Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Pole na hongera kwa maswahibu, bila shaka hilo ni jini lishakupenda kikubwa zidi kuomba Mungu kwa imani yako, usithubutu kwenda kwa waganga utazidi jiharibia au likuue kabisa...
% zote sahihi ndugu
 
Chai imeisha? Mbona wageni tumekaa tu bila kupewa updates zozote? Au jini kaisha fanya yake !


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilikuwa natesti zari tu. Huwezi jua mipango ya shetani kiongozi wangu


Hahahaha babu kweli bado mkuyati una kusaidia. ... ila huo mzigo sio wa kitoto sidhani kama utaweza kuuendesha. Inabidii uwe umeshiba haswa.
 
Hahahaha babu kweli bado mkuyati una kusaidia. ... ila huo mzigo sio wa kitoto sidhani kama utaweza kuuendesha. Inabidii uwe umeshiba haswa.
Usisahau ng'ombe hazeeki maini.
 
Habar zenu wadau. Naomba mnisaidie maana nipo njia panda sielew nifanye Nini.
Waswahili wanasema mficha maradhi Kifo humuumbua.
Mimi sitaki kusubiri Kifo kinikute. Ileweke nimekuwa humu JF kwa muda mrefu, Mara nyingi nimekuwa msomaji tu, wa matukio ya watu, pamoja na kujielimisha, Mara chache sana nimekuwa nikichangia mijadala pale inapobidi. Hii ndio thread yangu ya kwanza. Hivyo sijaandika kwa ajili ya kuburudisha/kumtisha mtu, ninachokiwasilisha hapa Ni ukweli mtupu. Lengo na madhumuni Ni kupata ushauri na msaada pale inapobidi.

***** ****** ******** ******** ******
Iko hv, Mimi Ni mfanya biashara mdogo ninaejishughulisha na uuzaji wa nguo za kiume katika sehemu Fulani hv hp jijini DSM. Kiufupi Nina maduka mawili ya nguo za kiume, hiyo ndio ajira yangu inayonifanya niishi hapa mjini. Sasa mnamo Tar 27 Dec ya mwaka Jana (2018)nipo ktk moja ya ofisi yangu na endelea na majukumu yangu ya kawaida, tena nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi mida ya Kama saa 7 mchana kuelekea saa 8 hv, alikuwa mteja ambae Ni mwanamke ( Alikuwa mrembo sana, mweupe Ana asili Kama ya kiarabu hv) ila rafudhi Ni yakipemba. Kama kawaida nikawa namsikiliza, akaniambia nimchagulie nguo nzuri anataka ampelekee mme wake, Yani shati na suruali.
Wakati naendelea kumchagulia nikawa namuuliza anavaa size gani? Akacheka akasema yupo Kama wewe, kwa kila kitu...Tena akaongeza na kusema nguo nitakazo zipenda Mimi hata yy atazipenda.
Nikawa namtania, nikamwambia kwa jinsi ulivyomzur hvy nataman mume wako niwe Mimi, akaniuliza Kweli? Nikamwambia hakuna mwanaume chini ya jua anaweza kukukataa msichana mrembo Kama wote tukacheka.
Zoezi la kuchagua nguo likaendelea tukafanikiwa kupata nzuri akazipenda. Tumezoea wabongo tunapenda discount, lkn kwake ilikuwa ni tofauti, akauliza nikiasi gani alipe, nikamwambia akalipia bila kuomba punguzo la Bei Kama tulivyozoea kwa wateja walio wengi. Wateja wa namna hii hutokea ila ni marachache sana, hvy nilifurah maana inakuwaga bingo unapata faida nzur.
Nikiwa namfungia hz nguo, aliniuliza...umeoa? Nikamwambia hapana akacheka akasema, nilijua tu...huwez kuoa mapema 7bu unapenda pombe na wanawake wa aina tofauti tofauti, kifupi we Ni mzinifu. Hii ya pombe ilinistua kidogo, amejuaje mm nakunywa pombe, ila sikutaka kumuonesha hadharani.
Akaniambia, Kuna sehemu anaenda hvy akirudi atauputia mzigo wake, ila nimuhifadhie, akaniuliza huwa nafunga saa ngapi? Nikamwambia, akaniomba namba ya simu Kama sitojali nimpe ili Kama atachelewa anijulishe nisije chelewa kufunga kwa 7bu yake. Nami sikuona Tatizo, kwanza Ni mteja lakini pia Ni mrembo sana[emoji847] Kama tunavyojijua sisi wanaume, basi nikampa namba, akaaga na kuondoka.
************
Hapo ndipo kizazaa kilipoanza. Hata hapa naandika thread hii, Sina amani kabisa. Kufika mida ya Kama saa mbili na robo usiku, sms ikaingia kwenye simu yangu.inasema "Zawadi niliyo kununulia umeipenda"? Mmmh, mm nikahisi itakuwa mtu kakosea namba, coz ilitokea namba mpya, baada ya Kama dk 10 hv, ile namba iliyotuma sms ikawa inanipigia, kupokea nasikia sauti ya msichana, akaniuliza...mbona hujajibu sms yangu hau unapenda zawadi yangu, nikamuuliza unajua unaongea na Nan?
Akasema ndio Ni Fulani (akataja jina langu), nikashangaa nikamwambia mbona hakuna mtu nilimwagiza zawadi akasema, Tena umechagua na kuzijaribisha mwenyewe Mara hii umesahau? [emoji849][emoji50] Akawa anacheka[emoji1787][emoji1787][emoji1787] akaniuliza umeshanikumbuka? Nikamwambia ndio...nikamuuliza umejuaje jina langu wakati sikumtajia, (Nilimdanganya jina) Mara nyingi Sina destruri ya kukwambia jina langu la ukweli mtu nisie mjua, Hilo likanishangaza...nikachekecha akili nikahis labda ameangalia kwenye tigo pesa maana nilimpa namba ya tigo, swali lililozidi kuniumiza akili anawezaje kuja dukani kwangu kuninulia nguo Ikiwa hanifahamu, wakat aliniambia Ni za mumewe?
Nikamuuliza si ulisema unampelekea mumeo? Akaniambia kwani wewe hufai kuwa mume wangu? Akiwa anacheka, akaendelea.....na si ulisema hujaoa au ulinidanganya? Nikabaki na kigugumiz nisiamini ninachokisikia, akaniambia nimeamua kukutunuku. Usiku mwema, nitakuja kukutembelea siku nyingine akakata simu. Nikabaki na maswali chungu nzima, kupiga ile namba ikawa haipatikan...baada ya hapo ndio vitimbi vilipoanza.

Itaendelea.......

NB: Nimechoka kuandika nitaendelea kesho ila kiukweli mwezenu nipo njia panda sielew, mwaka nimeanza na mauzauza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah pole sana mkubwa wangu jambo usilo lijua sikuzote nilazima likutatize ila kabla hujafikilia mbali sana hadi ukawaza kuwa kilicho tokea ni mkosi au Nuksi ......Waza hili kwanza "Wewe ni mfanya biashara na ukweli unafahamika na watu wengi sana kuliko unao wafahamu wewe huyo binti huenda akawa anakufahamu vizuri kuliko unavyo fikili kwakua ukiwa unapenda au kuitaji kitu ambacho kinaitaji mbinu kukipata nilazima utakifuatilia sana ili pengine ujue mazaifu yake au mapungufu ...............Mtazamo wangu huwenda binti anajalibu kutafuta namna ya kufanya uwe nae.!!!!!
 
Daah pole sana mkubwa wangu jambo usilo lijua sikuzote nilazima likutatize ila kabla hujafikilia mbali sana hadi ukawaza kuwa kilicho tokea ni mkosi au Nuksi ......Waza hili kwanza "Wewe ni mfanya biashara na ukweli unafahamika na watu wengi sana kuliko unao wafahamu wewe huyo binti huenda akawa anakufahamu vizuri kuliko unavyo fikili kwakua ukiwa unapenda au kuitaji kitu ambacho kinaitaji mbinu kukipata nilazima utakifuatilia sana ili pengine ujue mazaifu yake au mapungufu ...............Mtazamo wangu huwenda binti anajalibu kutafuta namna ya kufanya uwe nae.!!!!!
Umewaza kwa kina sana mkuu hongeraa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba hiyo ni Live na siku nikiwa ofisin sina hata hela ya lunch ghafla Tigopesa inasoma..yani mbwa hawa wanajua kila kitu, mkibishana kwenye sms au ukimletea jeuri siku nzima inaharibika..hata ukiwa bar nilikua nahisi napigwa viwembe na kunyolewa nywele yani nakua uncomfortable mpaka naacha kunywa pombe, kumwambia mtu siwezi yani aarrghhh zile heka heka hapana kwakweli mpaka nikiwa club namuhisi basi naanza kumtukana kwamba flani acha mambo ya kis** nge maana sometimes unahisi **** inashikwa livee!

Schizophrenia is characterised by thoughts or experiences that seem out of touch with reality, disorganised speech or behaviour and decreased participation in daily activities. Difficulty with concentration and memory may also be present.
Treatment is usually lifelong and often involves a combination of medications, psychotherapy and coordinated speciality care services.
 
Huwa napata tabu kumuelewa kijana tena anaejitanabaisha kuwa wa kiume..

kwanza, akitumia emoji katika maandishi yake

Pili, kukatisha maneno eti '7bu'..sasa hako ndio kakitunguu swaumu gani?

Anyway..hapo njia panda unafanya nini saivi? Au ndio unakula mavitunguu swaumu ili uje uendelee?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom