Nimeku "miss" kwa kiswahili

Nimeku "miss" kwa kiswahili

Lengo la kuwasiliana kila wakati ni kutafuta kueleweka. mashairi ya vijembe hueleweka kweli?

Mashairi ya vijembe yako wapi? Watu wameelewa string theory na Nostradamic quatrains itakuwa hayo unayoyaita "mashairi ya vijembe"?
 
Nani anelewa string theory na Nostradamic quatrains hapa. Kuna forum za abstract math tangu lini JF? Forum za molecular physics zimeanza lini hapa?
 
Swali siyo zimeanza lini. Swali ni hazijakuwepo lini?
 
Mi nadhani ina maana ya kua kuna baadhi ya mambo anayofanya umeyakosa hali ya kua hauko nae.Nahitaji msaada
 
Unapenda sana ku complicate issues. Tafakari....

Yawezekana wewe ndiye unayependa sana ku simplify issues.

Kama hapa, suala la ku complicate umeliweka kirahisi tu, bila kueleza wapi nime complicate na kivipi.

Sasa hapo mimi na complicate au wewe una oversimplify?
 
We Kiranga, ni watu wangapi wanaelewa string theory na Nostradamic quatrains. Kwanini usieleze tu kwa lugha rahisi tukuelewe.... Hebu anza na mimi kama kweli una lengo la kuchangia uzi. String theory na Nostradamic quatrains ndo nini? Ihusishe na hoja ya uzi inayosema Nimeku "miss" kwa kiswahili. Haya haya sema sasa. String theory na Nostradamic quatrains inaingiaje hapo
 
We Kiranga, ni watu wangapi wanaelewa string theory na Nostradamic quatrains.

Hata kama hamna hata mmoja anayeelewa hayo - which is not necessarily the case by the way, I have discussed Einsteinian "action at a distance spookiness" and virtual particles springing out of nowhere with Kuhani ana Mama here before-, bado hilo si la kumfanya Kiranga aache kuyataja. pengine inabidi yatajwe sio kwa sababu kila mtu anayajua, bali kwa sababu hamna anayeyajua. Hapo mchango wa Kiranga unaweza kuwa kuleta kitu kipya ambacho vijana wa miaka 14 mpaka 18 wanaochipukia kufuatilia mambo haya wajue hata cha kutafuta kusoma.

Kama wewe huna inquisitiveness ya kutaka kujua mambo usiyoyajua, hilo halimaanishi kila mtu kadumaa kama wewe.

Kwanini usieleze tu kwa lugha rahisi tukuelewe....

Unajuaje kama hiyo lugha niliyotumia si rahisi na unachotaka wewe ni kurahisishwa ambako hakupo kama vile kugawanya a Planck unit?

Hebu anza na mimi kama kweli una lengo la kuchangia uzi.

Kwa nini nianze na wewe? Kwa nini nitake kuanza na mtu ambaye ameshajidhihirisha kukumbatia kudumaa kimawazo?

String theory na Nostradamic quatrains ndo nini?

Kwa nini mimi ndiye niwe mualimu wa kukufundisha wewe? Niambie mpaka sasa ushafanya jitihada gani za kuelewa haya mambo kwa Google search, na umekwama wapi unapohitaji msaada.

Ihusishe na hoja ya uzi inayosema Nimeku "miss" kwa kiswahili.

Nishahusisha hapo juu, swali ni, je wewe unajua kusoma?

Haya haya sema sasa. String theory na Nostradamic quatrains inaingiaje hapo

Swali sio kwangu kwamba inaingiaje hapo.

Swali ni kwako kwamba haiingiaji hapo?

Hujagoogle definition tu ushataka kurukia mahusiano ya concepts hizi na thread?
 
Hata kama hamna hata mmoja anayeelewa hayo - which is not necessarily the case by the way, I have discussed Einsteinian "action at a distance spookiness" and virtual particles springing out of nowhere with Kuhani ana Mama here before-, bado hilo si la kumfanya Kiranga aache kuyataja. pengine inabidi yatajwe sio kwa sababu kila mtu anayajua, bali kwa sababu hamna anayeyajua. Hapo mchango wa Kiranga unaweza kuwa kuleta kitu kipya ambacho vijana wa miaka 14 mpaka 18 wanaochipukia kufuatilia mambo haya wajue hata cha kutafuta kusoma.

Kama wewe huna inquisitiveness ya kutaka kujua mambo usiyoyajua, hilo halimaanishi kila mtu kadumaa kama wewe.

Unajuaje kama hiyo lugha niliyotumia si rahisi na unachotaka wewe ni kurahisishwa ambako hakupo kama vile kugawanya a Planck unit?

Kwa nini nianze na wewe? Kwa nini nitake kuanza na mtu ambaye ameshajidhihirisha kukumbatia kudumaa kimawazo?

Kwa nini mimi ndiye niwe mualimu wa kukufundisha wewe? Niambie mpaka sasa ushafanya jitihada gani za kuelewa haya mambo kwa Google search, na umekwama wapi unapohitaji msaada.

Nishahusisha hapo juu, swali ni, je wewe unajua kusoma?

Swali sio kwangu kwamba inaingiaje hapo.

Swali ni kwako kwamba haiingiaji hapo?

Hujagoogle definition tu ushataka kurukia mahusiano ya concepts hizi na thread?

eeh...nimechoka sasa. kwa nini unanituma ku-google wakati wewe unayejua upo? si unieleze tu... haya sema sasa. String theory na Nostradamic quatrains ndo nini?
 
Kwa nini nikueleze?

Nikikueleza kwamba string theory ni kabila la Wagita wenye macho matatu waliopotelea kileleni mwa mlima Kilimanjaro na Nostradamic quatrain ni bendi zao za watu wanne wanne ambazo mara moja moja hutumbuiza Uhuru Peak utasemaje?

For a Highlander you have such a low inquisitiveness.
 
Nitaita mods sasa ivi ujue.... Hilo neno kwenye blu ni tusi ati.
 
jibu ni misi

nasema hivi as ndio neno nililolitumia maishani mwangu.

torch = tochi.
 
m - o - o - o - o - d - s !!!!

And your "moods" right now are funnier than the Golden Girls experiencing unexpected suitors -years after ceasing cramps- live on stage.

This wolf crying is diluting the case for those with a genuine case to raise to the mods.
 
Kutafsiri hakuhusu maneno tu, kunahusu tamaduni nzima.

Muingereza akisema "I married my husband in 1983." ukaambiwa utafsiri sentensi hiyo Kiswahili utaitafsiri vipi?

Kiingereza kina maneno mengi zaidi kuliko Kiswahili. Kuna maneno mengi tu ya Kiingereza ambayo maana zake unazijua vizuri kabisa lakini ukiulizwa utoe corresponding phrases/words zake kwa Kiswahili unashindwa wakati Kiswahili ndiyo lugha yako mama, same kama huyu aliyeuliza swali hapa!

Mimi ninavyoelewa mojawapo ya njia ya kukua kwa lugha ni kwa kuazima maneno kutoka lugha zingine, ila watu wa TUKI naona hawapendi sana kuazima maneno kutoka kwenye ligha hii ambayo inaonekana wazi kuwa ni pana zaidi kuliko kiswahili chetu. Ninavyoona mimi, kitu kama hakikuwepo kwenye mazingira yenu halafu baadaye kikawepo kikiwa kimekuja na jina lake, bora utumie hilo jina kililokuja nalo rathher than inventing a new name for it. Kwa mfano haileti maana kabisa ninapoingia kwenye website ya lugha ya Kiswahili halafu nataka ku-login sehemu naombwa password kwa neno linaloitwa NYWILA, likimaanisha password. Wazungu walivyokuja huko nyumbani kwetu unyakyusani walileta vitu vingi ambavyo hapo awali havikuwahi kuwepo mojawapo ikiwa ni kijiko, amabcho mpaka leo huwa tunakiita esipuni. Kuna tatizo gani kuita website as webusaiti na badala ya kuinvent maneno mapya kama wavuti ambayo wala hata hayaendani na kitu chenyewe? Anyway maoni yangu.
 
Mimi ningependa kweli kama kungewezeka hesabu halisi ya maneno ya kiingereza tukailinganisha na hesabu halisi ya maneno ya kiswahili.

Swali hili ni gumu sana hasa ukizingatia kwamba lugha zote mbili ni "lingua franca", zimechanganya na kutohoa kutoka lugha nyingine nyingi pamoja na vilugha/lahaja za himaya yazo. Kwa hiyo Kiswahili cha Mvita kinaweza kuwa na maneno ambayo hayapo katika kiswahili cha Barawa au Ngazija. Kipi ni kiswahili na kipi kidigo linaweza kuwa swali gumu.

Pengine tunafikiri tu kwamba kiingereza kina maneno mengi zaidi kwa sababu kina historia ndefu zaidi ya kuchapishwa na kimetapakaa dunia nzima, na hatujui maneno mengi ya kiswahili.

Ukiangalia kamusi ya kiingereza - angalau mimi nikiangalia- naona maneno mengi sana yanatumiwa katika vitabu na magazeti, watumiaji wa kiingereza walioelimika kwa kadiri, hususan wale ambao kiingereza ni lugha yao ya kwanza, wanayajua. Hili jambo hunipa matatizo mara nyingine ninapoandika kwa kutumia maneno ya kiingereza ambayo nafikiri kwa kiwango cha mtu anayejua kiingereza cha kubabia kama mimi ni ya kawaida tu, wengine wanaona naandika maneno magumu. Lakini hili laweza kuwa kwa sababu Watanzania wengi si waongeaji wa kiingereza kama lugha yao ya kwanza, na mimi mara nyingine hutaka kuweza uandishi kama wa mtu ambaye kiingereza ni lugha yake ya kwanza.

Lakini nikiangalia kamusi za kiswahili nagundua kwamba maneno mengi sana yanabaki kuwa kwenye kamusi bila kutumiwa katika kiswahili cha kawaida. Sitashangaa nikisikia kwamba kwa kila maneno mawili yanayotumika kila siku kwenye kiswahili, kuna nane mengine hayatumiki na ukiwauliza waongeaji wa kiswahili hawayafahamu.

Kwa hivyo narudi katika swali langu, je tunafikiri kwamba kiingereza kina maneno mengi zaidi ya kiswahili kwa sababu huo ndio ukweli wenyewe au kwa sababu hatukijui kiswahili vizuri?
 
Yawezekana kabisa Kiingereza kina maneno mengi zaidi ya Kiswahili kwa sababu Kiingereza, kwa jinsi inavyoonekana, kiko huru zaidi katika kuruhusu kuingiza kwenye msamiati wake maneno mapya ambayo hubuniwa na watumiaji wake pamoja na kuazima kutoka lugha zingine.

Sasa hivi maneno kama 'bling-bling' na 'staycation', ambayo kwa kweli ni maneno mapya, tayari yameshaingizwa rasmi hata kwenye kamusi.

Bofya hapa uone maana ya bling-bling na lini matumizi yake yalipoanza (1999).

Bofya hapa uone maana ya staycation na lini ilianza kutumika (2005).

Hata 'irregardless' lipo kwenye kamusi pamoja na maelezo yake kwamba si neno sanifu.

Sasa sisi taasisi zetu za lugha ni nzito sana katika kuongeza misamiati kwenye lugha yetu. Wenzetu wazungumza Kiingereza taasisi zao kila mwaka huwa walau zinatangaza maneno mapya ambayo yameingia kwenye msamiati.

Sidhani (na niko tayari kusahihishwa) kama TUKI ama BAKITA huwa zina utaratibu unaofanana na huo hata kwa mbali.

Mara zote huwa nasema lugha hukua endapo watumiaji wake wataikuza. Misamiati huwa haishushwi toka mbinguni au kuota mitini. Huundwa na watumiaji wa lugha husika.
 
Back
Top Bottom