Nimeku "miss" kwa kiswahili

Nimeku "miss" kwa kiswahili

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Nwali nilidhani inaweza kuwa nimekukumbuka, lakini nahitaji msaada zaidi ili nisidhani tena
 
Unasema hivyo hivyo "nimekumiss".

Siyo lazima kila neno, sentensi, au msemo wa Kiingereza uwe na tafsiri yake ya moja kwa moja kwa Kiswahili.

Kama police ni polisi, judge ni jaji, schule (Kijerumani) ni shule...basi sioni ubaya miss isiazimwe kama hivyo hivyo ilivyo.
 
Kiswahili kina logic kubwa zaidi ya Kiingereza, kwa hiyo ukivilinganisha unaweza kukosea na kusema "Nimekumiss = nimekukosa" ukachekesha.

Ukishajua umemmiss mtu, tayari hujammiss, kwa sababu ushamfikiria.

Na ukimmiss mtu kikweli, hata humfikirii, kwa hiyo kuna haja gani ya kuwa na neno?
 
NN jana ulikuwa mkali sana na neno la kiingereza ifanyiwa modification, lakini neno la kiswahili kufanyiwa modification unaona poa tu. Hii tuiite nini?

cc Pasco
 
katika kinyakyusa kuna neno "nsukilwe". nsukilwe? sukilwe? whatever....
Kiswahili chake ni "nimekukumbuka sana."
literal translation huwaga haitakiwi kutumika kila wakati.
 
Kutafsiri hakuhusu maneno tu, kunahusu tamaduni nzima.

Muingereza akisema "I married my husband in 1983." ukaambiwa utafsiri sentensi hiyo Kiswahili utaitafsiri vipi?
 
NN jana ulikuwa mkali sana na neno la kiingereza ifanyiwa modification, lakini neno la kiswahili kufanyiwa modification unaona poa tu. Hii tuiite nini?

cc Pasco

Hapana ZeMarcopolo, umebugi meeen.

Bwana Paskali alichofanya jana ni marudio, yaani kurudia maneno yayo kwa yayo yenye maana ile ile kwenye sentensi moja.

Kwa Kiingereza tunaita 'tautology'

Mfano nilioutoa mimi hapo juu ni 'borrowing', yaani kuazima neno au maneno kutoka kwenye lugha moja na kutumia kwenye lugha ingine bila kubadili maana.

Kuazima huku kwa maneno ni jambo la kawaida sana katika medani za lugha. Hata Kiingereza kina maneno mengi tu kilichoazima kutoka lugha zingine kikiwamo Kiswahili.

Kwa hiyo mimi nilichofanya ni kupendekeza kuliazima tu hilo neno kama lilivyo na kulitumia kwa maana hiyo hiyo kama baadhi ya maneno mengine yaliyoazimwa toka lugha zingine.

Hivi unajua kwamba hata maneno 'dala dala' na 'matatu' sasa hivi yapo kwenye kamusi za Kiingereza za Oxford?

Na je, unajua kwamba shilingi ni shilling?
 
Miaka ya 90 kulikuwa na mtoto wa diplomat amerudi nyumbani alikuwa anatema English nzuri sana let call him A, kuna mwalimu wa English na yeye zamu yake, lazima hakuna kuongea Kiswahili, basi prefect akamkuta A kwenye mgahawa wa chai wakati wa vipindi, basi akamchukua A mpaka kwa mwalimu wa zamu, kufika kule, prefect anatafuta maneno ya kuongea A sikunyingi kashanyosha kuwa alikutwa chooni anajisaidia kwani ni kosa? Basi prefect alibaki 'are you jumping me infront of the teacher?'
 
Kiswahili kina logic kubwa zaidi ya Kiingereza, kwa hiyo ukivilinganisha unaweza kukosea na kusema "Nimekumiss = nimekukosa" ukachekesha.

Ukishajua umemmiss mtu, tayari hujammiss, kwa sababu ushamfikiria.

Na ukimmiss mtu kikweli, hata humfikirii, kwa hiyo kuna haja gani ya kuwa na neno?
Mkuu mchango wako nimeukubali, umeleta mkanasha mpya wenye maswali tele..kama kwel mtu wamfikiria manake hujammiss kwahiyo tujiulize zaid dhima ya neno kumiss linatumika kwenye muktadha gan?
 
uko juu NN

Back
Top Bottom