Nimekumbuka Mikasa ya Calculus, Algebra na Trigonometry nimewaza kama nilisomea ujinga bila sababu za msingi

Hakuna somo linalosaidia kufikiri kama hesabu. Hata kama mtu hatatumia hesabu moja kwa moja, lakini kuzifahamu kunamfanya awe anafikiria kimantiki zaidi. Muunganiko wa Neurons kichwani unakuwa imara na sharp zaidi. Kwa maneno yako, hesabu zinaongeza uwezo wa kufikiri wakati masomo mengine yanaongeza zaidi maarifa.
 
Inawezekana mtoa maada wewe kazi yako haipo kwenye application ya hesabu ngumu ya kila siku. Unawezaje kujenga daraja au magorofa bila hesabu? Unawezaje kuweka umeme kwenye jengo refu bila hesabu na kiasi gani cha umeme kipite sehemu husika?
Kwa mwenzetu Marekani wanatumia hesabu kupata idadi ya watu kwa sahihi kuliko kutumia census (Matrices in Population).
Hebu fikiria daraja la mwalimu Nyerere unafikiri watu waliweka Cement na nondo bila kuungali bending na banking angle? Mambo ni mengi.
Hata mafundi maiko hutumia hesabu katika kujenga nyumba zetu hizi za kawaida.
 
Hesabu ina faida kijana, hapo ulipo tu siku zako zinahesabika za kukaa hapa duniani na jawabu analo aliyekuumba ndiyo maana unaona kama hujui/huoni faida ya hesabu..
 
wanangu wa jakata hawatakuelewa kabisa.

Ila Mkuu kuna uhusiano gani kati ya kufikiri na ujanja (kwa ujanja siongelei uhuni bali uwezo wa kutambua jambo na wepesi na kulifanyia maamuzi nimble).
 
Mimi nimesoma EGM na advance mathematics imenisaidia sana chuoni kwenye field ya Architecture na kwa sasa Ni Registerd Architect bado naitumia hesabu katika ku calculate dimension,ratio,position,spacing,plot covergae,size nk nk nk kwahiyo EGM sijapoteza muda kusoma Mathematics
 
Mbona hesabu ndiyo life au hamjaona mambo ya cross multipication yanatumika wapi??
Squares na mistatili...
Area
Weight
Length
Width
Kg
mm
Litres
N.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…