Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Mimi ningependa kweli kama kungewezeka hesabu halisi ya maneno ya kiingereza tukailinganisha na hesabu halisi ya maneno ya kiswahili.
Swali hili ni gumu sana hasa ukizingatia kwamba lugha zote mbili ni "lingua franca", zimechanganya na kutohoa kutoka lugha nyingine nyingi pamoja na vilugha/lahaja za himaya yazo. Kwa hiyo Kiswahili cha Mvita kinaweza kuwa na maneno ambayo hayapo katika kiswahili cha Barawa au Ngazija. Kipi ni kiswahili na kipi kidigo linaweza kuwa swali gumu.
Pengine tunafikiri tu kwamba kiingereza kina maneno mengi zaidi kwa sababu kina historia ndefu zaidi ya kuchapishwa na kimetapakaa dunia nzima, na hatujui maneno mengi ya kiswahili.
Ukiangalia kamusi ya kiingereza - angalau mimi nikiangalia- naona maneno mengi sana yanatumiwa katika vitabu na magazeti, watumiaji wa kiingereza walioelimika kwa kadiri, hususan wale ambao kiingereza ni lugha yao ya kwanza, wanayajua. Hili jambo hunipa matatizo mara nyingine ninapoandika kwa kutumia maneno ya kiingereza ambayo nafikiri kwa kiwango cha mtu anayejua kiingereza cha kubabia kama mimi ni ya kawaida tu, wengine wanaona naandika maneno magumu. Lakini hili laweza kuwa kwa sababu Watanzania wengi si waongeaji wa kiingereza kama lugha yao ya kwanza, na mimi mara nyingine hutaka kuweza uandishi kama wa mtu ambaye kiingereza ni lugha yake ya kwanza.
Lakini nikiangalia kamusi za kiswahili nagundua kwamba maneno mengi sana yanabaki kuwa kwenye kamusi bila kutumiwa katika kiswahili cha kawaida. Sitashangaa nikisikia kwamba kwa kila maneno mawili yanayotumika kila siku kwenye kiswahili, kuna nane mengine hayatumiki na ukiwauliza waongeaji wa kiswahili hawayafahamu.
Kwa hivyo narudi katika swali langu, je tunafikiri kwamba kiingereza kina maneno mengi zaidi ya kiswahili kwa sababu huo ndio ukweli wenyewe au kwa sababu hatukijui kiswahili vizuri?
Kwa hiyo mimi nashauri ukubwa wa lugha tuungalie kwa kuzingatiaa maneno ambayo hasa watu walio wengi wanayajua na wanayatumia katika mawasiliano yao ya kila siku si uwingi wa maneno ndani ya kamusi. Yaliyo ndani ya kamusi yataendelea kutumika taratibu kwa ajili ya kuikuza lugha, ukizingatia kwamba Kamusi huwa inaandikwa na jopo la wataalamu wachache tu kuwakilisha lugha ya watu walio wengi ndani ya jamii husika.