Nimekua disappointed sana na Mtu ambaye nilikua namuona wa thamani sana....ni week sasa Tangu nikutane na hio disappointment

Ni hatari Mimi Kuna mmoja nilijua badae ni snitch na ni mswahili ,nikafuta namba yake. Siku moja boss kaniambia nimpigie nimwelekeze majukumu /Kuna kazi alitakiwa afanye [emoji2][emoji2][emoji2] Nikamwambia boss sina namba yake .

Boss akastuka Kwa nini , nikamwambia jamaa Nina hasira nae nikiona jina na hata namba yake nazidiwa na hasira na hapa tunakutana tu Kwa sababu ni sehemu ya kupatia risk....tusingekuwa tunaonana .Bosi alimaliza Kwa kutatua mgogoro huo lkn mpaka Sasa tunaonana tu Kwa sababu ya kazi.
 
Kazini ni sehemu ya vita boss akikupenda wafanyakazi wenzako watakupiga vita na majungu na watakuchukia ukiwa mtu wa misimamo boss anakuchukia tokea nimuone mtu ana resigns mkataba wa permanent wa million 10 kwa mwezi mpaka leo sina rafiki kazini nikitoka kazini ni mishe nyingine nakaa mbali nao maana hata tukikutana nao mtaani story ni za kazi kwa hyo najitahidi kukaa nao mbali.
 
Francis Chacha Wambura
Kazi; Mkulima
Umri: 98
Wake: 6
Watoto: 47
Wajukuu: 86
Sababu ya kifo: uzee

Lazaro Olemgbe
Kazi: Seremala
Umri: 115
Wake: 11
Watoto: 56
Wajukuu: 132
Sababu ya kifo: Uzee.

Mabura Mabondo Matinde
Kazi: Tailor
Umri: 109
Wake: 4
Watoto: 38
Wajukuu: 73
Sababu ya kifo: Uzee

Dk Benson Ngonyani (Phd)
Kazi: Mhadhiri
Umri: 53
Mke: 1
Watoto: 2
Wajukuu: 0
Sababu ya kifo: shinikizo la damu.

Samweli Julius Mushi
Kazi: Meneja wa Benki
Umri: 47
Mke: 1
Watoto; 2
Wajukuu; 0
Sababu ya kifo; BP, Sukari

Erick Charles James
Kazi: Mwanasheria
Umri: miaka 43
Mke : 1
Watoto: 3
Wajukuu: 0
Sababu ya kifo: Msongo wa mawazo

Sisemi chochote. Ni juu yako kutoa tafsiri yako mwenyewe....[emoji40][emoji40][emoji40][emoji2097][emoji2097][emoji2097]

Hiyo ndio sababu watu wengi waliojiriwa wanakufa mapema kwasababu ya vita makazini.
 
Sasa si ufunguke tuone hiyo disappointment imekujaje...yawezekana ukiisema tutajua namna ya kusaidia au kujifunza

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…