Nimekutana na Wanandoa wenye tarehe ya kuzaliwa inayofanana

Siku kadhaa zilizopita, kuna wanandoa wawili walikuja kupata huduma ofisi ninayofanyia kazi. Katika huduma hiyo kuna fomu walitakiwa kujaza kila mmoja, na kulikuwa na k kipengele cha kuzaja tarehe ya kuzaliwa.

Baada ya kuzipitia fomu hizo, nilipofika kwenye kipengele cha trehe ya kuzaliwa nikaona wote wamejaza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa vikiwa vina fanana.

Nikafikiri, labda mmoja wao amekosea akajaza tarehe ya mwenza wake kwa bahati mbaya. Lakini walinihakikishia kuwa hawajakosea, vile walivyojaza ndivyo ilivyo.

Katika kuhakikisha juu ya jambo hilo walinionyesha na vyeti vyao vya kuzaliwa. Vyeti ambavyo walitengenezewa na wazazi wao wakati wao wakiwa bado wadogo.

Nilijaribu kufikiria kuwa huwenda vyeti hivi wangevishughulikia/kuvitengeneza wenyewe wakiwa watu wazima, labda wangeweza kuweka tarehe za kufanana ili kijitengenezea "coincidence"

Ukweli nilistaajabu. Je, na wewe umewahi kukutana na "coincindence" ya aina hiyo? Au nyingine yoyote? Tushirikishe tafadhali.
Hata kufa watakufa pamoja
 
Ajabu iliyonitokea kuna mwaka nilisafiri
Nikiwa lounge nikisubiri mda kuna mzee alikuwa amekaa karibu
Kwa mda ulikuwa ni mrefu sikuweza kusahau sura yake

Miaka miwili baadae sehemu ile tena nikalutana na yule mzee
Nilishtuka sana na kujiuliza je siku ziliganda? [emoji23][emoji23]
Hii huwa inatokea kwa mambo mengi sana. Binafsi imenitokea kwa mazingira matukio na matamshi

Nimewahi kuokota hela (sh mia) sehemu ileile kiasi kilekile mkao wake ardhini uleule safari ni ileile nilikuwa nikienda shule asubuhi asubuhi sana

Kwenye mazungumzo si mara moja unakuta tunazungumza jambo na washkaji lakini kuna vipande vya mazungumzo vinajirudia kwa namna ileile ya siku nyingine kabla

Nafikaga baadhi ya sehemu halafu nashangaa kukuta eneo fulani linafanana kila kitu na eneo lingine la nyumbani mfano nimewahi kwenda sehemu fulani nikakuta barabara fulani kama ya kwetu mbaya zaidi mpaka kwenye kona kulikuwa na kibanda cha mangi na penyewe nikakuta mtu kama yule yule japo walitofautiana kiasi fulani
 
Ajabu iliyonitokea kuna mwaka nilisafiri
Nikiwa lounge nikisubiri mda kuna mzee alikuwa amekaa karibu
Kwa mda ulikuwa ni mrefu sikuweza kusahau sura yake

Miaka miwili baadae sehemu ile tena nikalutana na yule mzee
Nilishtuka sana na kujiuliza je siku ziliganda? [emoji23][emoji23]
Deja vu
 
Siku kadhaa zilizopita, kuna wanandoa wawili walikuja kupata huduma ofisi ninayofanyia kazi. Katika huduma hiyo kuna fomu walitakiwa kujaza kila mmoja, na kulikuwa na k kipengele cha kuzaja tarehe ya kuzaliwa.

Baada ya kuzipitia fomu hizo, nilipofika kwenye kipengele cha trehe ya kuzaliwa nikaona wote wamejaza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa vikiwa vina fanana.

Nikafikiri, labda mmoja wao amekosea akajaza tarehe ya mwenza wake kwa bahati mbaya. Lakini walinihakikishia kuwa hawajakosea, vile walivyojaza ndivyo ilivyo.

Katika kuhakikisha juu ya jambo hilo walinionyesha na vyeti vyao vya kuzaliwa. Vyeti ambavyo walitengenezewa na wazazi wao wakati wao wakiwa bado wadogo.

Nilijaribu kufikiria kuwa huwenda vyeti hivi wangevishughulikia/kuvitengeneza wenyewe wakiwa watu wazima, labda wangeweza kuweka tarehe za kufanana ili kijitengenezea "coincidence"

Ukweli nilistaajabu. Je, na wewe umewahi kukutana na "coincindence" ya aina hiyo? Au nyingine yoyote? Tushirikishe tafadhali.
Una tabia mbaya, nitachukua hatua dhidi yako.
 
Mbona ni kawaida tu, nilishakutana na dada mmoja tumeshare tarehe moja 26 Decmber, tukaishia kuitana pacha...tulvyomalizana kila mmoja akashika njia yake

Na ukimkuta wa hvyo ni kugusa tu unakula mzigo, manzi anahisi kuna cha tofauti au ajabu kumbe ni coincidence tu ya kawaida..
 
Mimi na wife pia tunafanana tarehe na mwezi wa kuzaliwa tofauti ni mwaka tu.

Wote tumezaliwa tarehe 7/04
Na kingine tunafanana alama za mikono yote
Kihusu alama za mokono, je mko group moja la damu?
 
Back
Top Bottom