Huo siyo utanashati,ni majivuno,maringo na dharau mkuuWakuu nadhani mko poa,kama kichwa cha habari kinavyojieleza,nimekuwa mtanashati mno hadi naonekana kero kwa watu wangu wa karibu nini nifanye ili nijiepushe na hali hii ???
Kama ujanipata hebu ngoja nikupe mfano wa ninachokieleza,nikisalimiana na mtu kwa kushikana mikono,basi siwezi kuvumilia bila kujifuta na kitambaa au kwa kunawa maji tena wakati mwingine hata mbele za wale nilioshikana nao mikono kiasi cha kwamba wananiona na wanamaindi na wale wanaonijua huwa hawanipi mikono kwa kuniona kama naringa hivi.
Hilo la kupangusa mikono tena kwa kuibia ni kawaida na majority wanafanya!! Lakini kunawa mikono kabisa ni total embarrassment kwa muhusika kama anakuona!Kujifuta mikono ninayo na huwa inakuja automatically tu.na si kwamba nafuta mpaka basi. Ni lazima nipanguse kwenye Nguo kidogo hapo ntakuwa na Amani. Na wakati nafanya hivyo hata alonipa mkono hawezi hisi chochote kwani nafanya kwa akili.
Ila hiyo ya kunawa sijawahi.
Sijui nifanyaje ili niiache hii tabia,maana huwa najihisi kama nimeubeba uchafu mikononi mwangu miaka 10 ?? Na huu wa mikono ni moja kati ya mambo mengi ya ninayoambiwa kuwa nimekuwa "mtanashati mno" wakati mimi mwenyewe najiona niko poa tu.Kujifuta mikono ninayo na huwa inakuja automatically tu.na si kwamba nafuta mpaka basi. Ni lazima nipanguse kwenye Nguo kidogo hapo ntakuwa na Amani. Na wakati nafanya hivyo hata alonipa mkono hawezi hisi chochote kwani nafanya kwa akili.
Ila hiyo ya kunawa sijawahi.
Kunawa maji ni kama nipo na maji karibu,lakini kiujumla nina tabia ya "utanashati iliyopitiliza" kama mkuu chige alivyotoa ushuhuda kwa mama yake basi nami niko hivyo,yaani hadi my wife wangu huwa namkera mno.Kwa hiyo unatembea na bobo la maji masaa yote kwa ajili ya kunawa siyo?
Hata kama ni kitambaa unatumia kujifutia huo siyo utanashati ni usharobasha, subiri wataalamu watakuja kukuelezea vyema!
Poa,japo kuna kipindi nilijaribu kama wiki hivi nikachemka nikajikuta nimerudia bila ya kujijua.Kweli unaringa...Jirekebishe, we nakupa mkono tunasalimiana halafu unaenda kuuosha au kujifuta kama sio dalili za DHARAU ni nini sasa?? JIREKEBISHE MKUU...Utanashati hauko hivyo!!