Nimekutana na skin walker usiku wa kuamkia leo. Alikuwa binadamu, akageuka kuwa mbwa

Nimekutana na skin walker usiku wa kuamkia leo. Alikuwa binadamu, akageuka kuwa mbwa

Pole sana, itakuwa ndiyo mara yako ya kwanza? By the way havizoeleki hivyo, dunia hii haikaliwi na binadamu tu, ina Kila aina ya viumbe ambavyo hutokuja hata kufikiri kuwa wapo, hutokuja kuamini Hadi uwaone mwenyewe. Wako viumbe wako kwenye dimensions na frequencies mbalimbali tunaishi nao tu mitaani. Wengine ni shapeshifters unakutana nao baa, sokoni, stendi nk..haya mambo daima huwezi kuamini Hadi uyaone na pia, ni kama mazingaombwe vile. Usipende kupigapiga hovyo wanyama na watu usiowajua...Poleni itakuwa mmeogopa sana, ubaya ni kuwa We are not capable of comprehend or accept the truth of existence.
 
Siku zote mwenda wazimu huona wazima hawana akili!
IMG_20240922_035102.jpg
 
Viumbe wa hivyo wapo na kwenye cctv unaweza kuwaona. So poleni sana. Najua itamchukua mda kutoka akilini
 
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay.

Mwanga wa eneo la maegesho tulikiwa mkali, tukiwa umbali wa kama Meta kumi kutoka kwenye gari, tuliona mwanaume mwenye kama urefu wa futi SITA amesismama wima kwenye mlango wa nyuma wa gari yangu.

Wote tukiwa tumemkazia macho, alageuza pozi akawa kainama kama anafunga kamba za viatu, mara akageuka kuwa mbwa, na kutokomea. Wote tukapigwa na mshangao.

Mke wangu akaogopa kabisa hata kuingia kwenye gari, akawa anaogopa hata Sauti za mawimbi ya bahari.

Nikajaribu kumtuliza lakini kiwango chake cha taharuki kikawa juu sana, hadi walinzi ikabidi waje kujua kuna Nini?

Nikawaelezea tukio, wakabisha, wakasema twende kwenye CCTV camera kuangalia footage.

Basi wakaridisha video ya eneo like, na wenyewe wakaona hakika kilichotokea.

Tukajaribu kuomba copy ya kipande hicho cha video tumekataliwa.

Lakini hakika ukistaajabu ya Musa, utayaona ya uncle Firauni.
...Yaani Walinzi washuhudie wenyewe Kisha wakunyime copy ya clip hiyo inayoonyesha Nini ?? Sababu Yao Nini ? Wanamlinda Jini ???...Au story nzima ni Uongo TU ??
 
Back
Top Bottom