Nimekumbuka Mikasa ya Calculus, Algebra na Trigonometry nimewaza kama nilisomea ujinga bila sababu za msingi

Nimekumbuka Mikasa ya Calculus, Algebra na Trigonometry nimewaza kama nilisomea ujinga bila sababu za msingi

Nadhani yawepo ila yasiwe ya lazima.

Kuna watu wanasema hesabu zinasaidia kufikiri 😂😂😂 sijawahi kuona how, kwasababu watoto wadogo hawasomi hesabu na wanao uwezo wa kufikiri.

Binafsi naamini kufikiri kunatokana na mazingira na sio hesabu.

Ajabu ni kwamba wanaosema hesabu zinasaidia kufikiri, wamefundishwa kuwa hesabu zinasaidia kufikiri na hawajawahi kufikiri kivipi hesabu zinasaidia kufikiri ikiwa watoto wanaweza kufikiri ilihali hata bafo hawajaanza shule.

Watu wengi wanachanganya uwezo wa KUFIKIRI na MAARIFA. Na watakuja hapa kunipinga wakiwa wamevichanganya, tuwasubirieni waje.
Hakuna somo linalosaidia kufikiri kama hesabu. Hata kama mtu hatatumia hesabu moja kwa moja, lakini kuzifahamu kunamfanya awe anafikiria kimantiki zaidi. Muunganiko wa Neurons kichwani unakuwa imara na sharp zaidi. Kwa maneno yako, hesabu zinaongeza uwezo wa kufikiri wakati masomo mengine yanaongeza zaidi maarifa.
 
Hello JF,

Baada ya uchovu wa mishe fupi za Leo, nikiwa nimepitiwa na usingizi ndani ya matako ya mjapani nikawaza msoto wa kufundishwa ujinga Calculus Algebra na Trigonometry, plus econometrics kwenye uchumi, nikawa nafananisha kazi niliotoka kuifanya na pesa nilizopata na aina ya msoto wa hizo topics, nikawaza sawa hayo matako ya mjapani yanahusiana na hizo topics.

Sasa nikawaza inafaida gani nisome hizo topics wakati hata pikipiki tu hatuna uwezo wa kuziunda sasa je tunasoma kama mazombi au ndio nini sasa.

Mbona mjapani anasoma na anunda mahari kuna haja Gani sisi kuteseka na hizo sumu.

Africa ujinga ni mwingi sana

Tujirekebishe.

Calculus niliiweza na kuichukia.

Ni hayo tu

Wadiz
Inawezekana mtoa maada wewe kazi yako haipo kwenye application ya hesabu ngumu ya kila siku. Unawezaje kujenga daraja au magorofa bila hesabu? Unawezaje kuweka umeme kwenye jengo refu bila hesabu na kiasi gani cha umeme kipite sehemu husika?
Kwa mwenzetu Marekani wanatumia hesabu kupata idadi ya watu kwa sahihi kuliko kutumia census (Matrices in Population).
Hebu fikiria daraja la mwalimu Nyerere unafikiri watu waliweka Cement na nondo bila kuungali bending na banking angle? Mambo ni mengi.
Hata mafundi maiko hutumia hesabu katika kujenga nyumba zetu hizi za kawaida.
 
Hesabu ina faida kijana, hapo ulipo tu siku zako zinahesabika za kukaa hapa duniani na jawabu analo aliyekuumba ndiyo maana unaona kama hujui/huoni faida ya hesabu..
 
Hakuna somo linalosaidia kufikiri kama hesabu. Hata kama mtu hatatumia hesabu moja kwa moja, lakini kuzifahamu kunamfanya awe anafikiria kimantiki zaidi. Muunganiko wa Neurons kichwani unakuwa imara na sharp zaidi. Kwa maneno yako, hesabu zinaongeza uwezo wa kufikiri wakati masomo mengine yanaongeza zaidi maarifa.
wanangu wa jakata hawatakuelewa kabisa.

Ila Mkuu kuna uhusiano gani kati ya kufikiri na ujanja (kwa ujanja siongelei uhuni bali uwezo wa kutambua jambo na wepesi na kulifanyia maamuzi nimble).
 
Tatizo ni wanaopanga hizo combinations. Kama umesoma EGM basi advanced mathematics ilokuwa ni kupoteza muda bure kwa upande wako.

Advanced mathematics ni tool kwa wanaenda kusoma Engineering na Physics. Kwakifupi ile pamoja na michoro ndio lugha ya kihandisi.
Mimi nimesoma EGM na advance mathematics imenisaidia sana chuoni kwenye field ya Architecture na kwa sasa Ni Registerd Architect bado naitumia hesabu katika ku calculate dimension,ratio,position,spacing,plot covergae,size nk nk nk kwahiyo EGM sijapoteza muda kusoma Mathematics
 
Mbona hesabu ndiyo life au hamjaona mambo ya cross multipication yanatumika wapi??
Squares na mistatili...
Area
Weight
Length
Width
Kg
mm
Litres
N.k
 
Back
Top Bottom