ya maneno ya kejeli ya mara kwa mara

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Katika ukuaji wangu mimi na mama yangu hatujawahi kuwa na uhusiano mzuri. Mara kwa mara amekuwa akinitamkia maneno ya kejeli na yeye chuki hadi nikawa najiuliza huyu ni mama yangu kweli?

Nimevumili kwa muda mrefu tangu nikiwa mdogo na maneno yale yalijenga chuki na kuweka sumu kwangu nikawa najiweka naye mbali hata shule ikifungwa sitamani kurudi nyumbani. Mama yeye ni mweupe ila baba mweusi sasa kwa bahati mbaya nikachukua rangi ya baba. Kuna wakati alikuwa akinikana mbele za watu kuwa mimi si mwanae kwa sababu hatujafafanana ikanibidi nianze kutumia cream niwe mweupe kama yeye labda hali itapungua.

Kuna muda nikaanza kunywa na vidonge vyakupungua lakini baadae nikaja kujikubali nikaona ni ujinga. Siwezi kumlazimisha mtu anipende nilivyojipata nikaondoka nyumbani na kuanza kujitegemea sijawi kurudi nyumbani ila nikawa napiga simu kuwajulia hali. Mara ya mwisho nilipiga simu nikawa naongea na mama akaniambia "Nimekuona umejiposti status, sasa na hilo li mwili mwanaume gani atakubali kukuoa? Embu pungua bwana upate mume." Nilimkatia simu nikaanza kulia mwenyewe.

Ile ndo ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana nae. Nilimblock na sijawahi kwenda nyumbani wala kupiga simu kuwajulia hali. Enough is enough.

Watu wengi hawajui madhara ya maneno ya chuki yanayotamkwa mara kwa mara. Kwangu mimi, madhara hayakuwa majeraha ya kuonekana kwa macho; yalikuwa ni majeraha ya kisaikolojia.
  • Kujichukia: Maneno yake yalinifanya niogope kujiangalia kwenye kioo. Nilijiona sifai na kujichukia kwa jinsi nilivyoumbwa.
  • Kupoteza Kujiamini: Nilianza kuamini kwamba rangi yangu na uzito wangu ni kikwazo cha mimi kupendwa au kukubalika katika jamii. Kauli za mama ziliniulia ujasiri kabisa na kwa muda mrefu nikawa na struggle na self identity.
  • Msongo wa Mawazo: Nilijenga ukuta wa upweke na kuishi kwa hofu, nikiwaza kuwa ulimwengu mzima unanitazama kwa jicho lile lile la dharau alilokuwa nalo mama yangu.
Sasa naishi peke yangu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, ninasikiliza ukimya wenye amani badala ya sauti za kuniponda. Nimejifunza kuipenda ngozi yangu na kuukubali mwili wangu. Kujitenga naye halikuwa kosa, bali ilikuwa ni njia pekee ya kuokoa maisha yangu na kulinda afya yangu ya akili. Mwisho wa siku, thamani yangu haipimwi kwa maneno ya chuki, bali kwa jinsi ninavyojithamini mimi mwenyewe.
 
Wazazi nao ni binadamu na wana mapungufu yao mengi tu, hilo ulifahamu.

Hivyo hutakiwi kuyachukulia maneno na matendo yao kama benchmark au reference point ya wema mara zote. Kipimo pekee cha Wema usio na swali ni Mungu pekee.

Usijiweke fungu la kukosa na ukawa mnyonge kwa maneno ya wazazi wako tu, ikiwa hukwenda kinyume na mapenzi ya Mungu kama ni mtu wa imani, keep moving confidently.
 
Ukweli siku zote ni mchungu! Kama mzazi amekushauri kupunguza mwili, punguza! Unene uliopitiliza unakaribisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza mfano kisukari, shinikizo la damu, nk. Hayo mambo ya kukosa kuolewa ni kijembe tu. Hivyo usitilie maanani.
 
Ktika ukuaji wangu mimi na mama yangu hatujawahi kuwa na uhusiano mzuri. Mara kwa mara amekuwa akinitamkia maneno ya kejeli na yeye chuki hadi nikawa najiuliza huyu ni mama yangu kweli?

Nimevumili kwa muda mrefu tangu nikiwa mdogo na maneno yale yalijenga chuki na kuweka sumu kwangu nikawa najiweka naye mbali hata shule ikifungwa sitamani kurudi nyumbani. Mama yeye ni mweupe ila baba mweusi sasa kwa bahati mbaya nikachukua rangi ya baba. Kuna wakati alikuwa akinikana mbele za watu kuwa mimi si mwanae kwa sababu hatujafafanana ikanibidi nianze kutumia cream niwe mweupe kama yeye labda hali itapungua.

Kuna muda nikaanza kunywa na vidonge vyakupungua lakini baadae nikaja kujikubali nikaona ni ujinga. Siwezi kumlazimisha mtu anipende nilivyojipata nikaondoka nyumbani na kuanza kujitegemea sijawi kurudi nyumbani ila nikawa napiga simu kuwajulia hali. Mara ya mwisho nilipiga simu nikawa naongea na mama akaniambia "Nimekuona umejiposti status, sasa na hilo li mwili mwanaume gani atakubali kukuoa? Embu pungua bwana upate mume." Nilimkatia simu nikaanza kulia mwenyewe.

Ile ndo ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana nae. Nilimblock na sijawahi kwenda nyumbani wala kupiga simu kuwajulia hali. Enough is enough.

Watu wengi hawajui madhara ya maneno ya chuki yanayotamkwa mara kwa mara. Kwangu mimi, madhara hayakuwa majeraha ya kuonekana kwa macho; yalikuwa ni majeraha ya kisaikolojia.
  • Kujichukia: Maneno yake yalinifanya niogope kujiangalia kwenye kioo. Nilijiona sifai na kujichukia kwa jinsi nilivyoumbwa.
  • Kupoteza Kujiamini: Nilianza kuamini kwamba rangi yangu na uzito wangu ni kikwazo cha mimi kupendwa au kukubalika katika jamii. Kauli za mama ziliniulia ujasiri kabisa na kwa muda mrefu nikawa na struggle na self identity.
  • Msongo wa Mawazo: Nilijenga ukuta wa upweke na kuishi kwa hofu, nikiwaza kuwa ulimwengu mzima unanitazama kwa jicho lile lile la dharau alilokuwa nalo mama yangu.
Sasa naishi peke yangu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, ninasikiliza ukimya wenye amani badala ya sauti za kuniponda. Nimejifunza kuipenda ngozi yangu na kuukubali mwili wangu. Kujitenga naye halikuwa kosa, bali ilikuwa ni njia pekee ya kuokoa maisha yangu na kulinda afya yangu ya akili. Mwisho wa siku, thamani yangu haipimwi kwa maneno ya chuki, bali kwa jinsi ninavyojithamini mimi mwenyewe.
Pole sana!! Jikubali na jipe confidence.

Kuna watu huwa wanasema nani kama mama sijui nini na nini, mara mama ndiyo mzazi lakini sometimes huwa naona wanageneralize too much.

Kitendo tu cha kubeba mimba siyo sababu sana ya Mama au mwanamke kupewa thamani hizo za kiasi hicho. Ni mgawanyiko wa majukumu tu naturally, watu wawili (Mme na Mke) hawawezi wakabeba mimba hiyohiyo moja at the same time, lazima mmoja abebe jukumu la kuibeba.

Kuna mama wengine ni Blockheads na nongwa sana.
 
Hiyo ni tough love mzee, mama yako hakuchukii ila anakuchanaga tu ili uwe vizuri...Wazazi wengine hawanaga soft love, akiwa na hajaridhishwa na wewe anakuchana makavu kwa hasira, lakini ni ili ujirekebishe..

Wazazi wengi naona wanawaambiaga watoto wao maneno magumu, ila wanawapenda na kuwaombea sana

maneno magumu kama hayo ni mama yako anaweza kukuambia tu, sababu akikuambia rafiki yako itakuaa uadui mkubwa
 
Mara ya mwisho nilipiga simu nikawa naongea na mama akaniambia "Nimekuona umejiposti status, sasa na hilo li mwili mwanaume gani atakubali kukuoa? Embu pungua bwana upate mume." Nilimkatia simu nikaanza kulia mwenyewe.
POLE kwa mengine mengi ambayo mama yako anakusimanga.

LAKINI, kwenye swala la kupungua (kuondoa unene), naungana nae. Jitahidi Upungue kama una mwili mkubwa sana, hii ni sababu za kiafya zaidi na sio hizo alizosema Mama yako.

Mwisho: Yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu. Ukizungumza na Mama yako focus na main point, mengine muachie yeye mwenyewe.
 
Ktika ukuaji wangu mimi na mama yangu hatujawahi kuwa na uhusiano mzuri. Mara kwa mara amekuwa akinitamkia maneno ya kejeli na yeye chuki hadi nikawa najiuliza huyu ni mama yangu kweli?

Nimevumili kwa muda mrefu tangu nikiwa mdogo na maneno yale yalijenga chuki na kuweka sumu kwangu nikawa najiweka naye mbali hata shule ikifungwa sitamani kurudi nyumbani. Mama yeye ni mweupe ila baba mweusi sasa kwa bahati mbaya nikachukua rangi ya baba. Kuna wakati alikuwa akinikana mbele za watu kuwa mimi si mwanae kwa sababu hatujafafanana ikanibidi nianze kutumia cream niwe mweupe kama yeye labda hali itapungua.

Kuna muda nikaanza kunywa na vidonge vyakupungua lakini baadae nikaja kujikubali nikaona ni ujinga. Siwezi kumlazimisha mtu anipende nilivyojipata nikaondoka nyumbani na kuanza kujitegemea sijawi kurudi nyumbani ila nikawa napiga simu kuwajulia hali. Mara ya mwisho nilipiga simu nikawa naongea na mama akaniambia "Nimekuona umejiposti status, sasa na hilo li mwili mwanaume gani atakubali kukuoa? Embu pungua bwana upate mume." Nilimkatia simu nikaanza kulia mwenyewe.

Ile ndo ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana nae. Nilimblock na sijawahi kwenda nyumbani wala kupiga simu kuwajulia hali. Enough is enough.

Watu wengi hawajui madhara ya maneno ya chuki yanayotamkwa mara kwa mara. Kwangu mimi, madhara hayakuwa majeraha ya kuonekana kwa macho; yalikuwa ni majeraha ya kisaikolojia.
  • Kujichukia: Maneno yake yalinifanya niogope kujiangalia kwenye kioo. Nilijiona sifai na kujichukia kwa jinsi nilivyoumbwa.
  • Kupoteza Kujiamini: Nilianza kuamini kwamba rangi yangu na uzito wangu ni kikwazo cha mimi kupendwa au kukubalika katika jamii. Kauli za mama ziliniulia ujasiri kabisa na kwa muda mrefu nikawa na struggle na self identity.
  • Msongo wa Mawazo: Nilijenga ukuta wa upweke na kuishi kwa hofu, nikiwaza kuwa ulimwengu mzima unanitazama kwa jicho lile lile la dharau alilokuwa nalo mama yangu.
Sasa naishi peke yangu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, ninasikiliza ukimya wenye amani badala ya sauti za kuniponda. Nimejifunza kuipenda ngozi yangu na kuukubali mwili wangu. Kujitenga naye halikuwa kosa, bali ilikuwa ni njia pekee ya kuokoa maisha yangu na kulinda afya yangu ya akili. Mwisho wa siku, thamani yangu haipimwi kwa maneno ya chuki, bali kwa jinsi ninavyojithamini mimi mwenyewe.
Ukiona hivyo mama yako hampendi Baba yako. Kama hawaishi wote, baba yako alimkataa mama yako sasa hasira zake anazileta kwako kwa vile una sura kama yeye. Ni kawaida, wengi wa mabinti mama zao wanawachukia sana huwezi amini kama ni watoto wao wa kuwazaa. Nikupe mfano mmoja wa member wa JF. Binti anampenda baba yake, ambayo ya kawaida, ilifika wakati mama yake mzazi alitoa sharti kwa baba yake kuwa aidha binti ahame na kama hahami, yeye atahama mpaka binti yake atakapoondoka katika nyumba ile. Huwezi amini, mama aliondoka. Binti alikuwa 20 yrs na anasoma Chuo day. Mpaka tukamhoji kuwa pengine anajichanganya na baba yake. Kwa muda mrefu mama yake alikuwa haishi nao. Baba yake aligoma kumfukuza mtoto kwani ni mtoto wa pale nyumbani na wakike.

Kwa hiyo Wild Flower ichukulie kama changamoto ya kawaida. Ipo siku utajua umuhimu wako na atakutafuta. Kikubwa jitahidi kuzisaka ngawira ukizipata atajileta tu.
 
Ukweli siku zote ni mchungu! Kama mzazi amekushauri kupunguza mwili, punguza! Unene uliopitiliza unakaribisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza mfano kisukari, shinikizo la damu, nk. Hayo mambo ya kukosa kuolewa ni kijembe tu. Hivyo usitilie maanani.
Mkuu hata mimi nikiwa mzazi huko mbeleni kuna maneno siwezi kuyatumia kwa mwanangu kama nataka abadilike. Kama wewe ni mzazi jifunze kutumia lugha ya kirafiki. Ukubwani nimekuja kugundua wengi wetu tuna trauma nyingi sana tumepata kutoka kwa familia. Na mtu usipokuwa makini unaweza ukaibeba kwa watoto na kizazi chako. We should stop being bitter parents.
 
Back
Top Bottom