Katika ukuaji wangu mimi na mama yangu hatujawahi kuwa na uhusiano mzuri. Mara kwa mara amekuwa akinitamkia maneno ya kejeli na yeye chuki hadi nikawa najiuliza huyu ni mama yangu kweli?
Nimevumili kwa muda mrefu tangu nikiwa mdogo na maneno yale yalijenga chuki na kuweka sumu kwangu nikawa najiweka naye mbali hata shule ikifungwa sitamani kurudi nyumbani. Mama yeye ni mweupe ila baba mweusi sasa kwa bahati mbaya nikachukua rangi ya baba. Kuna wakati alikuwa akinikana mbele za watu kuwa mimi si mwanae kwa sababu hatujafafanana ikanibidi nianze kutumia cream niwe mweupe kama yeye labda hali itapungua.
Kuna muda nikaanza kunywa na vidonge vyakupungua lakini baadae nikaja kujikubali nikaona ni ujinga. Siwezi kumlazimisha mtu anipende nilivyojipata nikaondoka nyumbani na kuanza kujitegemea sijawi kurudi nyumbani ila nikawa napiga simu kuwajulia hali. Mara ya mwisho nilipiga simu nikawa naongea na mama akaniambia "Nimekuona umejiposti status, sasa na hilo li mwili mwanaume gani atakubali kukuoa? Embu pungua bwana upate mume." Nilimkatia simu nikaanza kulia mwenyewe.
Ile ndo ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana nae. Nilimblock na sijawahi kwenda nyumbani wala kupiga simu kuwajulia hali. Enough is enough.
Watu wengi hawajui madhara ya maneno ya chuki yanayotamkwa mara kwa mara. Kwangu mimi, madhara hayakuwa majeraha ya kuonekana kwa macho; yalikuwa ni majeraha ya kisaikolojia.
- Kujichukia: Maneno yake yalinifanya niogope kujiangalia kwenye kioo. Nilijiona sifai na kujichukia kwa jinsi nilivyoumbwa.
- Kupoteza Kujiamini: Nilianza kuamini kwamba rangi yangu na uzito wangu ni kikwazo cha mimi kupendwa au kukubalika katika jamii. Kauli za mama ziliniulia ujasiri kabisa na kwa muda mrefu nikawa na struggle na self identity.
- Msongo wa Mawazo: Nilijenga ukuta wa upweke na kuishi kwa hofu, nikiwaza kuwa ulimwengu mzima unanitazama kwa jicho lile lile la dharau alilokuwa nalo mama yangu.
Sasa naishi peke yangu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, ninasikiliza ukimya wenye amani badala ya sauti za kuniponda. Nimejifunza kuipenda ngozi yangu na kuukubali mwili wangu. Kujitenga naye halikuwa kosa, bali ilikuwa ni njia pekee ya kuokoa maisha yangu na kulinda afya yangu ya akili. Mwisho wa siku, thamani yangu haipimwi kwa maneno ya chuki, bali kwa jinsi ninavyojithamini mimi mwenyewe.