Nimeku "miss" kwa kiswahili

Nimeku "miss" kwa kiswahili

Unasema hivyo hivyo "nimekumiss".

Siyo lazima kila neno, sentensi, au msemo wa Kiingereza uwe na tafsiri yake ya moja kwa moja kwa Kiswahili.

Kama police ni polisi, judge ni jaji, schule (Kijerumani) ni shule...basi sioni ubaya miss isiazimwe kama hivyo hivyo ilivyo.

Sasa mkuu! Tukilazimisha au kuliazima hilo neno kwa kiswahili liwe "nimekumiss" huoni kama tutakuwa tume "codemix" badala ya kutengeneza neno sahili kama SHATI kutoka neno SHIRT? Na ikiwa limekubalika liwe nimekumiss, semantically litakuwa na maana gani kwa lugha ya kiswahili?
 
Kutafsiri hakuhusu maneno tu, kunahusu tamaduni nzima.

Muingereza akisema "I married my husband in 1983." ukaambiwa utafsiri sentensi hiyo Kiswahili utaitafsiri vipi?

Hivi we Kiranga mbona kila siku maswali tu?! Saa ingine na wewe uwe unaleta solutions... siyo maswali tu. eeh!
 
Katika Socratic method hata solution italetwa kwa swali. Unaweza kuona swali katika jibu, na jibu katika swali.
 
Haya bwana, ingalau hapo umejaribu kuleta solution--hata kama ni kwa kutumia Confucius method.
 
Sasa mkuu! Tukilazimisha au kuliazima hilo neno kwa kiswahili liwe "nimekumiss" huoni kama tutakuwa tume "codemix" badala ya kutengeneza neno sahili kama SHATI kutoka neno SHIRT?

Kwani kuna ubaya gani tuki "codemix" kama unavyodai? Mbona sasa hivi tunafanya sana na bado tunaelewana tu. Kwani kwa mfano inaposemwa 'spika (speaker) wa bunge' kunakuwa hakuna codemixing? Au shule (schule - Kijerumani) ya sekondari (secondary), kunakuwa hakuna codemixing hapo?

Na ikiwa limekubalika liwe nimekumiss, semantically litakuwa na maana gani kwa lugha ya kiswahili?

Maana zinaweza zikawa kadhaa kulingana na muktadha kwani hata kwenye Kiingereza neno 'miss' lina maana tofauti tofauti kulingana na muktadha.

'Miss Becky Lindsey' sio sawa 'miss the boat'.

Na ili lugha ikue ni lazima watumiaji wake waikuze.

Ila, si lazima kila neno la msamiati wa hiyo lugha liwe linatokea kwenye lugha hiyo tu. Kuazima (na hata kufanyia modification za hapa na pale) kunakubalika kabisa.
 
Kwani kuna ubaya gani tuki "codemix" kama unavyodai? Mbona sasa hivi tunafanya sana na bado tunaelewana tu. Kwani kwa mfano inaposemwa 'spika (speaker) wa bunge' kunakuwa hakuna codemixing? Au shule (schule - Kijerumani) ya sekondari (secondary), kunakuwa hakuna codemixing hapo?

Maana zinaweza zikawa kadhaa kulingana na muktadha kwani hata kwenye Kiingereza neno 'miss' lina maana tofauti tofauti kulingana na muktadha.

'Miss Becky Lindsey' sio sawa 'miss the boat'.

Na ili lugha ikue ni lazima watumiaji wake waikuze.

Ila, si lazima kila neno la msamiati wa hiyo lugha liwe linatokea kwenye lugha hiyo tu. Kuazima (na hata kufanyia modification za hapa na pale) kunakubalika kabisa.

Ok. Ninakubaliana na wewe kwamba hakuna lugha iliyo jitoshereza ki msamiati/ki istilahi. Lakini nikukumbushe kwamba, maneno kama Speaker(spika) na schule(shule) ni maneno ambayo tayari yana simama yenyewe(na ukichunguza yapo katika kategoria ya Nomino. Na si vitenzi) sasa neno 'MISS' Kwa maana ya mleta mada, sidhani kama italeta mantiki katika vitenzi vya kiswahili tukiwa na neno
Ni-me-ku-'MISS' lenye mchanganyo wa lugha mbili tofauti katika neno moja. Labda ungesema liwe 'MISS'(Misi) kama yalivyo mengine na ilete maana kama mleta mada alivyo kusudia.
By the way sikusudii kukubishia. Ni katika kutafua vigezo vinavyo zingatiwa katika mchakato wa kuchukua maneno kutoka lugha zingine kwenda lugha nyingine.
 
uko deep
Kwani kuna ubaya gani tuki "codemix" kama unavyodai? Mbona sasa hivi tunafanya sana na bado tunaelewana tu. Kwani kwa mfano inaposemwa 'spika (speaker) wa bunge' kunakuwa hakuna codemixing? Au shule (schule - Kijerumani) ya sekondari (secondary), kunakuwa hakuna codemixing hapo?

Maana zinaweza zikawa kadhaa kulingana na muktadha kwani hata kwenye Kiingereza neno 'miss' lina maana tofauti tofauti kulingana na muktadha.

'Miss Becky Lindsey' sio sawa 'miss the boat'.

Na ili lugha ikue ni lazima watumiaji wake waikuze.

Ila, si lazima kila neno la msamiati wa hiyo lugha liwe linatokea kwenye lugha hiyo tu. Kuazima (na hata kufanyia modification za hapa na pale) kunakubalika kabisa.
 
kwa sasa hivi ukimwambia mtu yoyote nimekumisss ataelewa tu, lakini naona ingalikua vyema tungepata chetu
 
Back
Top Bottom