Nimekumbuka Mikasa ya Calculus, Algebra na Trigonometry nimewaza kama nilisomea ujinga bila sababu za msingi

Nimekumbuka Mikasa ya Calculus, Algebra na Trigonometry nimewaza kama nilisomea ujinga bila sababu za msingi

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Hello JF,

Baada ya uchovu wa mishe fupi za Leo, nikiwa nimepitiwa na usingizi ndani ya matako ya mjapani nikawaza msoto wa kufundishwa ujinga Calculus Algebra na Trigonometry, plus econometrics kwenye uchumi, nikawa nafananisha kazi niliotoka kuifanya na pesa nilizopata na aina ya msoto wa hizo topics, nikawaza sawa hayo matako ya mjapani yanahusiana na hizo topics.

Sasa nikawaza inafaida gani nisome hizo topics wakati hata pikipiki tu hatuna uwezo wa kuziunda sasa je tunasoma kama mazombi au ndio nini sasa.

Mbona mjapani anasoma na anunda mahari kuna haja Gani sisi kuteseka na hizo sumu.

Africa ujinga ni mwingi sana

Tujirekebishe.

Calculus niliiweza na kuichukia.

Ni hayo tu

Wadiz
 
Hesabu nazipenda , nikiwa ndogo form two mzee aliniambia hesabu ni somo jepesi mno,akanitia moto kuwa kila topic ina opposite yake...

Kujumlisha...kutoa
Kuzidisha....kugawanya
Sehemu...desimali
Log...exponential
N.k

Advance

Integration... Differentiation
Etc

Chuo ni app zake tu...kwenye courses mbalimbali.
 
Kwani umekatazwa kuunda hizo pikipiki,huo no ujinga wako mwenyewe!
 
Either ni uvivu wa ku apply hizi hesabu kwenye kazi zetu za kila siku au hatukuelewa application zake. Hesabu zote ulizotaja zina application zake katika maisha ya kila siku. Ila wabongo tumeziweka pembeni.

Calculus kwa mfano unaweza kutumia kwenye mipango mbalimbali ya nchi. Unaweza kutengeneza equation ambayo uki plug-in number inakupa idadi ya madarasa unayohitaji mwakani, miaka 2, 3 ijayo etc. Lakini sisi tunasubiri ikifika january ndo tunaanza kukimbizana kama vile ni dharula.

Niwaombe tu mjifunze jinsi ya ku apply hizo hesabu katika maeneo tofauti katika kuleta tija kazini na lwenye biashara zenu.
 
Hesabu niliipenda sana ,sema na bahati mbaya ilinikataa . Japo anayepinga hesabu namuona mwehu. Hesabu ya muhimu sana.
 
Mkinga mmoja ambaye hata std hakumaliza, anapiga biashara yake safi ya viazi au mbao leo ni milionea!, mwenye LLB anapiga domo humu, Songea hapo watu wenye roho za kikatili wanamkata pumzi fighter mmoja wa maisha ambaye hata kuandika na kusoma hakujua, ila alikua tajiri wa kutosha, Tanzania tunakaririshwa vitabu huu ni ujinga mkubwa, wenzetu sasa nursery school watoto wanaanza kufundishwa programming na coding.

Sisi bado tunafundishwa kilimo cha kahawa Brazil!kinatusaidia nini? Zimbos pamoja na politicians wake wame F nchi, mfumo wao wa ELIMU ni top class, zimbos hadi leo kuingia UK ni entry na hawahangaiki sana kupata permits pale.
 
Hesabu nazipenda , nikiwa ndogo form two mzee aliniambia hesabu ni somo jepesi mno,akanitia moto kuwa kila topic ina opposite yake...

Kujumlisha...kutoa
Kuzidisha....kugawanya
Sehemu...desimali
Log...exponential
N.k

Advance

Integration... Differentiation
Etc

Chuo ni app zake tu...kwenye courses mbalimbali.
Balaa mademu na hesabu unajichotea tu kwenye jaba
 
Nadhani yawepo ila yasiwe ya lazima.

Kuna watu wanasema hesabu zinasaidia kufikiri 😂😂😂 sijawahi kuona how, kwasababu watoto wadogo hawasomi hesabu na wanao uwezo wa kufikiri.

Binafsi naamini kufikiri kunatokana na mazingira na sio hesabu.

Ajabu ni kwamba wanaosema hesabu zinasaidia kufikiri, wamefundishwa kuwa hesabu zinasaidia kufikiri na hawajawahi kufikiri kivipi hesabu zinasaidia kufikiri ikiwa watoto wanaweza kufikiri ilihali hata bafo hawajaanza shule.

Watu wengi wanachanganya uwezo wa KUFIKIRI na MAARIFA. Na watakuja hapa kunipinga wakiwa wamevichanganya, tuwasubirieni waje.
 
Tatizo ni wanaopanga hizo combinations. Kama umesoma EGM basi advanced mathematics ilokuwa ni kupoteza muda bure kwa upande wako.

Advanced mathematics ni tool kwa wanaenda kusoma Engineering na Physics. Kwakifupi ile pamoja na michoro ndio lugha ya kihandisi.
 
Hizo vitu ni muhimu sana kwenye uhandisi.

Bila hesabu hizo watu wasingeelewa chochote kwenye field za engineering.

Pia kwenye computer science na IT hesabu hizo zina umuhimu sana
 
Back
Top Bottom