KERO Nimekoma kukopa mitandaoni, wanagawa namba yangu kwa watu ili wanipigie

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Aisee nilipata dharula nikakopa kwenye moja ya hizi app siku ya marejesho, sikuwa na kiasi husika. Walichokifanya wamegawa namba zangu kwa watu hata siwafahamu kwa siku, napigiwa simu hata Mia na watu tofauti.

Kisha wamewapigia ndugu zangu wa karibu waliopo kwenye contact list yangu.

Dah nimeamua liwalo na liwe maana wanasema watapost NIDA yangu mitandaoni na kuuambia umma kuwa mimi ni mhalifu hatari wa mtandao.

Msaada wa mawazo, kwa sasa nakunywa sana pombe kali ili kupunguza mawazo ila pombe ikiisha tatizo bado linabaki palepale
 
Lipa yakhe....... Ama zungumza nao vizuri wape ahadi ya uhakika. Nakushauri usikope zile pesa za halimashauri utatukwaza .
 
πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£β›ΉοΈβ€β™‚οΈβ›ΉοΈβ€β™‚οΈβ›ΉοΈβ€β™‚οΈ
 
Wape muda watapoa tu hao..
 
Badili line,,,,hata kama wanaijua nida yako sio hoja, itaondoa usumbufu wa kupigiwa simu ovyo ! Kopa kiasi unachomudu kurejesha,,,ona unadhalilika sas
 
Hao jamaa ni matapeli kiwango unachoomba hupewi kilekile mfano kama umeomba laki na nusu unapewa say laki na kumi halafu zinakuja kwa mafungu mafungu labda 20k 30k 40k na 60k na kila hela itadaiwa kivyake na kampuni tofauti tofauti mwishowe wanawapa namba wale jamaa wa tuma hela kwa namba hii...najuta
 
Unafanya makosa sana badala ya kulipa deni unatumia pesa inayoweza kupunguza deni ukaamua kulewea
 
Nilikuja kuwalipa baada ya miezi 6. Mwisho wa siku walipe tu alafu achana nao, wanakuwa na taarifaa zako nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…