Nianze kwa kucheka kwanza.
Hii stori naiandika kwa lugha isiyo Rasmi, lugha za kiujana ujana.
Wayback nlikuwa na mamiloo, alinipenda ye then mie nikausoma mchezo tukawa wapenzi. Tumeenda miezi kadhaa penzi likaanza kumiss, nikajaribu boost boost haikuwa ridhiki likafa Baada ya kukaushiana tu kila mtu akasepa na zake. Hii ni mwaka jana.
Mwaka huu mwanzoni wa mwezi Feb Binti akawa na shida na mie ndo ninaeweza kumsaidia, ilipigwa simu ya jamaa yangu na nlivopokea nkaisikia sauti yake, na kumtaja jina lake akabaki anashangaa nimejuaje kama ni yeye, but hivo naijua sauti yake na namna yake ya kuongea, akaeleza shida yake, nikamsaidia.
From that moment onwards, tukaanza wasiliana Tena kama zamani lakini sikuwa namzingatia sana maana ashasepa awali bila kuaga namie sikuwa bothered kuulizia nn shida.
This time kaja sikutaka muuliza what happened in our last relationship, anakuja na maswali ya kuniuliza indirectly kama nampenzi now namie jibu langu Niko single ili nijuee her next move. Kaja na bra braa kibaooo tu mie namsomea radar, penzi limeenda kiasi nikaanza ona red flags zisizoeleweka.
This girl is almost 3 years older than me so she is approaching her 30, Yuko desperate sana na mtoto but nyumbani anaogopa coz kwao ni familia flani hivi za dini dini sana.
Binti hayuko romantic kabisaa ,chatting zake ni boring hazikupi mood ya kuendelea kuchat nae, hanaga story sana BUT she is real a wife material kwa tabia zake, SHIDA inakuja Binti anaonekana anakaumimi au kauchoyo flani hivi as per mie na nlivolelewa naona hizo tabia siwezi endana naye
Mosi, hapendi kujihusisha na mambo ya kijamii, yeye anakasehem anaingiza Senti 5 sio haba, Kuna siku tunapiga story seriously ananambia ye hawezi hata siku Moja kuchangia sherehe yeyote Ile na sio kuwa hana Hela au laah hata akiwa nazo hatofanya hivo naye hataki sherehe yetu Ichangiwe na watu.
Duuúh nikaona hii Kali mie navopenda shughuli hivi ntaja mkwaza mtu au namwambia apeleke Hela ya mchango wa jambo fulan akapiga panga nije kumtia makofi Bure.
Pili, kuna siku nimemtext ... Hello my love kaja kunambiaa unajua mie dadako, nikaona huyu kaanza kutokuheshimu, nikamjibu ... So Then hakujibuu. Kakaa kimya we mie nikabidi nijishushe nikamtext umeshindajeee etc .
Tatu, nshasahauu mara ya mwisho nimeambiwa napendwa lini, ikumbukwe ye ndokanitaka namie kwa huruma zangu nikamfungulia lango Moja wazi la moyo ila akafikia tu seburen[emoji28][emoji28], on contrary mie ndo nimekuwa nagonganinsha sms za nakupenda, good night, good morning but she didn't respond na anaview status zangu nakupost shit zake. Leo kanipostia ... Vile unaenda kuomba msamaha alafu unakuta tayati Yuko kwa MAHUSIANO mapya.
Nne, ana ego ya kijinga kwake samahani ni ngumu kutamka I wonder if she becomes my wife huko nyumban itakuwaje au ni vile ananiona mdogo kwake.
Na kalivo kashenzi ukikaomba mchezo kanachekeaa tu au ndo hakajibu sms mazima utamkuta status kapost meme.. mwanamme tujjfunze kuwasaidia wapenzi wetu waafikie malengo Yao kuliko kudemand sex tu.
Nkakaona kajinga. Hajala hata 100 yangu, so at this point I have reached END OF THE ROAD. I have considered it as a Bad debts , not expecting to recover it.
Only those two failed attempts zimemtosha.
NIMEKUBALI KUACHWA.