Nimekosa Mkopo benki kisa nilichelewesha rejesho mwaka 2018 kwa siku 60

Mnataka kuishi kama wananchi wa Dunia ya kwanza wakati mnalia kurudisha mkopo

HIYO NDIO MAANA YA CREDIT CHECK

itawaliza wengi

Mimi niliomba huduma ya Internet wakataka credit check ya phone bill wakakuta nilipitiliza siku 7, nikagomewa
 
Anha,kumbe ni CRDB tu nkajua benki zote. Sasa ina maana hao NMB hawana hyo taarfa yako? Au wao wameamua kupotezea

Anha,kumbe ni CRDB tu nkajua benki zote. Sasa ina maana hao NMB hawana hyo taarfa yako? Au wao wameamua kupotezea tu
Crdb ndo nilikutana na hiyo changamoto,sa sijui nmb walipotezea tuu ama laa ila nilienda nmb nikawauliza kwanza kabla sijaanza process wakaniambia hiyo mpya ndo wanaisikia kwangu,ikabidi nianze kuapply kwa kujaribisha tu nikafanikiwa
 
NB:Kwa wale mliotumia nida zenu kusajilia watu namba za simu nenda mkafute hizo namba.
Juzi tu hapa nilikosa mkopo bank kisa nadaiwa songesha nimewekwa kama mdaiwa sugu nikiangalia sijawahi kukopa kabisa'kuja kufatilia kumbe nilimsajilia dogo line na dogo alikopa songesha elfu 50 hakulipa deni.
 
Mikopo ya simu na bank vinaingilianaje mkuu,na what if nikibadili namba?
Hata kama uki badili namba. Wakati unakopa lazima ulimtumia vitambulisho vyako halali kama NIDA ni lazima, vitambulisho na barua toka kazini kwako. Kama hujaajiriwa utapeleka barua ya serikali za mitaa, leseni ya biashara nk. Unachomoka vipi hapo?
 
dawa ya deni ni kulipa tena kwa wakati
kuna mjinga mmoja alikopa songesha akatupa line bila kulipa
akareportiwa kwenye mamlaka husika, yuko blacklisted hawezi kopa popote. kipindi hicho alikuwa chuo
alipoajiriwa hawezi kopa
tulipe madeni tena kwa wakati. kama umekwama usikimbie, mjulishe mkopeshaji wako
 
Wakopeshaji wanajua na hata hapo Mimi nimeeleza vizuri tu. Wala sijawahi kimbia deni.

Ila system ya BOT hanijui hizo arrangement tunazofanya na wakopeshaji.
 
Vipi sisi ambao tunadaiwa na watoa huduma kama mamlaka ya maji, inatuhusu pia, sababu hapa napanga kuendelea kutowalipa bill ya maji waliyonitumia juzi 14,000+
 
Hiyo Lugha ya benki ni Lugha Laini ya kukataa kukupa mikopo polite language loan denial ili ujisikie tu vizuri kidogo kumbe wanachokuambia ni kuwa mbwa Wewe Huwa hulipi mikopo hatukupi ng'oo

Ila wanakujibu kisiasa tu

Ukikopa lipa Kwa Wakati usifikiri benki wanajikomba sana kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…