Habari zenu wanajamvi, kipekee kabisa nipende kuwashukuru, kwa michango yenu katika ushauri juu ya tatizo lililo nikumba. Pia, namshukuru Mungu naendelea vyema kabisa, ingawaje vita ni kubwa mno...kwa sasa nimeshauriwa nisiseme chochote (sio kwa ubaya) ila ni kwa ajili ya usalama wangu pia.
Kwa wale wenye hofu na wasiwasi mm ni mzima wa afya... Ingawaje kumetokea mambo mengi sana ya kunirudisha nyuma, ikiwa ni pamoja na matapeli waliochukulia tatizo langu kama fursa. Nimepoteza pesa nyingi sana katika kutafuta suluhu la jambo langu, lakini nikiri wazi Mungu aliejuu mbinguni ashindwi na kitu, naamii atarejesha kila nilichopoteza.
Kwa sasa nimefunga biashara zangu zote (kwa muda) ili niokoe maisha yangu. Kwa sasa nipo kambini na timu ya maombi sehemu fulani (nisingependa kupataja) wananifanyia huduma. Kiukweli kabisa Vita ni kubwa mno Mama yangu kaponea chupu chupu kumpoteza.
Pia niwaweke wazi katika hili...mimi ndio msaada mkubwa katika familia yangu, matatizo haya yamesababisha ni yumbe sana kiuchumi. Hapa nilipo sina chochote (fedha) timu ya maombi inakesha usiku na mchana kunipigania..ukweli ni kwamba kama si nyinyi wana JF kunisisitiza ishu ya maombi nisingekuwa hai sasa. Naomba muendelee kuniombea pia.
Nashindwa nisemeje lkn najisikia aibu na fedhea kubwa kwa watu wanaopigania maisha yangu kushindwa kuwahudumia hata chakula na maji. Sio malipo kama wengine walivyohitaji ni bure kabisa ila hawa nao pia ni binadamu. Kama kuna yoyote ataguswa katika hili naomba aje Pm nitampa utaratibu aweze kunichagia chochote alichonacho (Nisieleweke vibaya tafadhali) kama utaguswa katika hilo naamini kabisa Mungu hatukuacha kama ulivyo ulipotoa atakuongezea mara dufu.
Nawashukuru sana kwa msaada wenu wana Jamii Forum. Niwatakie mchana mwema.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using
Jamii Forums mobile app