Nimekoma walahi! Pilau la buku nimelinunua kwa 32,000 za dripu mbili

😀 😀 😀 @kalaga baho mkuu hilo pilau umekula wapi mana siku hizi pilau ni bei ya 5 elfu kwa jinsi ulivolisifia ila pole sana.
 
Yani uliishiwa Hadi nauli ila ukatoa 32 elfu ya kulipia Hospitali.
Uliitolea wapi akati uliishiwa kabisa ?.
Hongera Sana Kamanda.
 
Hali hii leo mbona kazi ipo!

Katika pitapita zangu maeneo flani flani hiv nikasikia sauti kutoka katika kipaza ikinadisha "pilau buku, pilau nyama buku... njoo ujipatie". Nikaona yesss, dunia ni yetu sote.

Nikajikoki pale ndizi ya mia mbili na juisi ya muwa. Nikaketi taratiibu nijipimie. Wallahi punde baada ya kujishindilia pilau la nazi nikasikia "prrr prrrr prrr" tumbo linaunguruma na maumivu kias.

Nikajaa kujishtukia niko mlangoni mwa choo cha msikiti mana hata nauli iliishia kwemye choo cha kulipia. Nikajimaliza pale vya kutoshana nguvu ikatoweka, nikaomba msaada wa pikipiki ya msikiti nikapelekwa hospitali. Hapa nilipo nina drips ya pili na nishamaliza elfu 32 kwa matibabu haya yanayoendelea

Dua zenu wazee
🤣🤣🤣🤣Pole jamani mara nyingi vya bei rahisi vina tu-cost
 
Pole sana Mkuu

Kuna wakati niliwahi kuugua tumbo la namna hiyo baada ya kunywa juicy kwenye Mgahawa Fulani hapo Masaki

Kutokea Siku hiyo, nimekuwa mwoga sana wa juicy.
 
Hali hii leo mbona kazi ipo!

Katika pitapita zangu maeneo flani flani hiv nikasikia sauti kutoka katika kipaza ikinadisha "pilau buku, pilau nyama buku... njoo ujipatie". Nikaona yesss, dunia ni yetu sote.

Nikajikoki pale ndizi ya mia mbili na juisi ya muwa. Nikaketi taratiibu nijipimie. Wallahi punde baada ya kujishindilia pilau la nazi nikasikia "prrr prrrr prrr" tumbo linaunguruma na maumivu kias.

Nikajaa kujishtukia niko mlangoni mwa choo cha msikiti mana hata nauli iliishia kwemye choo cha kulipia. Nikajimaliza pale vya kutoshana nguvu ikatoweka, nikaomba msaada wa pikipiki ya msikiti nikapelekwa hospitali. Hapa nilipo nina drips ya pili na nishamaliza elfu 32 kwa matibabu haya yanayoendelea

Dua zenu wazee
Pilau limetangazwa kwenye spika 😹

Pole sana mkuu.....
 
Siku zote ogopa saana kujiweka cheap huku unahonga ghali katika maisha yangu nina kanuni mbili popote nilipo nakula sehemu ya maana na kulala sehemu ya maana hasa nikiwa nasafiri
 
Shida sio hiyo pilau ni hiyo Juisi ya miwa.

Kati ya vitu siwezi kununua barabarani ni Juisi ya miwa. Ile kitu ni uchafu 85% nzi wanasagiwa sana huko
 
😀 😀 😀 @kalaga baho mkuu hilo pilau umekula wapi mana siku hizi pilau ni bei ya 5 elfu kwa jinsi ulivolisifia ila pole sana.
Pilau uswahilin ndo bei yake mpaka buku jero. Mm leo nimeona buku kamili nikasema siliachi mana hii ni promotion
 
Back
Top Bottom