Nimekosa ajira za ualimu tena

Pole sana nakwambia tz ingekuwa kama marekani kwamba unaingia tuu duka i na kununua bastola tungeuana kinoma
 
Ni wakati sasa wa kubadili mtazamo wa kuajiriwa. Karibu mtaani tupambane. Mwanzoni utapata changamoto ya kuitafuta njia ya kutokea!

Ila ukifanikiwa tu kuipata, basi maisha hugeuka kuwa mepesi sana! Tena kuliko hata hayo ya kuajiriwa.
 
Mimi nimeshangaa tu kitu kimoja hivi ukisema nafasi zimebakia na walioomba hawa kukidhi vigezo unamaanisha nini?

Je, taarifa zilizopo siyo sahihi au vyeti vilivyotumwa vina tatizo?

Kuna Course ya afya aliomba Dogo langu lakini nimeahangaa eti imechagua hapo watu 24 kati ya 200 na hizo nafasi 200 ziko wazi [emoji1][emoji1][emoji1][emoji23][emoji23]

Hii nchi ni ngumu, je waliotuma walitakiwa kukidhi vigezo gani?
 
Pole Sana Mzee,hapo jipange kivingine..

Mimi jamaa yangu kabahatika this time around,maana Ali Disco Mlimani kozi ya Uchumi mwaka 2012,baadae akajiunga chuo Cha ualimu akahitimu 2015 na Diploma ya masomo ya Sanaa.

Tokea amesugua bench mpaka akakata tamaa lakini nikamwambia aombe,miaka yote aliyoomba alikosa..

Leo hii nimeangalia nimeliona jina,kafurahi hadi kanywa pombe huko hasomeki..

Ila sasa namhurumia maana salary ya Diploma ni ndogo na Bodi ya mkpo itachukua chake haijalishi uli disco au laa..

Ila jamaa yangu alishaanza life lake kitambo,ana mke na watoto 2 na alishajenga nyumba ya kawaida na ana mifugo na Kazi za ufundi..

Sasa anatakiwa kuhama huku aliko na ni mjini aende kwa kina Mwigulu huko Vijijini.
 
Unataka aje kutuchamba?
Tuonee huruma Mkuu bado tuna maumivu ya kukosa ukimuita tena huyu anakuja kupigilia msumari kwenye kidonda ha!ha!
Si anajitoa tu ufahamu huyo, awachambe ilhali na yeye pia aliomba hizo Ajira....!?

Na dunia vile haijawahi kuwa Fair unakuta pamoja na kuikandia Sana kazi ya Ualimu lakini unakuta lenyewe ndio limepata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…