Mpwimbe
JF-Expert Member
- Oct 13, 2023
- 455
- 818
Utapeli ni biashara kubwa na halali kabisa Tanzania.Biashara ya mabasi ni biashara ya kitapeli sana.
Enzi zile kuna darlux wakawa wanasema gari ina wifi hivyo watu wakawa wanalipishwa bei ya luxury ila ukiingia ndani kila siku mtaambiwa kwamba kifaa cha wifi kina matatizo.
Mbaya zaidi wakawa kama unatokea dar wanaenda kusimama kwenye kihoteli kimoja kiko bahi, mshikaji wangu alikula pale wali aliharisha nusu afe.
Vile nilikua mteja wao siku moja nikawaambia huu Uswahili wenu ipo siku hii kampuni itakufa, kweli Uswahili ukaiua darlux.
Maisha yamebadilika kidogo sasa long safari yoyote kama sijaenda na gari binafsi basi ni flight tu. Mabadi ni waswahili sana.
Na nchi hii ni FAILED STATE. Mambo yanaendeshwa kwa CONNECTION, NETWORKING na LOBBYING.
Watu wa Mabus Wana Wana watu bungeni kwaajili ya kutetea mambo yao.
Biashara ya Bus - Shabiby, Tabasamu
Betting - Abbas Tarimba
Watoto wa vigogo na wake zao - Salima Kikwete.
Vituo vya Mafuta - Tabasamu
Wale wasio na watu wa kuwasemea huko nuu ndio WANAPIGIKA