Sawa
Mimi kudanganya kuhusu maisha yangu kunahusiana nini na hii mada inayohusu jamii kwa ujumla hebu jibu hayo maswali acha kukwepa hoja, endelea kushusha hayo magazeti yako ili nikudhalilishe ijulikane nani mweupe kichwani, mbona umekimbia mada umejificha kwenye kichaka cha hiyo comment yangu kama kweli unajiamini una hoja si urudi kwenye mada au vipi
Oohh kwahiyo hiyo kwa mujibu wa hiyo kanuni yako ni kwamba siku baba akitetereka kiuchumi, na mama akalazimika kusukuma gurudumu mpaka baba atakapokaa sawa, maana yake kwa kipindi hicho baba atatakiwa kumtii mama si ndio
By the way unasahau kwamba huko kwa wenzetu mke hawajibiki kumtii mume na hakuna mgawanyo wa majukumu yeyote ana wajibu wa kufanya jukumu lolote, kwahiyo huko 50/50 haipo kwenye kulipa bills tu bali ipo hadi kwenye kazi za nyumbani na malezi ya watoto, na kama mnaweka housemaid yeye ndio atafanya majukumu yote ya nyumbani ili mume na mke wasaidiane majukumu ya kiuchumi tu
Na hutasikia mwanaume akilalamika kuwa eti mke wake kajisahau kazi zote kamuachia dada na wala hawafikii hatua ya kutembea na hao wadada kwa sababu hiyo, lakini huku afrika ambako hadi leo wanaume wanapenda kunyenyekewa, kupikiwa na kufuliwa na wake zao na wanaona kwamba kazi za nyumbani haziwahusu kabisa
Msitegemee wanawake wataikubali hiyo 50/50 ya kwenye kulipa bills kwa sababu hata ninyi hamuwasaidii majukumu yao, kwahiyo msiwalaumu kwamba hawawezi kuwasaidia yenu siku mtakapokubali kuacha kupenda kunyenyekewa, na mtakapokubali kuyachukulia majukumu ya nyumbani na malezi ya watoto kama wajibu wenu
Basi nawahakikishia hata wanawake nao wataanza kulichukulia serious hilo suala la kulipa bills 50/50, yani kwa kifupi hiyo 50/50 isiwe applicable kwenye majukumu ya mwanaume tu bali hata ya mwanamke pia kama huko kwa wazungu, ila tatizo linakuja wanaume ndio hamko tayari kufanya majukumu ya wanawake yani unataka wewe ufanye majukumu yako tu ila mwanamke afanye majukumu yako pamoja na yake hapo ndipo wanawake wanapogoma